Mengi awataja wanaompa kiburi

Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.

Kwa kifupi ni kuwa Mengi nae ni FISADI ndio maana anapewa nguvu na JK ambaye anaendesha serikali ya KIFISADI.
 
Msaada wandugu eti JK na RA ni mashemeji?yaani JK kaoa dadake RA aneishi Dubai?msaada wakubwa nipo kijijini saaana na kimodem changu kina run bankrupt
 
Kwa nionavyo Mengi ana maana kubwa sana kumtaja JK,inawezekana amemtega.
Tena mtego mmoja mbaya sana !!!Nina uhakika mkubwa kabisa Mengi anajua anachokifanya..

Na nadhani yote anayo zungumza Mengi atakuwa kesha yafanyia kazi kwa muda mrefu na sasa anayatoa moja baada ya jingine ili akijua analenga alichodhamilia.

Je tunadhani kwamba Mengi hajui kwamba JK ndio nembo ya UFISADI Tanzania..I am sure he knows...Anachofanya ni sawa na Kumcharaza mtoto wako bakora kisha kumpa pipi machugwa afyonze..!!
 
Kwa kifupi ni kuwa Mengi nae ni FISADI ndio maana anapewa nguvu na JK ambaye anaendesha serikali ya KIFISADI.

kama ni hivyo basi ina maana kila mtanzania ni fisadi.

Tuongee ukweli jamani japo sina uhakika Mengi ametoa fedha nyingi kupeleka watoto India kutibiwa moyo. Je Rostam aziz mbali ya kumpa hela Mtikila ni lipi amefanya japo kuonyesha kwamba kile alicho tuibia anarudisha angalau 0.001%.

Mengi ni mfanya biashara aliye huru lakini Rost-tam Aziza ni mwizi, tapeli, jambazi, muua albino, n.k.
 
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.

President amekuwa siku zote anasema tena hadharani kwamba anapambana na ufisadi. Hivyo mimi, wewe, Rostam, Mkuchika na Mengi kumuunga mkono ni wajibu. Mengi hajakosea!
 
Mengi anapigana hii vita strategically ameamua kumuingiza JK vitani whether anataka au hataki! Jk ndio kasika mpini kwahiyo haitakiwi si tushike makali bali kuushika mkono wake hata kama yeye hataki..!
 
kama ni hivyo basi ina maana kila mtanzania ni fisadi.

Tuongee ukweli jamani japo sina uhakika Mengi ametoa fedha nyingi kupeleka watoto India kutibiwa moyo. Je Rostam aziz mbali ya kumpa hela Mtikila ni lipi amefanya japo kuonyesha kwamba kile alicho tuibia anarudisha angalau 0.001%.

Mengi ni mfanya biashara aliye huru lakini Rost-tam Aziza ni mwizi, tapeli, jambazi, muua albino, n.k.

Juzi mbagala angalau Manji kajitutumu, RA sijasikia kapeleka.

RA yeye anafadhili CCM tena kwa hela nyingi na pia nina hakika Igunga atakuwa kapiga tafu sana!
 
Ushahidi upo kuwa, JK amewachoka jamaa zake, japo aliwahi kula nao hapo mwanzo. Anachofanya sasa ni kutumia third party kuwalima "washkaji" Labda anacopy system ya Wamarekani, usiwe na mshkaji wa kudumu.
who's more suitable kwa hili than Mengi. So my fellow wananchi, don't raise ur hope kwa sana yaani. Kidogo tu, kwani mapambano haya ni magumu. Kama alivyowahi kusema Bosi wa takukuru, (mlinzi wa mafisadi) ukiamua kuwakamata mafisadi wote, basi nchi itakufa!!
 
Hilo ni kanyaboya. Huyu mzee anamtumia JK kama ngao lakini hamaanishi. Kwani huwezi kuwa umezungukwa na mafisadi mpaka kwenye familia harafu wewe usiwe. Unaweza usiwe lakini ukafaidika na matunda ya ufisadi. Hivyo huyu mzee anamtumia kama shield ili asema na jamaa waufyate.

JK kama anadhani kuwa nyota yake inang'ang'aa kachemsha kwa sababu anatumiwa tu.
 
Mengi is so smart, wait you will see! taratiiiiiibu mpaka kitaeleweka.
 
Hapo ndipo anapokosea.JK hawezi kuwa inspiration ya mapambano dhidi ya ufisadi.Instead,yeye ni sehemu muhimu ya ustawi wa mafisadi.

Naungana na maoni yako mia kwa mia. I hope Mengi knows that Jakaya is part of the problem!
 
Waberoya,

Mimi ni miongoni mwa wale tuliokatishwa tamaa na serikali kutumia kodi zetu kuwaandalia makao ya hadhi pale Keko wale wezi. Tangu hapo, sioni ni kitu gani kitanishawishi kuwa serikali hii kweli ina dhamira yakupambana na ufisadi. Ni usanii tu!
Lakini hili la Mengi kuua vyama vya siasa, unaweza kutusaidia tulio gizani?

Nadhani Mugezi amekujibu japo amejichanganya, ITV walipita vijiji vingi na kuonyesha mauaji ya kimbari Rwanda na Burundi, sio siri hizi picha mpaka leo ninazo akilini, niliziona mnazi mmoja! 94/95

kama tunafanya analyisis zetu careful, mwamko wa watu kuhusu upinzani mwaka 95 ulikuwa juu, na kama Mrema hakushinda, basi may be next years tungetegemea matokeo bora zaidi!

Vijijini bado wanazikumbuka hizi picha (believe me) na inahitajika vyama vya upinzani kuondoa hii image!.kumbuka mjini tunapiga kelele lakini vijijini ndio kuna wapigakura wengi na huwa wanaenda kupiga kura, hakuna foleni kule!
 
Mengi is so smart, wait you will see! taratiiiiiibu mpaka kitaeleweka.

Nani ana nguvu ya kuwashinda mafisadi kati ya Mengi na JK?? naona ama anamtukana JK, JK ana kila kitu ni rais jamani! unless kama anaanisha Nyerere kama wengine walivyosema!
 
Mengi anatumia tactic ya 'devide and rule". Amemuweka JK "on spot". Bila shaka JK hawezi kukubali wala kukanusha jibu la Mengi. Lakini ukweli moyo wa Rais wetu uko na mafisadi papa. Yeye kama Mwenyekiti wa chama tawala alipokea mchango wa Tshs. 400 milioni toka kwa Tanil Somaiya kwenda UV-CCM wakati anajua fika SFO ya UK inamtuhumu ufisadi wa Rada? Tell me your friend and I will tell you what you are.
 
Lakini ni vyena tukapambana na hao vinara wa juu wa ufisadi na kuweza kuelimishana hadi mitaani kuwa ufisad ni matumizi mabaya ya rasilimali na jasho letu vinavyotumika vibaya na wachache wanaodhani sisi wengine ni mambumbu then tujipange kuchague Viongozi watakao tusaport. Na watakao kuwa ma ndumi la kuwili tutawajua na kuwaaibisha kwa njia hiyihiyo ya umoja wa mapambano, nadhani hakuna haja ya ku suspect kuwa nani mpambanaji wa kweli na nani siye, TIME WILL TELL
 
Juzi mbagala angalau Manji kajitutumu, RA sijasikia kapeleka.

RA yeye anafadhili CCM tena kwa hela nyingi na pia nina hakika Igunga atakuwa kapiga tafu sana!

Shangazi, Igunga ni choka mbaya. Nilikwenda huko week chache zilizopita. Sikuamini kuwa Mbunge wao ndiye FISADI mkuu katika nchi hii. Yaani kule ni umasikini wa hali ya juu ndio unaoonekana dhahiri.
 
Katika taarifa ya habari ya juzi usiku, Mzee Mengi aliwataja watu watatu wanaompa ujasiri wa kupambana na ufisadi. Alikuwa akijibu swali juu ya wapi na nani anampa ujasiri. Alimtaja Mwenyezi Mungu, Rais JK na Maskini/wanyonge kuwa ndiyo nguzo za ujasiri wake.

Kati ya nguzo alizotaja nina wasiwasi na ya Rais JK. Lakini jinsi alivyomtega ni vigumu JK kukubali au kukataa hadharani kuwa yeye ni nguzo ya Mzee Mengi.

Eti Wana-JF, mnaonaje kuhusu jibu la Mzee Mengi, JK kweli ni nguzo iliyo upande wa wapinga ufisadi au ni ngao ya adui zetu (mafisadi)?

Anaposema JK anamaanisha Julius Kambarage Nyerere siye huyu aliyefutikwa mifukoni mwa mapapa wa mafisadi.

Umejuaje kama anamaanisha Mwalimu Nyerere...? Raisi JK kwani ni nani?
 
Mengi is so smart, wait you will see! taratiiiiiibu mpaka kitaeleweka.
Ukiangalia wakati anawataja mafisadi tarehe 23 Aprili, utaona jamaa pamoja na kuwa anadai JK anampa kiburi lakini wote aliowataja wana ukaribu kabisa na JK.

Katika video hizi unaweza kung'amua kitu.

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=nj5RN-xHwlQ]YouTube - Mengi s Press Conference on 23 April 2009 Part I[/ame]

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=rDMD8nOBfEo]YouTube - Mengi s Press Conference on 23 April 2009 Part II[/ame]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom