Mfahamishe mtanzania mwenzio

Haya mambo ndio ya kuelimisha wenzetu ambao, hawana access ya kuingia humu. Watawala wamekua wadanganyifu kana kwamba kuna maendeleo makubwa kumbe uzushi mtupu. Ningependa iandaliwe makala ndefu inayoeleza kwa kina kuhusu tofauti ya kimaisha toka miaka ya 70s hadi leo. Ili tuone wamedhubutu nini na wameweza nini na kwa lipi wanalosongesha mbele?
 
kama kuna Mtanzania anasema tumerudi nyuma compared na 1961 basi huyo si mzalendo au anasukumwa zaidi na utashi wa kisiasa. Utandawazi (ambao ni mfumo mpya wa ukoloni) ndo ulizozisukuma nchi nyingi maskini zikubali kubinafsisha mashirika yao kwa wenye pesa, na hasa baada ya kushindwa ujamaa. Believe me or not, nchi maskini kokote kule duniani zinaendeshwa kwa matakwa ya mataifa makuu kama Marekani, Uingereza etc.
compare it in this way....
ulikuwa unatumia muda gani kuwasiliana na ndg zako kule shamba wakati wa uhuru na sasa ni vipi(it termz za teknohama)?
ulikuwa unatumia muda gani kwenda kijijini kwenu kule kasulu na kwingineko wakati wa uhuru ukilinganisha na sasa?
kulikuwa na watanzania wangapi wenye elimu ya kuanzia atleast secondary hadi uprofesa 1961 compared na sasa?
fursa za ajira kipindi kile na sasa (of course after uwekezaji hasusani sekta ya mawasiliano) ziko sawa?
hivi makazi na malazi mijini na vijijini yalikuwa bora wakati ule kuliko sasa?
uhuru wa habari ulikuwa bora wakati ule kuliko sasa?hivi wakati ule ungethubutu kumtukana rais gazetini na ukaendelea kucheka mtaani?
idadi ya watanzaia wanaoshika nafasi mbalimbali kwenye organs za kimataifa zimepungua/zimeongezeka?
na mengine mengi.
mafanikio ya nchi hayapimwi kwa serikali kuwa na idadi kubwa ya mashirika ya uma yasiyo na tija yeyote kwa mustabali wa nchi
wala hayapimwi kwa porojo majukwaani bali kwa kufanya kazi kwa bidii. Jiulize wewe kama mtanzania mzalendo umefanya nini cha kujivunia kwa nchi yako. na ni ukweli usiopingika kwa yeyote mwenye utambuzi na upeo wa ziada kuwa serikali za nchi masikini kama yetu (ukubali ukatae) huendeshwa kwa matakwa ya magharibi, na bahati mbaya sana huwa tunawatelekeza wale wanaopambana na ufedhuli wao just kwa kudanganywa kidogo tu kama tulivyofanya kwa akina gadafi,mugabe na wengineo ambao tuliambiwa hadithi za kipuuzi tukaziamini. na ndio maana tumebaki watumwa wa fikra kwa wanasiasa mafukara wa hoja wa nchi masikini ambao wapo kwa ajili ya matumbo yao tu hata kama ni kwa kusacrifice wengine....NI KWELI....TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE...ninachoweza ku add kama mtanzania mzalendo ni kuwa (huu ni ukweli) tulitakiwa tuwe mbali zaidi ya hapa kama uadilifu ungesimama miongoni mwa viongozi wetu. ni wakati wa kutafakari kama Taifa...
 
takwimu ni za kwako binafsi umezitengeza ili kukidhi matakwa ya kisiasa. Wewe wenyewe hujasema umeifanyia nini nchi yako. Ni nini mchango wako kwa chi yako. Hiki ndicho kipimo cha Marekani na kimewafikisha mbali sana.

Wamarekani mmoja mmoja wanajikweza kwa kuzungumza walichofanya kwa nchi yao sio walichoharibu wengine. wanajitapa mmoja mmoja kwa kusahihisha makosa ya watangulizi wao kwamba wewe umeshiriki vipi kusahihisha makosa ya watangulizi kwa mambo yaliyoharibika
 
Nakupongeza,kweli leo umekuja kuwashika ila kama alivyokwisha sema LIGANGA,tusiende kwa mlengo wa vyama twende na facts basi.mtoa mada ongeza hapo MSHAHARA WA MBUNGE WA 1970 NA POSHO ZAKE NA 2011.
 
Haya ndo mambo tunayoyata Hapa Jf.Big up mkuu! Nlikuwa pungwani but kwa statistics hizo Nimeelimika.
 
UTAJIRI WA VIONGOZI WA UMMA

Lohassa - 1970's - Tshs 900,000/= 2011 -Tshs 800,000/= billion
Chenge - 1970's aliishi kwa mshahara, 2011 - USD 2 billion (anaita vijisent)
William Mkapa - 1970's aliishi kwa msharaha - 2011 analingana na Mengi
JK - 1970's aliishi kwa mshahara - 2011 untouchable wealth
Mwakyembe 1970's mwanafunzi wa kawaida - 2011 fisadi mjanja
 
Kwa wenye kumbukumbu nzuri enzi hizo dola 1 ya Kimarekani ilikuwa sawa na sh 5 ya Tanzania,hadi kupelekea sarafu ya sh 5 <gwala>kuitwa dala.Paundi 1 ya Uingereza ilikuwa sawa na sh 20 ya Tanzania hadi ikapelekea ile noti ya sh 20 wakati ule kuitwa paundi.Wenye vichwa vizuri watakuwa wanakumbuka vizuri sana.Sasa pima mwenyewe kama tunasogea mbele ama tunarudi nyuma?
 
kama hali ndio hii tuna miezi kadhaa tu Mkullo atakuwa keshatumaliza kabisaaaa!
 
nimependa sana huo utafiti ila umesahau kuweka nafasi za kazi

kwa kuwa umeliona hilo eneo, na yeye ameomba tumsaidie kuja na data sahihi za tofauti ya '70 na 2011, basi sasa weja facts. Huna soma na kupotea, sio kuja kukosoa kazi nzuri ya mwenzako kwa uvivu wako wa kusoma na uzito wa kuelewa.
 
kama kuna Mtanzania anasema tumerudi nyuma compared na 1961 basi huyo si mzalendo au anasukumwa zaidi na utashi wa kisiasa. Utandawazi (ambao ni mfumo mpya wa ukoloni) ndo ulizozisukuma nchi nyingi maskini zikubali kubinafsisha mashirika yao kwa wenye pesa, na hasa baada ya kushindwa ujamaa. Believe me or not, nchi maskini kokote kule duniani zinaendeshwa kwa matakwa ya mataifa makuu kama Marekani, Uingereza etc.
compare it in this way....
ulikuwa unatumia muda gani kuwasiliana na ndg zako kule shamba wakati wa uhuru na sasa ni vipi(it termz za teknohama)?
ulikuwa unatumia muda gani kwenda kijijini kwenu kule kasulu na kwingineko wakati wa uhuru ukilinganisha na sasa?
kulikuwa na watanzania wangapi wenye elimu ya kuanzia atleast secondary hadi uprofesa 1961 compared na sasa?
fursa za ajira kipindi kile na sasa (of course after uwekezaji hasusani sekta ya mawasiliano) ziko sawa?
hivi makazi na malazi mijini na vijijini yalikuwa bora wakati ule kuliko sasa?
uhuru wa habari ulikuwa bora wakati ule kuliko sasa?hivi wakati ule ungethubutu kumtukana rais gazetini na ukaendelea kucheka mtaani?
idadi ya watanzaia wanaoshika nafasi mbalimbali kwenye organs za kimataifa zimepungua/zimeongezeka?
na mengine mengi.
mafanikio ya nchi hayapimwi kwa serikali kuwa na idadi kubwa ya mashirika ya uma yasiyo na tija yeyote kwa mustabali wa nchi
wala hayapimwi kwa porojo majukwaani bali kwa kufanya kazi kwa bidii. Jiulize wewe kama mtanzania mzalendo umefanya nini cha kujivunia kwa nchi yako. na ni ukweli usiopingika kwa yeyote mwenye utambuzi na upeo wa ziada kuwa serikali za nchi masikini kama yetu (ukubali ukatae) huendeshwa kwa matakwa ya magharibi, na bahati mbaya sana huwa tunawatelekeza wale wanaopambana na ufedhuli wao just kwa kudanganywa kidogo tu kama tulivyofanya kwa akina gadafi,mugabe na wengineo ambao tuliambiwa hadithi za kipuuzi tukaziamini. na ndio maana tumebaki watumwa wa fikra kwa wanasiasa mafukara wa hoja wa nchi masikini ambao wapo kwa ajili ya matumbo yao tu hata kama ni kwa kusacrifice wengine....NI KWELI....TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE...ninachoweza ku add kama mtanzania mzalendo ni kuwa (huu ni ukweli) tulitakiwa tuwe mbali zaidi ya hapa kama uadilifu ungesimama miongoni mwa viongozi wetu. ni wakati wa kutafakari kama Taifa...

Mwanzo gamba @ work
Mwisho umekubali mwenyewe
 
Liganga uko sahihi sana!! Kijijini kwangu miaka hiyo ya sabini kulikuwa na mtandao mkubwa wa maji safi ya bomba ( jirani na nyumba yetu kulikuwa na mabomba 2 yaliyokuwa yanatoa maji muda wote) leo hakuna bomba hata moja na idara ya maji wameng'oa kila kitu; Miaka ya sabini pia nilikuwa naishi Mburahati NHC nyumba zote zilikuwa na maji na ushahilini kote waliweka vituo vya maji ya bomba unlipa sh 5 kwa ndoo; sasa hivi Mburahati maji ni ndoto!! kwa kweli mi naona badala ya kwenda mbele tumerudi nyuma kabisaaa!!! Hivyo tungeadhimisha miaka 50 ya kurudi nyuma!!
Leo kiunaga ubaga natoa uchambuzi wa Taifa la letu miaka ile ya sabini na leo wakati tuna

adhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Utakapo fika mwisho wa habari hii fupi naomba

utoe jibu lako katika kila kipengere cha kauli hii ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, yaani :

TUMETHUBUTU

TUMEWEZA

NA TUNASONGA MBELE

Miaka ile ya sabini, taifa letu lilifanana hivi Leo linafanana hivi

Mashirika ya Umma : 1970s = 300+ na 2011 = < 10
Benki ya biashara : 1970s = 1 na 2011 = 0
Benki ya nyumba : 1970s = 1 na 2011 = 0
Vyama vya ushirika : 1970s = 20+ na 2011 = 0
Dola kwa shilingi : 1970s = 1/8 na 2011 = 1/1800
Asilimia ya mapato ya kuuza nje iliyotumika kuagiza mafuta : 1970s = 10% na 2009 = 52%
Tani moja ya chai ilinunua mafuta ghafi : 1970s = 60 pipa na 2011 = 35 pipa
Gharama za vita : 1970s = $ 500 million na 2011 = 0
Kampuni za simu mezani : 1970s = 1 na 2011 = 1
Kampuni simu za viganja : 1970s = 0 na 2011 = 5
Uzalishaji umeme : 1970s = MW350+ na 2011 = MW780+
Bandari za baharini : 1970s = 3 na 2011 = 3
Meli : 1970s = 8 na 2011 = 3
Mashirika ya Reli : 1970s = 2 na 2011 = 2
Wakala wa meli : 1970s = 1 na 2011 = 0
Ndege za ATC : 1970s = 5 na 2011 = 1
Mtandao wa barabara za lami : 1970s = 3000+ na 2011 = 9000+

Tuendele kuiboresha orodha hii hili kuweza kujua je ni kweli

TUMETHUBUTU????

TUMEWEZA?????

TUNASONGA MBELE????
 
Back
Top Bottom