Kuna watuhumiwa wafanyakazi wa swissport wamefikishwa kituo cha polisi cha airpot kwa kupatikana na mzigo wa simu za mikononi zilizotokea dubai na kushindwa kupokewa hapo airpot na mwenye mzigo huo, wizi huo ulitoke tarehe 5 mwezi huu muda wa saa nane na nusu usiku kutoka dubai kwa ndege ya ethiopia, mlalamikaji ambaye ameibiwa mizigo hii yenye thamani ya 20,000000/= amesema alikuwa anazungushwa kipindi chote hiki kwa kuambiwa mizigo yake iko ethiopia na mwisho wakamwambia aendelee kusubiri watawasiliana nae, kwa kipindi hiki chama cha wauzaji simu za mkononi walijitolea kufanya kazi ya polisi jamii na hatma yake jana usiku saa nane mthumiwa anaejulikana kwa jina la mohd mfanyakazi wa swissport alipatikana na mzigo huo nyumbani kwake.