Mdau kaachwa na mpenzi wake, anaomba ushauri

Sam pizzo

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
846
515
"Bro nina stress ya mapenzi, Kuna Demu wangu nadhani unamjua nampenda sana lakini nakiri yeye alikua akinipenda sana na ni single mother. Nimeishi naye kwa muda wa mwaka na nusu tuliishi kama mke na mume alinipenda sana sana na tunatofautiana utaifa kuna siku aliniuliza unaoa lini mm nikakumuambia nina mpango nikifikisha miaka 30 ndio nilikua nimeplan kuoa na kwa hiko kipindi (mwaka jana ) nikiwa na 28yrs.

Basi sikua nimejua alikua analenga nn kuniuliza hivyo kuna kipindi nilikua namuambia tuzae wote lakini yeye alikua akiniambia ni lini tunaenda home kwetu Tanzania.Nilimuahidi mwisho wa huu mwaka ndio tutaenda akakubali. Nilihama eneo la kazi na kuenda sehemu jirani na huo mji bila kumtaarifu sababu nilikosana na Boss na hiko kipindi yeye Demu wangu alikua ameenda likizo nyumbani kwao ya wiki moja.

Aliporudi alianza kushambuliwa na wafanyakazi wenzake wakidai aliwakataa wao akataka kuwa na mm Mtanzania hatimaye nimemuacha. Ijapokuwa hiko kipindi nilikua kila Sunday nalala kwake na kumletea vijizawadi.Ilipofika mwezi June mwaka huu aliacha kazi akanifuata huo mji ninaoishi tukaanza kuishi kama mke na mume maisha yalikua raha sana ukirudi unakuta umetengewa chakula ukichelewa unapigiwa simu kuwa unakuja saa ngapi.

Hiki kipindi ndio nilitamani kumpeleka home lakini ghafla furaha ilikatishwa siku ameenda kwao home kama siku tatu aliporudi nashangaa usiku anachati WhatsApp kuchukua simu yake hataki tukaanza ugomvi nikampokonya kwa nguvu, basi nasoma hata sikuwa naamini nayoyaona alikua akichat na mwanaume tena akimlazimisha kwamba anataka aende kwake.Niliumia moyoni nikaona huyu ameniona ni kama zuzu nilimpiga Kiasi chake.

Akaomba msamaha akidai hawezi rudia, basi kumbe sikuwa najua nikitoka kwenda kazini yeye anachati na wanaume akitafuta kazi.kuna siku tunaangalia muvi kwenye simu yake ika"pop up" meseji ya mwanaume akimuita baby wangu sikuamini ilibidi nichat na jamaa then akapiga simu tulipandishiana sana na yule jamaa, alianza kulia na kukiri kuwa amekosea ilibidi nitoke nje nipunguze hasira.

Alikuja akinibembeleza niingie ndani lakini nilikataa akidai hawezi ingia ndani kama mm nipo nje.Nilikaa nje kwa muda wa kama nusu saa hivi then nikarudi ndani nikaanza kumuuliza maswali kuhusu huyo jamaa nikaona huyu anaanza kunipanda kichwani nilikumbuka lile tukio lililopita nikashikwa na hasira nilimpiga sana kipigo cha mbwa ilifika mahali nilikuta nimemkaba shingo ilibidi apige ukunga apewe msaada akijua nitamuua.

Nikamuachia nikaanza kujiuliza n NN nafanya hiki. Nikaanza kuomba radhi kwa kumpiga vibaya vile alianza hadi kutoa damu puani nikaona hapa nimekosea sana. nilimpa maneno makali akaanza kulia akidai amenikosea kiasi kwamba anaona hastahili kuwa na mm kwani yeye ni mkosefu sana. Nilikuta naanza kujishangaa imekuaje nimempiga kiasi hiko. Alikaa siku tatu akinihudumia kama kawaida lakini alikua akilalamika nimempiga kiasi hiko na sijamuoa je nikimuoa itakuaje. Hatimaye akasema anaenda kwao mara moja then atarudi.

Tangu alipoenda hakurudi aliniambia alipata kazi pembezoni mwa jiji. Hiko kipindi na mm nikaacha kazi nilikua siko sawa kiakili. Akawa ananipigia akiniambia kuna kazi amesikia kama naweza fanya. Ilipita takribani miezi miwili akanipigia simu akiniambia wazazi wake wanataka aje achukue vitu vyake kwangu then alikuja nikafanya naye mapenzi then akaondoka akirudi pembezoni mwa jiji.Kidogo akaanza kulalamika kazi ni ngumu na hakua ameizoea na mtoto wake anadaiwa ada ya shule nikawa namsaidia vipesa kidogo kwani hata mm hali yangu ni mbaya. Lakini Juzi ikabidi aniambie kuwa ananipenda lakini anaogopa kuja kwangu. Sababu anaogopa nikiolewa na mtu ambaye alimpiga sana nilianza kumbembeleza anisamehe. Then akaniambia ameanza kuwa na mahusiano na mwingine lakini ni sababu ya mm nilipush away hisia zake kwangu na hapendi hayo mahusiano na anahisi amenikosea hawezi kuwa na mm." Mdau anaomba ushauri afanye nn?
 
"Bro nina stress ya mapenzi, Kuna Demu wangu nadhani unamjua nampenda sana lakini nakiri yeye alikua akinipenda sana na ni single mother. Nimeishi naye kwa muda wa mwaka na nusu tuliishi kama mke na mume alinipenda sana sana na tunatofautiana utaifa kuna siku aliniuliza unaoa lini
Japo kuwa ni ngumu lakini inampasa akubali tu kuwa huyo mwanamke hana hisia naye tena na kwa sasa hampendi.

Nini afanye? Aanze sasa kutafuta mwanamke mwingine atakaye mpenda.

Lakini pia aache kupiga piga, Kuna JELA ukiua.
 
Hapo amuache aende tu pia akubari kuwa alimkosea kwa kumpiga na pia akubari kuwa huyo mwanamke hamfai kwa sababu amerudia kosa la usariti mara mbili inaonekana ndio hulka yake.
Ahsante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom