BinMgen
JF-Expert Member
- Jun 18, 2008
- 1,854
- 262
kunataarifa meli ya abibiria (spice) itokayo Unguja kwenda Pemba imezama katika mkondo wa Nungwi mwenye taarifa kamili atuwekee.
Updated Posts:
_________
__________
__________
__________
_________
_________
Updated Posts:
_________
_________TAARIFA RASMI: Waliookolewa jumla yao ni 545 ambapo Sea Express iliokoa 292, Super Sea Bus iliokoa 198 na Boti ya KMKM iliokoa watu 55.
source Jussa
Tunawashukuru sana kuwa kutupa mkono wa pole wana JF,tumepata pigo kubwa sana ambalo halijawahi kutokea,hivi hebu liangalieni hilo meli ni kweli la kupakia abiria ?
Hivi viongozi wetu wapo au wamelala,leo hii wametupa msiba mkubwa sana,tumepoteza vipenzi vyetu,ndugu zetu,watoto wetu,wazee wetu,inshallah allah atatulipia,mungu awalaze pema walifariki katika ajali hii ameen, na awape uzima wale walijeruhiwa ameen.
__________
Updated images by member:
__________
Mh. Kikwete katangaza siku3 za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoti na amefuta ziara yake ya kwenda canada,pia dr. Shein katangaza maombolezo yasiku3 zenj kwamsiba huu mkubwa wazaidi ya watu 1000, Innalilahi waina lilahi raajiuun.
__________
hadi hivi sasa 620 wameokolewa, 189 wamefariki. uikoaji bado unaendelea.
__________
Kwa hisani ya ZANTEL Zanzibar Update
LIST OF SURVIVORS
Zantel offers its deepest condolences to the Nation and all those affected.
In the interest of the general public, Zantel will be constantly updating this page with the list of Survivors as soon as we have more information.
*Update as per Mnazi Mmoja Hospital
ORODHA YA WALIONUSURIKA
Zantel inatoa salaam za rambirambi kwa wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika janga hili.
Katika jitihada za kusaidia umma kwa ujumla, Zantel itakuwa ikitoa orodha ya majeruhi kadri ya majina yatakavyopatikana.
*Orodha hii ni kama inavyotolewa na Hospitali ya Mnazi Mmojas.
ORODHA YA WALIONUSURIKA HAPA!
_________
DKT BILAL, ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MELI ZANZIBAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia leo, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati alipofika kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Baada ya hapo Makamu wa Rais alitembelea katika Viwanja vya Maisala na kutembelea shughuli za kiusaidia na kutambua maiti waliopatikana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
_________