Mene mene tekel peres

kuongezea hii, tz tuna viongozi hasa wa serikali wanafiki, na quran imesema kuwa ukitaka mjua mnafiki na imesisitiza kuwa heri mchawi kuliko mnafiki, na moja ya sifa za mnafiki ni hizi:
Akiahidi- hatekelezi
akiaminiwa-haamikiniki
hutenda yale asiyo hubiri
swali je ni sifa zipi kati ya hizi asiyokuwa nayo kiongozi yeyote wa serikali ya ccm?

hakuna hata wa ngama
 
Dalili za ufalme uliofitinika:
Kiongozi anaua watu wake.
Kiongozi kupoteza mvuto wa mwanzo.
Mparaganyiko wa mawazo na majadiliano
Kuelewana vibaya kila mahali
Wanyonge wananyanyaswa
Mungu haabudiwi tena
Ufisadi ni mtindo wa maisha
Hata ndani ya JF mawazo mazuri yanapingwa kipumbavu!!!!!!!

Kaka umeongea wewe, we acha tu!
 
lakni pia Mungu huangalia mtu na siyo chama na huwa anaangusha ufalme na majesh yake kisha kumnyanyua mnyonge na mara zote mnyonge kwake hutoka katika kundi lisilotarajiwa kama vile Daudi. hivyo ujiandae kwa ufalme wa tz kwenda kwa mtu tusiyemtarajia kabisa kwa maneno yako.
 
Upande wa pili wa mzani wako umeweka nini? Mawe au imani na je imani gani, je tanzania ikombolewe kwa imani au imani ip? Ingawa ujumbe mzuri sana lakini imani ya pili haita kuelewa. Asane ujumbe mzuri
 
Kama umejifunza biblia vizuri sina shaka umewahi kuona maneno haya, ''mene mene tekel peres'' maana yake '' Mungu ameuhesabu ufalme huu, umepimwa katika mizani na kuwa umepungua, watapewa Wamedi na Waajemi" cha ajabu ninachotaka kuzungumza hapa ni kuwa maneno hayo yaliandkwa ukutani na kiganja cha mkono usio na kiwiliwili kwenye sherehe kubwa ya mfalme tajiri (Belteshaza) mwenye kiburi na asiyemtukuza Mungu na mwenye kunyanyasa watu, usiku huo huo mfalme huyo aliuawa na watu wake walitekwa na utawala mwingine wa Wamedi na Waajemi ukasimama.

Kuna masuala magumu yanayokabili taifa letu sasa halafu kuna viongozi wanatumia akili zao zote na nguvu zao zote kutetea waliosababisha maafa yanayotukabili, watu wengi wanaumia kwa ajili yao bila huruma, nakumbusha 'mkono wa Mungu unaandika mioyoni mwao kuwa wanapimwa katika mizani na uongozi wao umefika mwisho' Mungu ibariki Tanzania.
CCM writing on the wall
 
Dalili za ufalme uliofitinika:
Kiongozi anaua watu wake.
Kiongozi kupoteza mvuto wa mwanzo.
Mparaganyiko wa mawazo na majadiliano
Kuelewana vibaya kila mahali
Wanyonge wananyanyaswa
Mungu haabudiwi tena
Ufisadi ni mtindo wa maisha
Hata ndani ya JF mawazo mazuri yanapingwa kipumbavu!!!!!!!
ukiona hivyo ujue mwisho dunia umekaribia,sali sana kwa dini yako ili usije ukawa miongoni mwa watakao unguzwa na moto mkali.LAKINI MIMI NIMECHAGUA KUTO KUKATA TAMAA,
 
Back
Top Bottom