Mdogo wangu aikosa ndoa kisa michirizi

Sikiliza,huyo jamaa hampend mchumba wake kwa zati tena n bora kaonesha dall mapema kabla hawajafunga ndoa sasa ni nyny kujiongeza,iv kwel kwa mtu unaempenda kabsa ata akiwa chongo utaendelea mpenda hvohvo mfano saiv akapungu na michrz ikaondoka kabsaaa wakafunga ndoa badae akanenepa na michrz ikarud inamana atamuacha tena si ndivo?Aisee nyie ndg wa huyo bnti ltazameni sana hl huyo sio mtu sasa wa kumkabz ndg yenu,ktk maisha kunamabadlko yanatokea ktk maumble yetu kwa hyo mwenzako akbadlka tu bas mnaachana?ebo bas dunia hii ndoa zngkua hazfk miaka ata3.kiufup huyo jamaa anatafuta sababu tu ya kujchomo yamkn kapata mwngne,
 
Wakuu habari za w,keend,

Wakuu naombeni ushauri juu ya huyu mdogo wangu,

Mdogo wangu ana mchumba wake ambae alishafanya proses zote za ndoa, ilibaki kumsubiri dogo amalize chuo wafunge ndoa.

Sasa tatizo limekuja mdogo wangu baada ya kumaliza chuo, amejiachia sana yaani kanenepa alafu kawa na michilizi kiunoni mpaka kwenye makalio na inavyoelekea inaendelea kumtoka maana anaviashiria kama inaendelea kumtoka hadi mapajani.

Sasa baada ya jamaa kumuona hivyo mchumba wake anamwambia jitahidi hiyo mistari ikutoke hangaika kama ni gharama nitalipia lakini hiyo mistari siitaki kuiona mbona wakati unasoma ulikua modo huna hiyo mistari kama ikishindwa kutoka mimi na wewe basi, mimi hiyo mistari inanitisha.

Dogo kanisimulia nikazani utani, kumbe jamaa yupo serious. Sijakaa vizuri huyu jamaa ambae ni shemu wangu akaniibukia mpaka Tanga. Anasema nipo serious na hii inshu jitahidi ukae na mdogo wako umsaidie apake dawa gani ili kuondoa hiyo mistari alafu ni mingi.

Wakuu dogo week ijayo anakuja kwangu nimsaidie maana mimi ndo dadaake mkubwa, alafu harusi ilipangwa mwezi wa na nane na jamaa kama hivyo haelewi somo.

Msaada please kuinusuru ndoa ya mdogo wetu.
huyo hampendi maana hata akimuoa c ataongezeka,ina maana atamuacha tena,mdogo wako atateseka tu huyo jamaa anachagua sana mwambie ampende alivyo vinginevyo tupa kule.
 
Kuna dawa za kuondoa michirizi, pia anaweza kuanza kupiga tizi ili kupunguza unene
 
Hivi Madame B na wewe upo hapa bize kuchangia hii mada ya michirizi na sio kumshauri huyo binti asepe?

Kama kuna kitu kwa mwenza wako na hukipendi kwanza jiulize swali hili;
Je, Kinaweza kubadilika? (Can I change it?)

Kama kinabadilika msaidie kukibadili na sio kumtupia yeye lawama. Kama kanenepa kidogo, amka naye asubuhi nenda naye mazoezi. Kama ni katabia kapya, kabla hakajakomaa kuwa active kumsaidia kukiacha. Kamwe usimpe mwenza wako mzigo wa, "Usipo..basi nita..." Mtu yeyote anayetumia sentensi hiyo ujue siku nyingi sana alishafanya maamuzi na keshachukua hamsini zake.

Kama hakiwezi kubadilika ujiulize, je, kinaathiri upendo wangu kwake? (Is it a deal breaker to me?) Kama ndiyo basi mweleze wazi na usepe. Kama siyo deal breaker kwako basi muombe Mungu akupe busara na hekima ya kukivumilia na kumchukulia mwenza wako kwa upendo ule ule.

Wewe dada Vero usimtese mdogo wako kisa sijui kamsomesha wala sijui alikuwa mwanaume wake wa kwanza. Mapenzi sio masharti.

Lakini ushauri mwingine kwa vijana wote walioko kwenye mahusiano na wanaotarajia kuingia kwenye mahusiano. Someni 1 Wakorintho 13:1-8. Hapo ndipo utapata maana halisi ya upendo. Hapo utaweza kujipima mwenyewe na kumpima mwenza wako. Hakuna kipimo kingine kizuri cha upendo kama hiyo mistari.

Kila la kheri.
Amen barikiwa Bro
 
Akimbie sana, vyakula vya mafuta aache, wanga na protein kdogo, vitamin za kutosha na atafte suplements za kupoteza uzito
 
Pole kwa mdogo wako.. ila huyo jamaa sio muoaj aiseh.. ila dawa mwambie apake maji ya viaz mbatata vilivyomenywa yale maji yanayo bak mwishon wakat wa kuosha viaz yanakuwa meupe apake kwa muda wa mwez itaisha.
 
Back
Top Bottom