Meya afika kwenye madanguro Mwananyamala, Wadada wanaojiuza wakimbia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Kufuatia ongezeko la madanguro katika maeneo ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amefika kwenye maeneo ya kunapodaiwa kufanyika kwa biashara ya kuuza mwili maeneo ya Mwananyamala na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa nyumba zinazotumiwa katika biashara hiyo.

Amesema: “Ukiacha danguro hili la Mwananyamala Mianzini kuna sehemu nyingine kama Tandale Uwanja wa Fisi na kuna Msasani Mikorosini na taarifa zinasema yapo mengi.

“Watendaji wetu wamepewa kazi ya kuhakikisha wanapata idadi kamili ya madanguro katika Kata zetu 20 na Mitaa 126.”

Ameongeza kuwa watawaita wenye nyumba wote kujieleza kwa nini wamegeuza nyumba zao kuwa madanguro, na kuwa biashara ya kujiuza inaanzia 2,000 hadi 10,000.

“Mipango mingi hairuhusu kinachofanyika, jambo hili siwezi kulifanya peke yangu, lazima Serikali Kuu iingilie, sheria lazima ifuatwe, hatuwezi kuacha jamii iendelee kuangamia.

“Tunasema tupambane na maradhi hasa magonjwa ya ngono kwa hali hii,” amesema Meya na kuongeza:

“Zipo taarifa zisizo rasmi hawa watu (dada poa) wanajipanga na kutoa fedha kwenye baadhi ya mamlaka zinazotakiwa kuzuia hii biashara, hatuwezo kuona Watoto wetu wanakua huku wanaangalia hiki kinaendelea, wataacha kusoma na kuamini hii ndio biashara stahiki.”

Amesisitiza kuwa wenye nyumba wanatakiwa kujitokeza na ambao hawatajitokeza nyumba itataifishwa na Serikali.

Naye Diwani wa Kata ya Makumbusho, Mohamed Mohamed amesema wameita wenye nyumba kuwauliza sababu za nyumba zao kuhusika katika biashara hiyo, lakini wakadai kuwa wale ni wateja wao wa kawaida na kuhusu wanachokifanya ndani hawawezi kuwaingilia.

Dada mmoja ambaye alijifungia ndani na kusikika sauti tu alisema “Watoto wenu wanakula, wa kwangu je, mnataka wale wapi?”

Nao baadhi ya Wateja waliohojiwa walisema kuna changamoto kadhaa wanazokutana nazo ni kufanyiwa fujo, kuibiwa vitu vyao na kushambuliwa hasa kama ukiwa si mwenyeji wa eneo husika.

Chanzo: ITV & Global TV
 
Dah kuna chimbo moja lilikuwa linaitwa Tururamba kule SIM2000 karibu na Law School nilipelekwagwa na mwana fulani kunywa beer ni nyumba ya mtu watu wamekaa sebuleni kidirishani ndio vinywaji vinauzwa nikajua ni wanafamilia ila nashangaa mijamaa inazama sebuleni inachukua mwanamke wanaenda vyumbani.

Kumbe ndio danguro.
 
Kufuatia ongezeko la madanguro katika maeneo ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amefika kwenye maeneo ya kunapodaiwa kufanyika kwa biashara ya kuuza mwili maeneo ya Mwananyamala na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa nyumba zinazotumiwa katika biashara hiyo.

Amesema: “Ukiacha danguro hili la Mwananyamala Mianzini kuna sehemu nyingine kama Tandale Uwanja wa Fisi na kuna Msasani Mikorosini na taarifa zinasema yapo mengi.

“Watendaji wetu wamepewa kazi ya kuhakikisha wanapata idadi kamili ya madanguro katika Kata zetu 20 na Mitaa 126.”

Ameongeza kuwa watawaita wenye nyumba wote kujieleza kwa nini wamegeuza nyumba zao kuwa madanguro, na kuwa biashara ya kujiuza inaanzia 2,000 hadi 10,000.

“Mipango mingi hairuhusu kinachofanyika, jambo hili siwezi kulifanya peke yangu, lazima Serikali Kuu iingilie, sheria lazima ifuatwe, hatuwezi kuacha jamii iendelee kuangamia.

“Tunasema tupambane na maradhi hasa magonjwa ya ngono kwa hali hii,” amesema Meya na kuongeza:

“Zipo taarifa zisizo rasmi hawa watu (dada poa) wanajipanga na kutoa fedha kwenye baadhi ya mamlaka zinazotakiwa kuzuia hii biashara, hatuwezo kuona Watoto wetu wanakua huku wanaangalia hiki kinaendelea, wataacha kusoma na kuamini hii ndio biashara stahiki.”

Amesisitiza kuwa wenye nyumba wanatakiwa kujitokeza na ambao hawatajitokeza nyumba itataifishwa na Serikali.

Naye Diwani wa Kata ya Makumbusho, Mohamed Mohamed amesema wameita wenye nyumba kuwauliza sababu za nyumba zao kuhusika katika biashara hiyo, lakini wakadai kuwa wale ni wateja wao wa kawaida na kuhusu wanachokifanya ndani hawawezi kuwaingilia.

Dada mmoja ambaye alijifungia ndani na kusikika sauti tu alisema “Watoto wenu wanakula, wa kwangu je, mnataka wale wapi?”

Nao baadhi ya Wateja waliohojiwa walisema kuna changamoto kadhaa wanazokutana nazo ni kufanyiwa fujo, kuibiwa vitu vyao na kushambuliwa hasa kama ukiwa si mwenyeji wa eneo husika.

Chanzo: ITV & Global TV
Huyo naye aache kuingilia biashara na starehe za watu. Hiyo biashara ipo tangu kuumbwa kwa dunia.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
JamiiForums-623456179.jpg
 
Toka nasoma shule ya msingi nawaona wadada wanajiuza ni kitambo Sana kumbe Toka mwaka 1978 watu wanajiuza?
Wilaya ya kinondoni imelaaniwa miaka mingi Sana
Hakuna cha laana wala nini hiyo ni biashara kama biashara nyingine tu, wafanye mpango irasimishwe kwani bila hao dada poa kesi za ubakaji na ulawiti zingekuwa nyingi sana kuliko ilivyo sasa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sio napajua tu, nimeingia vyumbani mara kadhaa. Unabwabwaja wewe na huyo mshamba anayeitwa Meya. Tafuteni kazi za kufanya.
Vile unaviita vyumba Wakati ukiwa njiani k unaziona zinaning'inia kama mishikaki?!

Hakika wewe umetoka migombani juzi Kati!
 
Dah kuna chimbo moja lilikuwa linaitwa Tururamba kule SIM2000 karibu na Law School nilipelekwagwa na mwana flani kunywa beer ni nyumba ya mtu watu wamekaa sebuleni kidirishani ndio vinywaji vinauzwa nikajua ni wanafamilia ila nashangaa mijamaa inazama sebuleni inachukua mwanamke wanaenda vyumbani.

Kumbe ndio danguro.

Wewe ulinunua kwa shingapi mkuu?
 
Back
Top Bottom