Meli ya MV Spice Islander, yazama ikelekea Pemba; wengi wahofiwa kupoteza maisha

sawa mkuu,,, hakuna haja ya kubishana sana kwa sasa,,, kama great thinkers, lets wait kwa hiyo idadi kamili,, tuzidi kuwafariji ndugu zetu walioptwa na msiba huu,,, pole zangu za dhati pia kwa rafiki yako ambaye baba yake na mdogo wake pia walikuwepo kwenye meli hiyo

na nchi hii ilivokuwa masikini............wamekata umeme tangu saa 12 na nusu.

ngoja tusubiri habari za saa mbili usiku (kupata taarifa za tukio la jana usiku).
 
Hizo taarifa kama nilivyosema hapo awali ni estimates..inaweza ikawa less au sitoshangaa ikawa more

kwa taarifa yako nimepewa habari baba yake rafiki yangu na mdogo wake wamo kwenye hiyo meli

sasa unaposema habari za kutaka umaarufu mie wa nini kwenye janga kama hili?
Asante kwa taarifa ndugu Slidingroof. Hard to imagine the shock in people who saw their loved ones boarding that boat last night.
 
Mkuu, Director1, tupo pamoja ndugu ya nimekupata sote tunajenga nyumba moja

mkuu tushindane kwa hoja hakuna haja ya hasira,nchi ni yetu wote kushindana ni muhimu ili kuharakisha demokrasia yetu
 
Dah poleni sana ndugu zetu........

Hivi bado hatujifunzi au ndio viongozi wameweka pamba masikioni!!.........why why why why why?
 
idadi kamili sijui kama tutaipata kamwe..MV Bukoba mpaka leo nani anajua idadi kamili ya abiria waliokumo kwenye meli na walio kufa..
 
ngoja tusubiri nazi yetu kama itaahirisha safari ya kwenda kunywa kahawa na Bush Washington
Kule Misri ubalozi wa Israel umevunjwa.Baraza la mawaziri la Misri limeitisha kikao haraka kujadili.Obama naye kapiga simu Misri kutaka kujua imekuwaje.
Watu wanaokufa wanatia majonzi sana lakini mpaka wawe wamekufa kwa UGAIDI na wawe wazungu hata wakiwa wachache.
 
Kule Misri ubalozi wa Israel umevunjwa.Baraza la mawaziri la Misri limeitisha kikao haraka kujadili.Obama naye kapiga simu Misri kutaka kujua imekuwaje.
Watu wanaokufa wanatia majonzi sana lakini mpaka wawe wamekufa kwa UGAIDI na wawe wazungu hata wakiwa wachache.

habari mpya hii,mkuu mimi ni mkristo lakini nimetokea kuchukia wazungu kuliko kabila yoyote ile,hayo mambo ya far east yatatuletea matatizo makubwa snaa
 
Kule Misri ubalozi wa Israel umevunjwa.Baraza la mawaziri la Misri limeitisha kikao haraka kujadili.Obama naye kapiga simu Misri kutaka kujua imekuwaje.
Watu wanaokufa wanatia majonzi sana lakini mpaka wawe wamekufa kwa UGAIDI na wawe wazungu hata wakiwa wachache.

yaani hii habari hata ukienda Google kuchungulia hupati... kweli bado tuko nyuma kimaendeleo
 
inasikitisha poleni sana wazanzibari kwa msiba huu mkubwa

Kiukweli hapa viwanja vya maisara huzuni tupu, huu ni msiba kwa watanzania wote sio wanzanzibari tu kwa walioguswa na mv bukoba wanajua uchungu wa ajali kama hii.
Taarifa za hv karibuni kuwa kundi la mwanzo la majeruhi na maiti wamepakiwa katika boti ya sea express na inaelekea bandarini malindi ili maiti zipelekwe maisara na majeruhi hospitali ya mnazi mmoja
 
Kwa wanaoifahamu ni boti iitwayo "Mv Spurs", imezama na abiria wanaokadiriwa kufikia 300 huku uwezo wa boti ni abiria 200-250. Imezama sa8 usiku ikiwa kwenye safari zake za kawaida. Natoa pole za dhati.
Sio boti ni meli...
 
KUna vitu sidhani kama viko sawa hadi taarifa zitakapokuwa zinakuja sawasawa.. Hiyo meli inaukubwa gani maana kusema watu 2,000 siyo meli ndogo hata kidogo na kama ilikuwa ya mizigo basi ni lazima kunahitajika maelezo zaidi. Binafsi I have a feeling kuwa meli haikuwa na watu 500 unless haikuwa na mizigo mingi na ni kubwa sana.

So twende pole pole tupate habari zaidi na sote tunajua katika mazingira kama haya na katika hali ya mashaka na ni usiku baadhi ya taarifa hazitakuwa sahihi sana. Hadi hivi sasa tunajua vitu vichache:

a. Kuna meli imezama
b. Kuna watu wamenusurika na wanaendelea kuokolewa
c. Kuna waliopoteza maisha
d. Hatujajiandaa kukabiliana na majanga kama haya, usiku, majini n.k

Ninasema hayo yote kwa sababu MV Victori ina uwezo wa watu 1200 na tani 200 na ninaamini ndiyo meli kubwa zaidi ya abiria nchini. Naweza kusahihishwa.
 
Back
Top Bottom