Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Hilo ni kanyaboya. Huyu mzee anamtumia JK kama ngao lakini hamaanishi. Kwani huwezi kuwa umezungukwa na mafisadi mpaka kwenye familia harafu wewe usiwe. Unaweza usiwe lakini ukafaidika na matunda ya ufisadi. Hivyo huyu mzee anamtumia kama shield ili asema na jamaa waufyate.
JK kama anadhani kuwa nyota yake inang'ang'aa kachemsha kwa sababu anatumiwa tu.
Mkuu Mugenzi, Mengi hana ubavu wa kumuanika JK hata kama angekuwa na kila ushahidi wa lolote ambalo angeweza kulianika. Mkuu, JK ana immunity, ni kiongozi mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote. Huwezi kwenda public na kumsema hovyo ukaendelea kutesa mtaani.
Mtu yeyote mwenye akili timamu asingeweza kufanya hivyo kwa uwazi kiasi hicho.Mbinu ya kumshirikisha JK katika mapambano haya, yanamuweka Mengi kwenye hali ya usalama zaidi.
Nakumbuka kusikia miaka ya nyuma viongozi wa Afrika walikuwa wakitumiwa delegation (wanapokwenda kinyume na matakwa ya nchi za magharibi) kuambiwa kuwa usalama wao hautakuwa na guarantee. Mkuu Mengi anahitaji guarantee ya usalama wake.