Mfahamishe mtanzania mwenzio

Liganga

Senior Member
Jul 4, 2007
165
125
Leo kiunaga ubaga natoa uchambuzi wa Taifa letu miaka ile ya sabini na leo wakati tuna
adhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Utakapo fika mwisho wa habari hii fupi naomba
utoe jibu lako katika kila kipengere cha kauli hii ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, yaani :

"TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE"

Miaka ile ya sabini, taifa letu lilifanana hivi na Leo linafanana hivi
Mashirika ya Umma : 1970s = 300+ na 2011 = < 10
Benki ya biashara : 1970s = 1 na 2011 = 0
Benki ya nyumba : 1970s = 1 na 2011 = 0
Vyama vya ushirika : 1970s = 20+ na 2011 = 0
Dola kwa shilingi : 1970s = 1/8 na 2011 = 1/1800
Asilimia ya mapato ya kuuza nje iliyotumika kuagiza mafuta : 1970s = 10% na 2009 = 52%
Tani moja ya chai ilinunua mafuta ghafi : 1970s = 60 pipa na 2011 = 35 pipa
Gharama za vita : 1970s = $ 500 million na 2011 = 0
Kampuni za simu mezani : 1970s = 1 na 2011 = 1
Kampuni simu za viganja : 1970s = 0 na 2011 = 5
Uzalishaji umeme : 1970s = MW350+ na 2011 = MW780+
Bandari za baharini : 1970s = 3 na 2011 = 3
Meli : 1970s = 8 na 2011 = 3
Mashirika ya Reli : 1970s = 2 na 2011 = 2
Wakala wa meli : 1970s = 1 na 2011 = 0
Ndege za ATC : 1970s = 5 na 2011 = 1
Mtandao wa barabara za lami : 1970s = 3000+ na 2011 = 9000+


Tuendele kuiboresha orodha hii hili kuweza kujua je ni kweli
TUMETHUBUTU????
TUMEWEZA?????
TUNASONGA MBELE????

Nyongeza
Nashukuru kwa maoni ya wachangiaji mbalimbali
Muda unabana lakini nafikiri tukishirikiana tutaboresha hiki kitu
Nimejitahidi kupitia vitabu vichache vyenye kueleza juu ya Tanzania wakati
ule, pia nimetembelea tovuti ya NBS (Taasisi ya takwimu apo nyumbani) nao pia wako na
takwimu za miaka ya hivi karibuni.

Tunaitaji takwimu kugusa maeneo yafuatayo :

1. Elimu >> wahitimu ngazi mbalimbali na idadi ta taasisi za elimu

2. Maji

3. Afya

4. Mauzo ya nje

5. Thamani ya bidhaa tulizoagiza

6. GDP

7. Mshahara kima cha chini

8. Bei za vitu vya msingi (mchele, mafuta kula, maharage, unga, ndizi, ngano, nyanya, vitunguu n.k)

9. Idadi ya watu (Population)

10. Ukubwa wa bunge (idadi ya wabunge, matumizi yake) na serikali (idadi ya mawaziri na manaibu, wakuu wa mikoa, matumizi ya serikali)

Ningependa sisi hapa JF tuifanye kazi yetu hii na ndio iwe mchango wetu katika maadhimisho ya
miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Tunaweza kuitoa humu na pia katika magazeti mbalimbali ya kila siku
na kama wahariri wakikubali badala ya kuwa makala, iandaliwe vizuri kama toleo maalum.



MWISHO :
Kwa wale walio na wasi wasi wa nini nimeifanyia nchi yangu, kazi hii ni moja wapo wa vitu ninavyoifanyia
nchi yangu (Muda na uchambuzi niliowekeza) pamoja na uwakilishi mzuri huku ughaibuni kwa kulinda
sifa na heshima ya mtanzania huku nikienzi lugha yangu ya kiswahili.
 
Mkuu,
Kutokana hiyo statistics, Hakuna tulichoweza wala kuthubutu na kusonga mbele, kwani as we talk now everyrhing in our country is shagrabagla na hata ukimuuliza kiongozi wapi wantupeleka naye atakujibu UNAFIKIRI tunaelekea wapi? na mwishowe atakutukana matusi ya nguoni. Mimi binafsi sioni cha kujivunia hasa ktk kipindi hiki.
 
Liganga,
Heko kwa tathmini nzuri.
Tunaweza kuongeza orodha ya vilivyokuwa vyanzo vya mapato vilivyo iwezesha serikali kutoa huduma za jamii bure kwa wananchi miaka ile tukalinganisha na utitiri vyanzo vya sasa ili kubaini kama uwezo wa sasa wa serikali kutoa huduma kwa jamii nao UMETHUBUTU, UMEWEZA na UNASONGA MBELE!
 
Nyinyi watu wa ccm mnaotupigia makelele hapa JF tunawasubiri sasa na nyinyi mtoe statistic zenu. Mnasema kila siku mmefanya mengi sasa ngoma ipo hapo tunahitaji michango yenu.
 
Ningesisitiza ili swala tulifanye kiufundi na kitaalamu zaidi, takwimu ni nyingi

naomba tushirikiane kuziweka hapa. Tusiweke mabishano ya kichama.

Nitafurahi kama tutaweza kukusanya taarifa nyingi ikiwezekana kabla ya

tarehe 9 Desemba tutoe huko nyumbani japo makala kwenye magazeti yetu

inayoakisi huu mchango wetu hapa.
 
Leo kiunaga ubaga natoa uchambuzi wa Taifa la letu miaka ile ya sabini na leo wakati tuna

adhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Utakapo fika mwisho wa habari hii fupi naomba

utoe jibu lako katika kila kipengere cha kauli hii ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, yaani :

TUMETHUBUTU

TUMEWEZA

NA TUNASONGA MBELE


Miaka ile ya sabini, taifa letu lilifanana hivi Leo linafanana hivi

Mashirika ya Umma : 1970s = 300+ na 2011 = < 10
Benki ya biashara : 1970s = 1 na 2011 = 0
Benki ya nyumba : 1970s = 1 na 2011 = 0
Vyama vya ushirika : 1970s = 20+ na 2011 = 0
Dola kwa shilingi : 1970s = 1/8 na 2011 = 1/1800
Asilimia ya mapato ya kuuza nje iliyotumika kuagiza mafuta : 1970s = 10% na 2009 = 52%
Tani moja ya chai ilinunua mafuta ghafi : 1970s = 60 pipa na 2011 = 35 pipa
Gharama za vita : 1970s = $ 500 million na 2011 = 0
Kampuni za simu mezani : 1970s = 1 na 2011 = 1
Kampuni simu za viganja : 1970s = 0 na 2011 = 5
Uzalishaji umeme : 1970s = MW350+ na 2011 = MW780+
Bandari za baharini : 1970s = 3 na 2011 = 3
Meli : 1970s = 8 na 2011 = 3
Mashirika ya Reli : 1970s = 2 na 2011 = 2
Wakala wa meli : 1970s = 1 na 2011 = 0
Ndege za ATC : 1970s = 5 na 2011 = 1
Mtandao wa barabara za lami : 1970s = 3000+ na 2011 = 9000+


Tuendele kuiboresha orodha hii hili kuweza kujua je ni kweli

TUMETHUBUTU????

TUMEWEZA?????

TUNASONGA MBELE????
hayo tu na bado under Mustapha Mkullo as the overseer of the economy.
 
1970s issei ya watu < 10 mil,2011 <40 mil.sukari Kg sh 1.20 2011 sukari 2500/Kg
 
Mtoa mada,unaweza kuongezea idadi ya shule, waalimu, enrollment, vifo vya watoto na wajawazito.
Ila hapi kwenye mashirika ya reli naona imebaki 1, trl sidhani kama inahesabika.
 
Wamethubutu kulidhoofisha taifa kiuchumi,wameweza kufukarisha watanzania na wanasonga mbele kuikabidhi nchi yetu mikononi mwa mabwana zao(wawekezaji/wachukuaji).
 
1970 mikataba haikuwa siri > 2011 mikataba yote ya serikali ni siri!
 
JAMBO MUHIMU MKUU UMESAHAU elimu ya darasa la 4 mwaka 1970 = darasa la kidato cha 6 mwaka 2010. migodi ya almasi 1 pekee na sasa dhahabu na gesi kibao huku pato likidorora
 
Magamba wamethubutu wameweza na sasa wanasonga mbele kuruhusu ushonga. Kwamba wanasherekea uhuru wa miaka hamsina na ushonga kuwa huru!
 
Waliokuwa na uwezo wa kusoma na kuandika 1970's=90%,2010's=65%

Viwanda vya nguo k.m Mutex,Urafiki,Kilitex,Mwatex 1970's=5, 2010's=0
 
Mtoa mada nakupongeza. We need people like u to advice presient JK.Kikwete. Big up.
 
Back
Top Bottom