Dar: RC Chalamila atoa siku 5 kuvunja madanguro. Hongera sana kwa kusambaratisha biashara ya ngono

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,148
7,724
Chanzo channel ten habari 3/11/2023 saa moja usiku.

Wakazi wa Jiji la DSM tunampa hongera RC Chalamila kwa kupambana na biashara haramu ya kuuza miili/ngono, biashara hii imekuwa chanzo kikuu cha maambukizi ya ukimwi lakini pia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii.

Naomba viongozi wwngine kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wakuu wa wilaya kwenye kila eneo wapambane na utovu huu wa maadili.

Sisi wananchi tutaendelea kufichua vyanzo vyote vya biashara ya ngono.

---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa siku tano kwa wamiliki wa madanguro akiwataka kuyavunja wenyewe, na kwamba wasipofanya hivyo, atataifisha nyumba hizo.

Pia amewaagiza wamiliki wa baa zote ambazo nje kunafanyika biashara hiyo kuhakikisha wanawaondoa vinginevyo atazifunga.

Chalamila ametoa maagizo hayo leo ijumaa Novemba 3,2023 wakati alipotembelea madanguro yaliyovunjwa na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.

Novemba Mosi mwaka huu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Saad Mtambule, walivunja madanguro hayo na kuwakamata baadhi ya wasichama waliodaiwa kuhusika kufanya biashara hiyo.

Chalamila amesema,nyumba zilizopewa leseni kwa ajili ya makazi na kubadilishwa matumizi ni kosa kisheria na kuwataka kuzivunja ndani ya siku tano."Natoa siku tano nyumba zote zilizojengwa na kugeuzwa madanguro muwe mmezivunja vinginevyo ntazitaifisha,"

"Na wale wamiliki wa baa ambazo nje biashara hii inafanyika, wakina dada wanajipanga,ikome maramoja vinginevyo nitazifinga zote,hatuwezi kulea ujinga wa namna hii," amnesema Chalamila.

Hata hivyo RC huyo amewataka Wakuu wa Wilaya katika mkoa huo kuhakikisha operesheni hiyo inaendelea kwenye maeneo yote ya kiutawala na kwamba wahakikishe biashara hiyo inakomneshwa.

Kuhusu biashara ya kusingwa mwili (massage) amesema baadhi ya saluni zinatoa huduma hiyo.

Alisema siku chache zilizopita kuna mtu alifariki kwenye chumba akipatiwa huduma hiyo,na kwambani ngumu kujua ni nini kilichompata na kuwataka viongozi hao kuzichunguza.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule alisemna eneo hilo lina nyumba nane zenye leseni za makazi lakini zimegeuzwa kuwa madanguro.

Alisema Juni mwaka huu walifanya kikao na wamiliki wa nyumba hizo pamoja na viongozi wa dini, na kukubaliana kuzibomoa lakini wakaomba kupewa miezi sita ili waweze kuondoka, japo walikuta biashara hiyo ikiendelea.

Amesema baada ya kukuta biashara hiyo inaendelea, waliamua kuchukua hatua ikiwemo kung'oa milango na kuwataka wamiliki wa nyumba hizo kuzivunja wenyewe kabla hawajachukua hatua zaidi.

"Tutaendelea kuchukua hatua kama ulivyotuelekeza, wakina dada hao wanazo kazi nyingi ambazo wangeweza kuzifanya ikiwemo kukopa mikopo ya asilimia kumi na kufanya biashara," alisema.

"Tumeendelea kushirikiana na baadhi ya kina dada ikiwemo watatu waliokuwa wakifanya biashara eneo hili wapo tuliowashauri, wakachukua ushauri wetu lakini wengi wamelikaidi," amesema Mtambule.

Amebainisha kuwa wote wenye madanguro wanafahamika kwa muda mrefu na kwamba hatua hiyo ya utekelezaji ilikuwa ni suala la muda tu, hivyo watahamia na maeneo mengine.

Kwa upande wake Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge amesema wamedhamiria kukomesha biashara hiyo ilivyokuwa inadhariirisha utu wa mwanamke kwa muda mrefu. Amesema watu waliokuwa hapo wameamua kukaa kimya na kusababisha watoto wadogo kufanya vitendo visivyo na maadili wakiwemo wanafunzi.

"Cha kusikitisha biashara hiyo inaanzia Sh 1,000 hadi 3,000, pale Halmashauri kuna mikopo ya asilimia kumi timewaambia waje wakope waachane na hii biashara wengi wao hawataki," amesema.
 
Shughuli ambazo serikali inaweza kuzifanya kwa umakini ni hizi ! Kamateni wanaokula mabilioni ya fedha ili hospital zetu ziwe vifaa vya kutosha !! tuboreshe mfumo wa elimu madogo wanakaa chini !! pelekeni huduma za umeme na maji vijijini !
siku hizi mambo ni mtandao mmewatoa vyumbani mmewaacha Telegram 🤣🤣

Yaani kukamata hao habari inawekewa bango kubwa kichizi
 
Kuwavunjia madanguro bila kuwapa kazi mbadala ni sawa na bure,, watahamishia show zao kwenye mapagale, maghetto, garage bubu, night club, guest bubu, salon, bar za vichochoroni hata makaburini pia, muhimu ni kuwapa elimu za ujasiliamali na mitaji ili kuwatoa huko, vinginevyo itakua ni kuongeza tatizo badala ya kulimaliza,,
 
Unaijua hii biashara vizuri? Haiwezekani kuizuia ila inawezekana kupunguza tu

Biashara hii inafanyika sana mtandaoni kuliko kwenye madanguro

Telegram ndio mtandao unaoongoza, watu wanatangaza biashara na location kisha mtu anakubaliana naye anamfuata lodge

Hapo inakuwa kama mtu na demu wake kumbe ni muuzaji na mnunuaji
 
Chanzo channel ten habari 3/11/2023 saa moja usiku.

Wakazi wa Jiji la DSM tunampa hongera RC Chalamila kwa kupambana na biashara haramu ya kuuza miili/ngono, biashara hii imekuwa chanzo kikuu cha maambukizi ya ukimwi lakini pia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii.

Naomba viongozi wwngine kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wakuu wa wilaya kwenye kila eneo wapambane na utovu huu wa maadili.

Sisi wananchi tutaendelea kufichua vyanzo vyote vya biashara ya ngono.
Hana ubavu wa kusambaratisha biashara hii sababu polisi ndio wateja wakuaminika katika biashara hii.

Anachoweza kubadili ni mfumo wa biashara yenyewe kutoka hapo ilipo kwenda kuwa take away au kuimarika kwa biashara ya online.

Huwezi kuuwa biashara ambayo soko lake ni kubwa sana. Ukitaka kuuwa biashara uwa soko lake.
 
Chanzo channel ten habari 3/11/2023 saa moja usiku.

Wakazi wa Jiji la DSM tunampa hongera RC Chalamila kwa kupambana na biashara haramu ya kuuza miili/ngono, biashara hii imekuwa chanzo kikuu cha maambukizi ya ukimwi lakini pia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii.

Naomba viongozi wwngine kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wakuu wa wilaya kwenye kila eneo wapambane na utovu huu wa maadili.

Sisi wananchi tutaendelea kufichua vyanzo vyote vya biashara ya ngono.
Wivu tu.
 
HABARI Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, ametoa siku kwa wamiliki wa madanguro zaidi ya 150 yaliyopo Mwananyamala waweze kubomoa kwa hiari kabla serikali haijawachukulia hatua kali za kisheria.

Chalamila ametoa agizo hilo leo, Novemba3, alipofika eneo hilo na kuwataka wabomoe ndani ya siku saba.

Aidha ametoa onyo kwa maeneo mengine yanayojishughulisha na shughuli za uuzaji wa miili watafute biashara ya kufanya na sio kuuza miili yao.

#EastAfricaTv

Habari zaidi
Chalanmila awapa siku tano wenyemadanguro Dar.
Muktasari:
Chalamila ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Novemba 3,2023 wakati alipotembelea madanguro yaliyovunjwa na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa siku tano kwa wamiliki wa
madanguro akiwataka kuyavunja wenyewe, na kwamba wasipofanya hivyo,atataifisha nyumba hizo.Pia amewaagiza wamiliki wa baa zote ambazo nje kunafanyika biashara hiyo kuhakikisha wanawaondoa vinginevyo
atazifunga.Chalamila ametoa maagizo hayo leo ijumaa Novemba 3,2023 wakati alipotembelea madanguro yaliyovunjwa na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.Novemba Mosi mwaka huu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Saad Mtambule,walivunja madanguro hayo na kuwakamata baadhi ya wasichama waliodaiwa kuhusika kufanya
biashara hiyo.Chalamila amesema,nyumba
zilizopewa leseni kwa ajili ya makazi na kubadilishwa matumizi ni kosa kisheria na kuwataka kuzivunja ndani ya siku tano."Natoa siku tano nyumba zote zilizojengwa na kugeuzwa madanguro muwe mmezivunja
vinginevyo ntazitaifisha,"
"Na wale wamiliki wa baa ambazo nje biashara hii inafanyika, wakina dada wanajipanga,ikome maramoja vinginevyo nitazifinga zote,hatuwezi kulea ujinga wa namna hii," amnesema Chalamila.
Hata hivyo RC huyo amewataka Wakuu wa Wilaya katika mkoa huo kuhakikisha operesheni hiyo inaendelea kwenye maeneo yote ya kiutawala na kwamba wahakikishe biashara hiyo inakomneshwa.
Kuhusu biashara ya kusingwa mwili (massage) amesema baadhi ya saluni zinatoa huduma hiyo.
Alisema siku chache zilizopita kuna mtu alifariki kwenye chumba akipatiwa huduma hiyo,na kwambani ngumu kujua ni nini kilichompata na kuwataka viongozi hao
kuzichunguza.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule alisemna eneo hilo lina nyumba nane zenye leseni za makazi lakini zimegeuzwa kuwa madanguro.Alisema Juni mwaka huu walifanya kikao na wamiliki wa nyumba hizo pamoja na viongozi wa dini,nakukubaliana kuzibomoa lakini wakaonmba kupewa miezi sita ili waweze kuondoka,japo walikuta biashara hiyo ikiendelea.Amesema baada ya kukuta biashara hiyo inaendelea,waliamua kuchukua hatua ikiwemo kung'oa milango nakuwataka wamiliki wa nyumba hizo kuzivunja wenyewe kabla hawajachukua hatua zaidi.
"Tutaendelea kuchukua hatua kama ulivyotuelekeza,wakina dada hao wanazo kazi nyingi ambazo wangeweza kuzifanya ikiwemo
kukopa mikopo ya asilimia kumi na kufanya biashara," alisema.
"Tumeendelea kushirikiana na baadhi ya kina dada ikiwemo watatu waliokuwa wakifanya biashara eneo hili wapo tuliowashauri,wakachukua ushauri wetu lakini
wengi wamelikaidi," amesema Mtambule.
Amebainisha kuwa wote wenye madanguro wanafahamika kwa muda mrefu na kwamba hatua hiyo ya utekelezaji ilikuwa ni suala la
muda tu,hivyo wataaamia na
maeneo mengine.
Kwa upande wake Meya wa Kinondoni Songoro Mnyonge amesema wamedhamiria
kukomesha biashara hiyo ilivyokuwa inadhalikisha utu wa mwanamke kwa muda mrefu.Amesema watu waliokuwa hapo wameamua kukaa kimya na kusababisha watoto wadogo kufanya vitendo visivyo na maadili wakiwemo wanafunzi.
"Chakusikitisha biashara hiyo inaanzia Shi, 000 hadi 3,000, pale Halmashauri kuna mikopo ya
asilimia kumi timewaambia waje wakope waachane na hii biashara wengi wao hawataki," amesema.
View attachment 2803210
 
Back
Top Bottom