Meremeta Report: Released to the Public (Revised & Free!)

Yaani ungehisabu pesa zinazoliwa kifisadi tz ...tungekuwa tushakuwa dubai ya pili sasa, nchi ina pesa kufuru ya Mungu, lakini viongizi hakuna hata mmoja mwenye kupenda nchi yake.

Sow can somebody take billions from people who get less than a dollar per day?
 
Nakumbuka jibu la Kikwete alipoulizwa swali, kwanini Tanzania inaendelea kuwa masikini licha ya kuzalisha dhahabu (third producer in Africa), kuwa na wawekezaji katika sekta mbalimbali, nk akajibu SIJUI.

Mimi pia nilisikia habari hizi.
Leo asubihi nilikuwa naitafuta hiyo statement kwenye net ila sijafanikiwa, ningependa sana kuona hiyo quote ya Mr. President.

Mimi naogopa CCM itakaposambaratika, mafisadi watakuwa pande zote mbili na itabidi tuchague kundi moja au jingine la mafisadi, tutakuwa kama Kenya tu!

Wala usiwe na shaka; hata kwa dakika moja usidhani kwamba bila CCM mambo yatakwenda kombo.
Kwa mawazo yangu, ni ishara mbaya chama cha siasa kugawanyika kwa sababu za ovyo-ovyo kama ubinafsi, ukabila nk. Ila kwa mambo ya msingi kama hili sakata la ufisadi, mbona hilo litakuwa jambo bora kabisa!
 
Meremeta Gold: Security, intelligence units all on red alert

-Revealed: Quiet investigations in progress

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

The mysterious dealings of the now-defunct Meremeta Gold Mine Company Limited have become the subject of collective curiosity from a number of top national security and intelligence departments long after its reported liquidation in 2005, it has now come to light.

Impeccable sources have informed THISDAY that investigators from the Tanzania Intelligence and Security Services (TISS), the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), and the Tanzania Police Forces own criminal investigations department (CID) have each been snooping around Meremeta company records filed at the Business Registration and Licensing Authority (BRELA) offices in Dar es Salaam for the past two years or so.

The sources said the investigators appeared mainly interested in gaining access to the companys financial statements and its list of shareholders.

It is understood that although the parallel investigations by all three state agencies are believed to have gathered a significant amount of evidence on the UK-registered company, there has been no status report so far.

It also remains unclear if TISS, PCCB and the police CID were and still are even working together at all, including coordination in gathering, compiling and analysing the evidence on Meremeta.

THISDAY has now learnt that after being formed in the UK, a local branch of the Meremeta company was registered in Tanzania in 1997 and given certificate of compliance number 32755.

At the time, according to THISDAY latest findings, the listed company directors were Russel John Schwartz (a South African national), Wilfred Nyachia (then a senior Treasury official), Zulu Lyana (a Tanzanian civil servant) and Gerald Augustine Mrudi (also a Tanzanian national).

According to the government, Meremeta Gold was originally registered as a joint venture company owned on a 50-50 basis by the Tanzanian government and a private South African company, Trinnex (Pty) Limited.

At least one senior police detective, identified as Senior Superintendent of Police (SSP) Ernest Sakawa, is reported to have visited the BRELA offices and asked to see the Meremeta company files as far back as May 2006.

And again in 2007, the PCCB is understood to have sent one of its own top sleuths, Dunia Kaongo, to gather information about Meremeta from BRELA.

Kaongo is now the PCCB director of investigations, a post he took over from Dr Edward Hoseah after the latters promotion to director general of the governments anti-graft watchdog.

Insiders have also told THISDAY that the police CIDs own quiet probe took it all the way to the Buhemba gold mine in Mara region, which was run by the Meremeta company but has since also been closed down somewhat unceremoniously.

THISDAY investigations have already established that as part of the Meremeta bankruptcy process, former Bank of Tanzania governor Daudi Ballali authorised a questionable payment of over $118m (approx. 150bn/-) to South Africas Nedbank to liquidate a loan issued to the outgoing company.

Following the liquidation of Meremeta, a new company was formed under the name of TANGOLD Limited, which then received an additional $13.34m (approx. 17bn/-) paid by BoT into its bank account at the National Bank of Commerce Limited Corporate Branch in Dar es Salaam.

Former energy and minerals minister Nazir Karamagi is on record as announcing in parliament that TANGOLD was a wholly-owned Tanzania government company, and that all assets and liabilities of the Meremeta company - including the Buhemba gold mine in Mara region � had been transferred to TANGOLD.

However, THISDAY investigations have also verified that TANGOLD Limited was in fact registered as an offshore company in Port Louis, Mauritius in April 2005 - albeit with at least five top government officials listed as directors.

They included Ballali and the permanent secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja, who has continued in the same position todate despite a whole government changeover in the interim.

Others were the then Attorney-General and later senior Cabinet minister, Andrew Chenge; the then permanent secretary in the Ministry of Energy and Minerals, Patrick Rutabanzibwa; and the then permanent secretary in the Ministry of Livestock Development, Vincent Mrisho.

Rutabanzibwa and Mrisho are now permanent secretaries in the Ministry of Water and the Prime Ministers Office, respectively. As for Chenge, he was recently forced to resign from his latest government position (as senior Cabinet minister) after being linked to the 70bn/- military radar scandal dating back from his days as AG.

It has also been verified that although TANGOLD is supposedly a government-owned company, the listed directors (shareholders) are permitted to transfer all or part of their shares to their next of kin.

Furthermore, the Ministry of Finance currently does not list TANGOLD among companies owned by the Tanzanian government.
 
Meremeta Gold: Security, intelligence units all on red alert

It has also been verified that although TANGOLD is supposedly a government-owned company, the listed directors (shareholders) are permitted to transfer all or part of their shares to their next of kin.

Furthermore, the Ministry of Finance currently does not list TANGOLD among companies owned by the Tanzanian government.

Mali za Taifa zinapogeuka kuwa mali binafsi, zinapoweza kurithishwa kwa watoto na vizazi vijavyo vya vigogo wachache huku taifa likibakia hohe hae.
 
Na hii ya KULIKONI ya LEO, nayo inazungumzia hayo hayo, kazi kwenu. Nani wa 'kumfunga paka kengele?'

Serikali yaogopa ufisadi Meremeta

•Uchunguzi wabaini ‘madudu’ ya ajabu

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Polisi kwa muda mrefu sasa wamekusanya ushahidi wa kutosha kuhusiana na watu wanaokabiliwa na kashfa ya rushwa ya Meremeta.

Haya yamejulikana sasa pamoja na serikali kusita kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na matumizi tata ya zaidi ya bilioni 155/- kupitia kampuni hiyo tata ya uchimbaji dhahabu ya Meremeta Limited.

Uchunguzi wa muda mrefu wa KULIKONI umebaini kwamba, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2006, vyombo vya dola ikiwamo Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na Takukuru, vimekuwa vikiichunguza Meremeta na wahusika wote walioguswa na kampuni hiyo.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID), yalianza upelelezi ulioongozwa na SSP Ernest Sakawa Mei, 2006.

Vyanzo vyetu vimeeleza kuwa katika upelelezi huo ushahidi wa kutosha kuhusu kampuni tata ya Meremeta ulikusanywa.

Habari zinaeleza kwamba baadaye mwaka 2007, Takukuru nao waliendelea na upelelezi wao ulioongozwa na Ofisa Mwandamizi wa taasisi hiyo, Dunia Kaongo, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Uchunguzi, akichukua nafasi ya Edward Hoseah, aliyepanda na kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba uchunguzi wa polisi ulikwenda mbali hadi mkoani Mara, ambako walishirikisha maofisa wa polisi mkoani humo uliko mgodi wa Buhemba, uliokuwa ukiendeshwa na Meremeta kabla ya kufilisiwa kiaina na kazi zake kuendeshwa na kampuni nyingine tata ya Tangold Limited.

Hata hivyo, haijafahamika mara moja hatua zilizofikiwa na wachunguzi hao wa vyombo vya dola, pamoja na kutolewa kwa kauli tata kuhusiana na makampuni hayo na mgodi wa Buhemba, ambao kwa sasa umefungwa.

Kampuni ya Meremeta inatajwa kuwa kampuni iliyokomba zaidi ya bilioni 155/- kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kiwango kinachozidi bilioni 133/- zilizochotwa kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Serikali imeunda timu kuchunguza upotevu wa fedha za EPA, chini ya uongozi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Hoseah, lakini haijasema lolote kuhusu Meremeta.

Tayari Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali Ludovick Utouh, ametamka kwamba ofisi yake haiitambui Meremeta kama kampuni ya umma kwa kuwa haijawahi kukaguliwa, huku baadhi ya viongozi wa serikali wakiwamo mawaziri wakidai kwamba ni ya umma.

Habari zinaeleza kwamba Meremeta iliweza kuchota kiasi kikubwa cha fedha kutokana na shinikizo na baraka zote za Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye anatajwa moja kwa moja kuihalalisha kampuni hiyo alipokuwa madarakani.

Utuoh katika maelezo yake yaliyonukuliwa katika vyombo vya habari, alisema ofisi yake haijawahi kukagua hesabu za Meremeta Limited huku kampuni hiyo tata ikiwa haimo katika orodha ya makampuni yanayomilikiwa na serikali ama serikali kuwa na hisa.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Matern Lumbanga amewahi kuandika barua kwenda benki moja ya Uingereza, ikieleza kwamba Mkapa kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri mwaka 2000, alitoa idhini ya kuanzishwa kwa shughuli za uchimbani dhahabu katika eneo la Tembo na Buhemba, mkoani Mara.

Katika barua hiyo ya Lumbanga, Ikulu ndiyo iliyobeba jukumu la kuithibitisha na kuitambulisha kampuni ya Meremeta kwa Deutch Bank AG London, iliyoko nchini uingereza kwa nia ya kupata mkopo wa uendeshaji wa mgodi wa dhahabu wa Buhemba ambao kwa sasa umefungwa.

“Tunathibitisha kwamba tunafahamu kuwapo kwa hazina kubwa ya dhahabu nchini Tanzania ambayo haijalinufaisha taifa na serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ilianzisha mradi wa Meremeta ikiwa na malengo ya kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo.

“Baadaye mwaka 2000, Rais (Mkapa) kupitia Baraza la Mawaziri aliazimia uchimbaji mkubwa wa chini ya ardhi katika eneo la Tembo na uchimbaji mwingine wa kawaida katika eneo la Buhemba, kaskazini mwa Tanzania,” inaeleza barua hiyo iliyosisitiza kwamba mradi huo utakua na manufaa kwa taifa.

Barua hiyo inataja kampuni ya Nedcor Trade Services Limited ya Afrika Kusini kuwa ndiyo iliyotoa mkopo wa fedha za kuanzishia mradi huo chini ya usimamizi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, iliyokua inatajwa sana kuwa mmiliki wa mgodi huo hapo awali kabla ya kubainika kuwapo kwa utata mkubwa.

Pamoja na Utouh kuikana Meremeta, kuna taarifa kwamba serikali ya Mkapa kupitia Msajili wa Hazina ilitoa cheti ya kuithibitisha Meremeta kuwa kampuni ya umma tokea Oktoba mosi, 1997 baada ya kudaiwa kwamba serikali ilikua na hisa katika kampuni hiyo.

Hisa zilizodaiwa kuwa za serikali zilikabidhiwa kwa waliokua watendaji wakuu serikalini, ambao hata hivyo hadi sasa wanaendelea kuzishikilia baada ya baadhi yao kuondolewa ama kubadilishwa nafasi zao.

Habari zaidi zinaeleza kwamba watendaji wakuu ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Wizara ya Ulinzi na JKT, walipata hisia za kuwapo kwa mikono michafu katika mradi wa Meremeta na hivyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa wenzao wanaochunguza sakata hilo.

Sakata la Meremeta limeelezwa kuweza kuwa kubwa na zito zaidi kutokana na maelezo ya uwezekano wa kuwapo wahusika wanaofahamika duniani katika biashara chafu na hivyo kuibua mjadala mwingine mkubwa utakaovuka hadi mipaka ya Tanzania.

Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi unaweza kwenda mbali kutokana na kampuni ya Nedcor Trade Services Limited ya Afrika Kusini, kuonekana kuwa na uhusiano na benki ya Nedbank ya Afrika Kusini ambayo sehemu ya fedha hizo zilielekezwa huko, zikitokea BoT, huku baadhi ya wakurugenzi wa kampuni nyingine tata ya Deep Green Finance Limited wakiwa watumishi wa benki hiyo maarufu ya Afrika Kusini.

Deep Green Finance Limited ni kampuni iliyosajiliwa nchini na baadaye kupokea fedha kutoka BoT, kabla ya kufilisiwa bila ya kuwapo maelezo ya kutosha ya madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo katika kipindi ambacho nchi ilikuwa inaelekea katika uchaguzi mwaka 2005.

Kashfa hiyo ya Meremeta inaelezwa kuwa zaidi ya ile ya EPA kutokana na kuwa uwezekano wa kurejesha fedha hizo ni mdogo kutokana na kuingia katika mkondo unaoihusisha zaidi Serikali yenyewe na watendaji wake wakiwahusisha wafanyabiashara wa kimataifa.

Baadhi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Meremeta ambao wanaelezwa kuwa katika nafasi hizo kutokana na nyadhifa zao bado wanaendelea kushikilia hisa hizo akiwamo Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali, ambaye ajira yake ilisitishwa na Rais Jakaya Kikwete na Andrew Chenge, aliyejiuzulu uwaziri hivi karibuni.

Fedha hizo ambazo zilibadilishwa na kuwa Dola za Marekani 131,736,628.73 kwa maelekezo yaliyotolewa Desemba 20, 2005, siku moja kabla ya kuapishwa kwa Rais Jakaya Kikwete, zilifanyiwa uhamisho kwenda Afrika Kusini na kuingizwa Nedbank, na nyingine kuingizwa katika akaunti za kampuni ya Tangold na Meremeta.

Taarifa za wakaguzi zinaonyesha kwamba baada ya ununuzi huo wa dhamana, Benki Kuu ilizibadilisha sehemu ya dhamana hizo kuwa dola za Marekani 118,396,460.36 ambazo zilipelekwa kwenye akaunti moja isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini, benki hiyo ikiwa imezipokea fedha hizo kupitia HSB Bank ya New York, Marekani zikitajwa kuwa malipo ya madeni ya kampuni mufilisi ya Meremeta Ltd.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba sehemu nyingine ya fedha hizo zipatazo Dola za Marekani 13,736,628.73 zililipwa kwa kampuni ya Tangold kwenye akaunti ya kampuni hiyo iliyoko Benki ya NBC Corporate Branch, Dar es Salaam.

Mwaka jana Mbunge wa Karatu Dk. Willibrod Slaa (Chadema), aliliingiza suala hilo katika hoja yake iliyokuja kugonga mwamba.

Katika hoja yake hiyo, Dk. Slaa alibainisha kwamba Meremeta Ltd. ni kampuni binafsi ya kigeni iliyoandikishwa Agosti 19, 1997 katika kisiwa cha Isle of Man nchini Uingereza na kupewa namba ya usajili 3424504, ikimilikiwa na Triennex (PTY) LTD ya Afrika Kusini yenye asilimia 50 ya hisa za kawaida na Msajili wa Hazina (Treasury Registrar) akiwa na asilimia 50.

Kwa upande wa Tanzania, Dk. Slaa alisema Meremeta ilipewa Hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) Oktoba, 1997 lakini akasema kwamba Meremeta ilifilisiwa Uingereza Januari 2006.

Hata hivyo, Dk. Slaa ameeleza kwamba pamoja na kampuni hiyo kufilisiwa nchini Uingereza, hakuna ushahidi kuwa kwa upande wa Tanzania kampuni hiyo imefilisiwa au la kutokana na kutajwa katika marejeo mbalimbali kuwa moja ya makampuni yanayozalisha dhahabu.


“Taarifa na takwimu muhimu kuhusu Sekta za Nishati na Madini’, ya Julai, 2007, inaonyesha kuwa Meremeta bado inafanya kazi, na inazalisha tani 2.27 za dhahabu. Kama Serikali inasema Meremeta imefilisiwa na mali zake kuhamishiwa Tangold hali hii inaelezwa vipi? Taarifa hizi za utata zinaashiria nini?” alihoji Dk. Slaa.

Maelezo mengine yanayoibua utata zaidi na ambao Kamati ya Rais inayopitia mikataba ya madini itapata wakati mgumu kuitolea taarifa ni kuhusu Meremeta kudaiwa kuwa ni kampuni iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia JWTZ, Kikosi cha Nyumbu wakati ikiwa imeandikishwa nchi ya kigeni.

Taarifa ya awali ya wakaguzi waliokagua BoT, Juni 2006, ziliibua sakata hilo la Meremeta pamoja na kashfa nyingine lakini haikuweza kufahamika ripoti hiyo ya wakaguzi ilivyoyeyuka na kutoanikwa hadharani kabla ya wakaguzi wengine wa nje kuibua suala la EPA pekee miongoni mwa uchafu mwingi ndani ya BoT na serikalini.

Taarifa hiyo ya wakaguzi ilibainisha kwamba serikali ilitoa fedha hizo kiasi cha Sh. bilioni 155 kwa njia ya dhamana ya hazina ambayo inatakiwa kulipiwa riba ya asilimia 14.92 kila mwaka lakini hakukua na makubaliano yoyote rasmi kati ya Serikali na Meremeta hali inayoibua zaidi utata na kuonyesha hakuna njia yoyote ya kuweza kuzipata fedha hizo.

Ndani ya BoT bado kuna mianya mingi ambayo huenda ikaendelea kuibuka siku hadi siku hususan baada ya Bunge kuonyesha njia kwa kushughulikia sakata la umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani, sakata lililosababisha kuanguka kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekua Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Source: Kulikoni, Na.330, Jumatano Mei 14, 2008
 
Hiki kigugumizi kinatoka na TU na kuwa, wote wenye usemi katika hili walikuwa wanahabari na kinachoendelea, sasa watafanyaje masikini? ni kusubiri tu upepo mbaya upite.

Hata kama ni wewe, umefanya mwenyewe, au mwanao au kaka yako, anatafutwa na polisi utatoka kifua mbele? ujitoe ukamatwe, au umtoe mwanao ua nduguyo wa kufa na kuzikana? si rahisi jamani, inahitajika nguvu ya nje!!!

JF NDIO NGUVU, WAPINZANI NDIO NGUVU, MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI, NCHI MARAFIKI,
inabidi tuwe na msukumo mkubwa hadi wa-crumble. There is no way watajiachia wenyewe tu kukamatwa au kukamatana.
 
vitu kama hivi ndo unakuta upande mmoja wa jamii ya tanzania unataka kujtenga! kwa sababu hawaoni faida ya kuwa na serikali iliyopo!
 
Haya ndo makampuni wanayotumia kuamisha hazina za watanzania kuingiza kwenye account binafsi na kuyafilisi.
 
watanzania walio wengi wanaugua gonjwa liitwalo MNYONG'ONYO ambalo linawafanya kuwa mashabiki wa mafisadi badala ya kuwachukulia hatua.

Ninaibeza kauli ya pindwa kuwa chonde chonde kuwa ufisadi usihusishwe na chama, naomba twende wote ktk physics hii...:- Kiongozi wa kiwango cha waziri ni matokeo ya sera nzuri na makuzi ya kiuongozi ndani ya CCM, na kila jema alifanyalo chama kinachukua sifa kwa jema hilo, na utendaji wake woote hutawaliwa na miiko na taratibu za kichma, na mkiona waziri anahulka za kifisadi bsi mfahamu kuwa hayo pia ni matokeo ya makuzi ndani ya chama, Siamini kuwa eti waziri ashiriki ufisadi akisha pata uwaziri tu, bali tabia hii imejengwa na siasa za kimakundi ndani ya ccm ambapo ili uweze kupigiwa kura za maoni ni shurti ujifisadishe ndipo utaonwa, na kingine ni kuwa kama kiongozi ameshindwa ni chama kimeshindwa, haiwezeani eti timu ya taifa ifungwe halafu tuseme kufungwa huko nchi haihusiki wala haiguswi na kipigo hicho bali kufungwa huko ni matokeo ya maandalizi duni ya kuokoteza yasiyo na chembe ya utashi chanya.

Next time ndugu yangu Pinda, jitahidi kutenda zaidi ya kunena maana wewe si mwanasiasa na usijaribu kuwa mwanasiasa au la, white head atakucheka.
 
Sheria zipo za kuwashughulikia hawa mafisadi lakini waliopewa hiyo dhamana hawataki kufanya hivyo.
 
Sheria zipo za kuwashughulikia hawa mafisadi lakini waliopewa hiyo dhamana hawataki kufanya hivyo.

Nakumbuka MKuu Rev. Kishoka alisha maliza hili tatizo hatuna watawala makini.

Itatakiwa siku tukiwapata kazi ianzie hapo hapo wote watarudisha tu. na hayo makampuni hayahitaji hata masaa 6 kujua wamiliki wake.
 
meremeta2.jpg


Baada ya kutoka kwa mara ya kwanza tumepata mwitikio mzuri na ambao umetusaidia kuziba mapengo kadhaa. Maoni ya watu mbalimbali yametufanya tuupdate ripot hiyo kwa hiyo hata kwa wale walioipata ya awali waiangalie hii mpya hasa kwenye maeneo ya EO na Tanzania na vile vile juu ya mapendekezo yetu katika sehemu ya mwisho.

Tunatumaini mjadala sasa uko tayari kuanza na kuipima ripoti hii kikosoaji. Na isambazwe na kuwa "Cheche".

Kuna mambo mengine vile vile ambayo tunayashikilia mkononi kusubiri hatua zitakazochukuliwa miongoni mwao ni orodha ya ndege zote za V. Bout ambazo zimekuwa zikitumika katika usafirishaji wa bidhaa na silaha katika eneo la maziwa makuu.

Tunaendelea vile vile kupokea taarifa yoyote mpya ambayo itaziba mapengo mengine ili kuchangia katika kitabu chetu kijacho cha Historia ya Uporaji wa Raslimali zetu kuanzia Loliondo hadi Meremeta!

Nitakuwa tayari kujibu maswali yoyote hapa kuhusu ripoti hii; maswali ambayo yanaweza kujibika hapa.
 

Attachments

  • MEREMETAREVEALED.pdf
    907.1 KB · Views: 1,903
  • Vielelezo-Meremeta.pdf
    288.9 KB · Views: 1,387
Last edited:
Back
Top Bottom