Meli za kivita za Japani zawasili

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Meli tatu za kivita za Jeshi la Wanamaji kutoka Japani zimewasili nchini na kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.


Kuwasili kwa meli hizo kuliambatana na kupigwa mizinga ya baridi 21 huku zikiingia kwa zamu kuanzia saa tatu asubuhi ambapo mpaka kufikia saa nne asubuhi zote zilikuwa zimeshatia nanga.


Meli hizo zilizokuwa zimebeba mabaharia 1,176, zitakuwa nchini kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya mafunzo kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya kijeshi.

Kiongozi wa meli hizo, Rear Admiral Hidetoshi Funchnoue, alisema kuwa katika ziara hiyo watafanya mazoezi ya matukio ya dharura katika meli za vita kama vile majanga ya moto na uharibifu wa nchi huku zikiwa bandarini.

Balozi wa Japani hnchini, Masaki Okada, alisema meli hizo zilipaswa kuja mwaka jana wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
 
safi kwa kutuhabarisha,yule mama wa malawi ase fyoo aone moto wake sasa,
 
wakati wa uchaguzi mkuu wachina walikuja namna hii...janja ya ccm kutisha wamalawi
 
Maandalizi kwa ajili ya vita ya majini na malawi sio....good news wajeshi wetu wapunguzwe vitambi
 
Nasikia hatua inayofuata ni kutengeneza mfereji mkubwa kutoka bahari ya hindi mpaka lake Malawi, au siyo?!
Maandalizi kwa ajili ya vita ya majini na malawi sio....good news wajeshi wetu wapunguzwe vitambi
 
Siamini kuwa hii ni kuwatisha Malawi, huu mgogoro umepamba moto ndani ya takribani mwezi mmoja, maandalizi ya kufanya joint military exercise au tour yoyote hufanywa kwa muda mrefu. Hii ni coincidence tu.
 
Back
Top Bottom