Mengi ni mfano wa kuigwa au wa kuogopwa?

Bravo777

Member
Jul 5, 2009
13
0
Juzi nilimshangaa mbunge mmoja alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Habari na kudai eti Mengi ni 'mfano wa kuigwa' katika kushughulikia maslahi ya wafanyakazi. Ukweli ni kwamba waandishi wa habari ndani ya IPP Media wanateseka sana kwa kucheleweshewa au kutolipwa kabisa mishahara kiasi cha wengi wao kuacha kazi na kukimbilia vyombo vingine. Nawajua waandishi kadhaa ambao wameondoka IPP huku wakiwa bado wanadai malimbikizo ya mishahara na stahili nyingine ya siku nyingi, miezi kadhaa. Anawatumia waandishi kujiendeleza yeye mwenyewe kibiashara, halafu anawatosa kiaina, wengi wao bila hata kuwalipa stahili yao! Mfano wa kuigwa? Hiyo ni kichekesho.

Huyu hawezi kuwa mfano wa kuigwa, bali wa kuogopwa sana. Nasubiri wapambe wake waingie humu kumtetea ili niweke mambo yote hadharani, tena kwa SERIES.
 
Back
Top Bottom