Mengi awataja wanaompa kiburi

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Katika taarifa ya habari ya juzi usiku, Mzee Mengi aliwataja watu watatu wanaompa ujasiri wa kupambana na ufisadi. Alikuwa akijibu swali juu ya wapi na nani anampa ujasiri. Alimtaja Mwenyezi Mungu, Rais JK na Maskini/wanyonge kuwa ndiyo nguzo za ujasiri wake.

Kati ya nguzo alizotaja nina wasiwasi na ya Rais JK. Lakini jinsi alivyomtega ni vigumu JK kukubali au kukataa hadharani kuwa yeye ni nguzo ya Mzee Mengi.

Eti Wana-JF, mnaonaje kuhusu jibu la Mzee Mengi, JK kweli ni nguzo iliyo upande wa wapinga ufisadi au ni ngao ya adui zetu (mafisadi)?
 
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.
 
You never know. There is a lot of behind doors politics going on. Maybe it's true JK is on his side or maybe he is just using it as a bluff. Either way, the fact that he is so openly courageous shows that he does have people he believes have his back. Lets wait & see.
 
Fisadi Mengi apewa kiburi na Mwenyekiti wa Chama cha Mafisadi. Amedhihirisha kuwa he is one of them fisadis. Halafu mnamwita mpiganaji, mpiganaji vita dhidi ya ufisadi.

Kawaruka kweupeee kalaghabaho.
 
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.

Mlalahoi,

Mengi hawezi kutomtaja JK kama Raisi; akifanya hivyo ataonekana anakwenda kinyume na juhudi ndogo za Serikali zilizofanyika mpaka sasa.
 
Politics!

Tangu mwanzo tulishakuwa na wasiwasi nae! there is no way ukamtaja JK, wakati kwawekwa na KAGODA, then ukasema RA fisadi JK msafi, there is no way!

mlioupande wake haya na nyie JK anapigana na mafisadi? miaka minne sasa! tunaposema JF ni critical thinkers nadhani kila mmoja awe prpud na hii motto, then you have to show and lead! sio kuchukuliwa na upepo.

There is no way Mengi leo aliyeua vyama vya siasa akaonekana shujaa! no way kama hujui go back 1994/1995 !!
 
Anaposema JK anamaanisha Julius Kambarage Nyerere siye huyu aliyefutikwa mifukoni mwa mapapa wa mafisadi.
 
Inawezekana kuwa JK anampa ujasiri kutokana na kushindwa kwake kufanya lile ambalo jamii ilitarajia kuwa angefanya kama Rais hivyo Mengi anafanya hilo kwa niaba yake.
 
Sioni kama JK anafanya juhudi zozote kujinasua na kashfa ya kuwekwa madarakani na KAGODA. hii inaonyesha ni kweli KAGODA ilifanya kazi yake.
 
Waberoya,

Mimi ni miongoni mwa wale tuliokatishwa tamaa na serikali kutumia kodi zetu kuwaandalia makao ya hadhi pale Keko wale wezi. Tangu hapo, sioni ni kitu gani kitanishawishi kuwa serikali hii kweli ina dhamira yakupambana na ufisadi. Ni usanii tu!
Lakini hili la Mengi kuua vyama vya siasa, unaweza kutusaidia tulio gizani?
 
Mimi nafikiri JK ametajwa kama kiwakilishi tu cha serikali, ila practically...nay! Anauma na kupuliza, he is trying hard to save two masters (with different interests of course) at a time, wananchi and the wafisadis...
 
Sidhani kama JK yuko nae katika nafsi yake kabisa kwa dhati anamfanyia unafiki tu.
 
JK amelala fofofo kwenye vita dhidi ya uchafu wake mwenyewe (ufisadi). Mengi anatumia nafasi hii kumtaja kama njia ya kumfikishia ujumbe kwamba alitakiwa kuwa macho kazini. JK yumo kwenye ufisadi, sio mpiganaji. However, Mengi hawezi kusema raisi wenu ni fisadi maana ataswindwa jela kilaini na vita itaishia hapo. Dola haichezewi bwana, inaheshimiwa. Kamwulize ze utamu for details.
 
Politics!

Tangu mwanzo tulishakuwa na wasiwasi nae! there is no way ukamtaja JK, wakati kwawekwa na KAGODA, then ukasema RA fisadi JK msafi, there is no way!

mlioupande wake haya na nyie JK anapigana na mafisadi? miaka minne sasa! tunaposema JF ni critical thinkers nadhani kila mmoja awe prpud na hii motto, then you have to show and lead! sio kuchukuliwa na upepo.

There is no way Mengi leo aliyeua vyama vya siasa akaonekana shujaa! no way kama hujui go back 1994/1995 !!

Nakumbuka ITV ilikuwa ikionyesha picha za mauaji ya Rwanda na wakieleza kuwa wananchi wakichagua upinzani tanzania itakuwa na mauaji kama hayo.

Lakini mi nadhani hapa ilikuwa ni suala la biashara kwa sababu matangazo yale yalikuwa yanalipiwa na CCM
 
Mwenye mapenzi akiona PENGO uita MWANYA......
Kwani hayo yalikuwa matangazo ya kampeni au biashara mpaka yalipiwe na CCM? au ndio mambo ya kufikirika mnatuletea hapa.......
 
Fisadi Mengi apewa kiburi na Mwenyekiti wa Chama cha Mafisadi. Amedhihirisha kuwa he is one of them fisadis. Halafu mnamwita mpiganaji, mpiganaji vita dhidi ya ufisadi.

Kawaruka kweupeee kalaghabaho.

Nadhani ni vizuri kuchangia hoja ambayo umeifanyia kazi...!! Nina wasi wasi na wewe..:rolleyes:!!
 
Politics!

Tangu mwanzo tulishakuwa na wasiwasi nae! there is no way ukamtaja JK, wakati kwawekwa na KAGODA, then ukasema RA fisadi JK msafi, there is no way!

mlioupande wake haya na nyie JK anapigana na mafisadi? miaka minne sasa! tunaposema JF ni critical thinkers nadhani kila mmoja awe prpud na hii motto, then you have to show and lead! sio kuchukuliwa na upepo.

There is no way Mengi leo aliyeua vyama vya siasa akaonekana shujaa! no way kama hujui go back 1994/1995 !!

Waberoya hapo umesema sawa kabisa. Unajua kitu ambacho nimekigundua kwenye majadiliano haya ni kwamba watu wengine wanajisingizia kupingana na ufisadi kumbe wanapigania maslahi yao. Watu wanamtetea sana Mengi kwamba anapambana na ufisadi wakati yeye mwenyewe anajielekeza na kujipambanua na kiongozi wa ufisadi yaani JK. Mengi anapewa kiwanja na Rais city centre anamuuzia mhindi, halafu baadaye anakuja kusema hawa wahindi ni mafisadi. Sasa hapa anatofauti gani na Mtikila aliyekuwa anakwenda kuvuta kwa Rostam halafu kwenye TV anawaponda magabacholi. Wote hawa ni mafisadi tu. Zamani walikuwa wakifanya ufisadi wao na hao wahindi/waarabu halafu wanakuja kuwasema wakijua kuwa hao wahindi/waarabu wataaogopa kwenda kwenye media. Sasa siku hizi wanakwenda kwenye media na hivyo mafisadi wanaamua kuumbuana wao kwa wao. Mengi anapojifaragua kwa Kikwete ni kwamba hataki CCM ishindwe kwa sababu anajua ikishinda utajiri wake utaangaliwa vile vile. Hivyo yeye anataka kumpa karata Kikwete ya kushinda 2010.

Mengi lazima aambiwe kwamba unafiki ni aina mojawapo ya ufisadi tena wa hali ya juu mno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom