Mene mene tekel peres

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Kama umejifunza biblia vizuri sina shaka umewahi kuona maneno haya, ''mene mene tekel peres'' maana yake '' Mungu ameuhesabu ufalme huu, umepimwa katika mizani na kuwa umepungua, watapewa Wamedi na Waajemi" cha ajabu ninachotaka kuzungumza hapa ni kuwa maneno hayo yaliandkwa ukutani na kiganja cha mkono usio na kiwiliwili kwenye sherehe kubwa ya mfalme tajiri (Belteshaza) mwenye kiburi na asiyemtukuza Mungu na mwenye kunyanyasa watu, usiku huo huo mfalme huyo aliuawa na watu wake walitekwa na utawala mwingine wa Wamedi na Waajemi ukasimama.

Kuna masuala magumu yanayokabili taifa letu sasa halafu kuna viongozi wanatumia akili zao zote na nguvu zao zote kutetea waliosababisha maafa yanayotukabili, watu wengi wanaumia kwa ajili yao bila huruma, nakumbusha 'mkono wa Mungu unaandika mioyoni mwao kuwa wanapimwa katika mizani na uongozi wao umefika mwisho' Mungu ibariki Tanzania.
 
Wewe ni m adventista? maana mambo ya ufunuo wachache huelewa alama za nyakati hizo. Bravo!
 
Umenena vyema. Afrika tulipaswa kuendelea kwa haraka zaidi kuliko bara lolote la ulimwengu huu. Kila siku tunajifunza historia. Unajua kulikuwa na Dark period kule ulaya, hali hii ilisababishwa na manyanyaso, ufisadi, kutokuwajibika, kumdharau Mungu, kudharau watu, wizi na viongozi kutetea uovu. Hali hii ilipelekea ulaya nzima kuingia katika vita vya mapinduzi. Katika kipindi hiki watu walikufa sana nauharibifu mkubwa sana wa mali na miundo mbinu ulitokea. Hata hivyo, heshima, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na maendeleo yalitokana na dhiki hiyo.
Hapa kwetu tulipaswa kujifunza mambo haya kupitia historia. Lakini wapi, viongozi wana vichwa vigumu kama mataruma ya reli. Hawasikii, hawajali, hawana habari, na wapuuziaji wakubwa. Ila sasa wakati umefika, naamini kilichotokea ulaya kinakuja hapa kwetu.
Uwezekano wa hali hii kutotokea upo, kwani Uingereza iliepuka hali hiyo. Na kutoingia katika hali hiyo kulitokana na vingozi wake kubadilika na kuwa naheshima, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na kuleta maendeleo.
Naomba Mungu afanye muujiza kama ule alioufanya kwa nchi ya Uingereza. Mungu ibariki Tanzania.
 
Unamaana kuna wakristo wasiruhusiwa kusoma biblia?

Biblia ni kubwa Shossi, kama Quran wapo wanaosoma tu kama hadithi alafu basi, kumbe yaliyoandikwa ni mambo halisi aidha yaliyokuwako au yatakayokuwako. Maarifa ana ufahamu zaidi anao ndio maana ameuliza japokuwa sitamjibu hapa.
 
Kama umejifunza biblia vizuri sina shaka umewahi kuona maneno haya, ''mene mene tekel peres'' maana yake '' Mungu ameuhesabu ufalme huu, umepimwa katika mizani na kuwa umepungua, watapewa Wamedi na Waajemi" cha ajabu ninachotaka kuzungumza hapa ni kuwa maneno hayo yaliandkwa ukutani na kiganja cha mkono usio na kiwiliwili kwenye sherehe kubwa ya mfalme tajiri (Belteshaza) mwenye kiburi na asiyemtukuza Mungu na mwenye kunyanyasa watu, usiku huo huo mfalme huyo aliuawa na watu wake walitekwa na utawala mwingine wa Wamedi na Waajemi ukasimama.

Kuna masuala magumu yanayokabili taifa letu sasa halafu kuna viongozi wanatumia akili zao zote na nguvu zao zote kutetea waliosababisha maafa yanayotukabili, watu wengi wanaumia kwa ajili yao bila huruma, nakumbusha 'mkono wa Mungu unaandika mioyoni mwao kuwa wanapimwa katika mizani na uongozi wao umefika mwisho' Mungu ibariki Tanzania.

hapa sitarajii kusikia mambo ya udini tena, maana mods nao samtaimz NOOO!!!
 
Biblia ni kubwa Shossi, kama Quran wapo wanaosoma tu kama hadithi alafu basi, kumbe yaliyoandikwa ni mambo halisi aidha yaliyokuwako au yatakayokuwako. Maarifa ana ufahamu zaidi anao ndio maana ameuliza japokuwa sitamjibu hapa.

Alaa una maana waislam wanasoma tu hawajui wanasoma kitu gani? mimi mwenyewe Mwislam lakini ndio kwanza nasikia maneno hayo kwako.
 
Alaa una maana waislam wanasoma tu hawajui wanasoma kitu gani? mimi mwenyewe Mwislam lakini ndio kwanza nasikia maneno hayo kwako.

ivi kwa nini mnamsikilizaga sana shehe sharifu?

wamama, wababa, wabibi, wababu, wajomba, washangazi, watoto, woooooote!

uwa mnakusanyika kumskiliza yule dogo.
 
ivi kwa nini mnamsikilizaga sana shehe sharifu?

wamama, wababa, wabibi, wababu, wajomba, washangazi, watoto, woooooote!

uwa mnakusanyika kumskiliza yule dogo.

Tukuulize wewe lini mara yako ya mwisho uliona waislam wamejazana wanamwangalia huyo unaemsema? na mbonamie simjui unaweza kunifahamisha wapi anapatikana?
 
Alaa una maana waislam wanasoma tu hawajui wanasoma kitu gani? mimi mwenyewe Mwislam lakini ndio kwanza nasikia maneno hayo kwako.

We Bwana mbaya sana! unapenda udini! usinichonganishe na waislam wala wakristo, form four ulipata nini kwenye kiswahili (A au F)? Hapo namaanisha kama Biblia ilivyo kubwa na Quran pia ni kubwa na wengi wanasoma kama hadithi badala ya kujifunza maagizo yake. nikija Korogwe utaona amaa!.
 
Alaa una maana waislam wanasoma tu hawajui wanasoma kitu gani? mimi mwenyewe Mwislam lakini ndio kwanza nasikia maneno hayo kwako.

Kwa kuwa sikupenda ulivyoandika narudia tena hata kwenye bandiko langu sikutaja mkristo wala mwislam na ndio maana sikutaka Maarifa ajue mimi ni dini gani kwani nia hapa ni kuelimishana na kueleza yanayotusibu, nakutaarifu kuwa Biblia na Quran inasomwa na watu wote wenye haja ya kujifunza mambo ya imani. Weweee!
 
watanzania tunaogopana. Mpaka sasa nsha ona kila mtu au tulio wengi tunahitaji kufanya mapinduzi lakini nani aanzishe?
 
sredi nzuuuuuri lakini watu wanaiharibu

Dalili za ufalme uliofitinika:
Kiongozi anaua watu wake.
Kiongozi kupoteza mvuto wa mwanzo.
Mparaganyiko wa mawazo na majadiliano
Kuelewana vibaya kila mahali
Wanyonge wananyanyaswa
Mungu haabudiwi tena
Ufisadi ni mtindo wa maisha
Hata ndani ya JF mawazo mazuri yanapingwa kipumbavu!!!!!!!
 
Kuongezea hii, TZ tuna viongozi hasa wa serikali wanafiki, na Quran imesema kuwa ukitaka mjua mnafiki na imesisitiza kuwa heri mchawi kuliko mnafiki, na moja ya sifa za mnafiki ni hizi:
Akiahidi- HATEKELEZI
Akiaminiwa-HAAMIKINIKI
Hutenda yale asiyo HUBIRI
Swali je ni sifa zipi kati ya hizi asiyokuwa nayo Kiongozi yeyote wa serikali ya CCm?
 
Back
Top Bottom