Mfanyabiashara afanya kufuru

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Aua naye ajiua

Mfanyabiashara Rodrick Mbwilo wa jijini Mbeya amemuua kwa kumchinja mtoto na kumjeruhi mwingine kwa kisu na baadaye kujiua mwenyewe kwa kujinyonga kwa kamba ya manila.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana katika maeneo ya Itua kando ya reli ya Tanzania - Zambia (Tazara), umbali wa kilometa tatu kutoka katikati ya Jiji la Mbeya.
Mtoto aliyeuawa katika tukio hilo ametajwa kuwa ni Kalebu Andrea anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 5 na 7 ambaye alikuwa mwanafunzi wa chekechea katika shule ya Baby Flower Nusery.
Mtoto aliyejeruhiwa kwa kukatwa na kisu nyuma ya shingo na kuchanwa vibaya usoni, ni Joshua Andrea (4), ambaye ni mdogo wake Kalebu.
Waandishi wa gazeti hili jana walifika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo na kushuhudia umati wa waombolezaji.
Mdogo wa mfanyabiashara huyo, Maskat Mbwilo ameliambia gazeti hili kuwa mtoto aliyeuawa pamoja na aliyejeruhiwa ni ndugu wa tumbo moja ambao ni wa shemeji yake ambaye ni mdogo wa mke wa mfanyabiashara Rodrick.
Alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, kulikuwa na mgogoro baina ya marehemu na mkewe.
Imedaiwa kuwa mke huyo alikuwa amekwenda mahakamani ili apewe talaka, kitu ambacho anahisi kinaweza kuwa chanzo cha marehemu kuchukua uamuzi huo mzito.
Alisema kutokana na mgogoro huo, Rodrick alijaribu kujinyonga, lakini watu waliwahi kumuokoa kwa kukata shuka alilokuwa amelitumia kujitundikia kwenye kenchi la nyumba chumbani kwake.
Alisema walijaribu kuingilia kati kusuluhisha mgogoro huo, hadi wakafikia kwenda kwa wakwe wa marehemu huko Kiwira, lakini jitihada zao hazikuzaa matunda baada ya marehemu kukataa kwenda ukweni ili kutafuta suluhu.
Alisema juzi wakati yeye na ndugu wengine wakiwa wamekwenda Kiwira, marehemu aliwachukua watoto wanne na kuwapakia kwenye gari kisha akatoweka nao kusikojulikana.
Alisema miongoni mwa watoto hao, wawili walikuwa wa kwake wa kuzaa na wawili walikuwa watoto wa shemeji yake (mdogo wa mke wake).
Kwa mujibu wa Maskat, kaka yake alizungumza na baadhi ya ndugu zake kwa njia ya simu juzi saa 10 jioni, ambapo aliwaeleza kuwa ameamua kujiua kutokana na matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yakimkabili.
Hata hivyo, aliwadanganya kuwa wakati huo alikuwa maeneo ya Kawetele, wakati yeye alikwenda eneo tofauti kabisa, hali ambayo ilisababisha shughuli ya kumtafuta kuwa ngumu.
Alisema jana hiyo walitoa taarifa Polisi na shughuli ya kumtafuta ikaanza, wakielekea huko maeneo ya Kawetele ambako hawakumpata na badala yake Polisi walipata maiti ya mtu mwingine aliyekuwa amejinyonga.
Alisema ilibidi warudi mjini na kwenda katika ofisi za mtandao wa Vodacom, kwa ajili ya kujua simu yake (Rodrick) ilikuwa ikipatikana katika maeneo gani ya Jiji.
Alisema wakiwa huko katika ofisi ya Vodacom, walielezwa kuwa simu ya marehemu wakati huo ilikuwa inapatikana maeneo ya Ihyela na ndipo walipobadili mwelekeo na kuelekea huko ambako ilipofika saa 3 usiku walifanikiwa kulipata gari la marehemu alipokuwa ameliegesha.
Alisema walipotafuta zaidi maeneo ya jirani na mahali lilipokuwa limeegeshwa gari, walifanikiwa kuupata mwili wa mtoto aliyeuawa na baadaye mtoto aliyejeruhiwa kabla ya kuingia bondeni zaidi walikofanikiwa kuupata mwili wa marehemu uking'inia juu ya mti.
Alisema wakati wakiwa huko porini, majira ya saa 12 jioni mtoto mmoja kati ya wanne walioondoka na marehemu kwenye gari, aitwaye Richard alirejea nyumbani na kuwaeleza watu kuwa baba yake alikuwa amemuua mwenzake aitwaye Kalebu.
Alisema yeye alinusurika kifo baada ya kumtoroka na kutimua mbio kurudi nyumbani, huku akimwacha baba yake akiendelea kuwaua watoto wenzake.
NIPASHE lilifanikiwa kuzungumza na mtoto wa marehemu aliyenusurika kuuawa, Lilian, ambaye pia ni mwanafunzi wa chekechea katika shule ya Babyflower, ambaye alisema alishuhudia jinsi baba yake alivyomuua mwenzake.
Alisema baba yake alimchinja Kalebu, akamkata shingo Joshua kisha akamchukua yeye na kumpeleka njiani, ambako alimweleza kuwa mama yake atamkuta hapo, kwa kuwa yeye (baba yake) alikuwa anakwenda kufa.
"Baba alianza kwa kuchinja Kalebu, nikaona anamkata shingo Joshua damu zikatoka, alipokuja kwangu hakunikata, akanichukua hadi njiani akaniambia mama atanikuta hapa eti yeye anakwenda kufa," alisema Lilian.
Alisema akiwa hapo njiani, alipita mtu mmoja mwenye baiskeli akamchukua na kumpeleka katika kituo kidogo cha Polisi cha Ilma, ambako jana asubuhi ndugu zake walifika na kumchukua.
NIPASHE lilipowasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alisema hana taarifa za tukio hilo na kuwa angelitolea taarifa baadaye baada ya kufuatilia au litakapofikishwa ofisini kwake.
Maskat alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa, Mbeya ambako pia mtoto Joshua alikuwa amelazwa kwa matibabu.
Jana mchana mwili wa mtoto Kalebu ulichukuliwa na ndugu zake na kupelekwa wilayani Mbozi kwa ajili ya mazishi.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana. Kama yeye alitaka kujiua, kwa nini aue na watoto?

RIP Kalebu.
 
huyu jamaa kwa kweli alichanganyikiwa

kwa kweli kwenye jamii yetu tunatakiwa tuwe na watu wa elmu nafsi kila pahala na kuisaidia jamii kiukweli

pole wote waliokutwa na msiba huo
 
siku za mwisho zimekaribia... dah! unyama wa hali ya juu
 
Huyu mtu alionyesha dalili za kuchanganyikiwa wiki nzima kabla alipojaribu kujinyonga kwa mara ya kwanza. Angepata huduma za ushauri nasaha/tiba ya afya ya akili kungali mapema pengine hayo machukizo yasingetokea.

Tunayo njia ndefu kufikia huduma bora za kitabibu.
 
Huyu marehemu ni hakika kuna mambo mazito yalikuwa yanamchanganya akili.
Kweli huu ni unyama mzito.
 
familia ya huyo marehemu pia ni ya kulaumiwa sana, kwa stress alizokuwa nazo huyo bwana hakutakiwa kabisa kuachwa peke yake zaidi alihitaji wataalamu wa saikolojia na viongozi wa dini kuhakikisha wanakaa nae muda wote hadi arudi hali ya kawaida na sio kumuacha mwenyewe hadi akafikia maamuzi mazito kama hayo, mungu amlaze mtoto aliyeuwawa mahali pema peponi.
 
MMh. nimekosa neno nimebaki kusikitika na kuumia. Unyama gani huu. Namhurumia huyo mtoto aliyeshuhudia unyama huo maana itamsumbua sana. Pleni familia ya mtoto aliyeuawa na aliyejeruhiwa.
 
Wanafamilia wa muuaji na polisi hawakuwa makini kwani tangu alipojaribu kujiua alipaswa kuwa amehifadhiwa chini ya mkono wa sheria.

KAREBU RIP
 
Too bad, wanasaikolojia nao bei zao za consultation ni ngapi, I need to see one. Guys help me out
 
Hivi jamani watu mliosoma sociology na psychology hebu jaribuni kuanzia social social counselling centres mtasadia na kuepusha mengi sana. Hii ni maumivu sana kwa watoto wale waliokufa na waliobaki. Hizi ndoa jamani tuziweke mikononi mwa kristo mwenyewe.
 
chanzo cha mke kutaka talaka hakijazungumziwa.na marehemu aliamua kuua watoto wa mdogo wa mkewe(shemejiye). Inawezekana kuna sababu,nilishawahi kuona mtu kazaa na mdogo wa mkewe na wanaishi wote nyumba moja bado!ila kweli huyo aliyeshuhudia anahitaji kufanyiwa counselling makini kabisa.mnaoshughulika na haki za watoto ,plz do something!vichaa vya ulaya vimeanza kuja kwa kasi!
 
too sad jamani!huyo jamaa wangemuwahi kumfanyia counsellings hizo hasira zingekwisha na haya yote yasingetokea!
na huyo mtoto aliyeshuhudia wanatakiwa wafanye kazi ya ziada awe normal coz hiyo kitu itamsumbua sana!RIP Kalebu
 
Ingawa jambo hili limetokea lakini wakati mwingine lingeweza kuzuilika tangu mara ya kwanza alipotaka kujiua na jaribio lake kushindwa kwa kuokolewa na ndugu zake.Huyu hakuwa mtu wa kuachwa peke yake kwani tayari alikuwa na tatizo kubwa lililotaka ufumbuzi wa kina na wa muda mrefu.
Mungu awarehemu.
 
Ameuwa Watoto kwa sababu ya kutaka kumkomowa mke wake anaye taka aachike Mahakamani.
..Kama angekuwa anataka kumkomoa mkewe angewachinja watoto wake (ambao amezaa na mkewe) kwa nini mtoto wake hakumchinja??? Huyo alikuwa na matatizo yake tu!!
 
Back
Top Bottom