Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Jamani hata mimi pia natoa shukrani nyingi sana kwa forum hii ya JF. Sikusikiliza radio au kuangalia tv lkn nimepata message ya mdaharo, nadhani nimepa kiasi cha 80% ambayo inatosha sana. Sasa naomba Mungu aliyetuumba, anayetupenda sana, atupatie Dr Slaa kuwa kiongozi wa nchi yetu. Amin
 
Dr Slaa amezungumza vizuri sana. Kwa yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania na alibahatika kuangalia kipindi kile ni lazima ampe kura Dr Slaa, vinginevyo mtu huyo haitakii mema nchi yetu. Nilikuwa nimekaa na wadada wawili ambao wote kabla ya mdahalo kuanza walisema kura zao watampa Kikwete na wabunge wa CCM hata kabla ya kipindi kuisha walikuwa wamebadili mawazo na kusema kwamba kura zao watampa Dr Slaa na wagombea ubunge wa chadema. Hongera sana Rais Mtarajiwa Dr Slaa, hongera sana chadema kwa kuwa makini sana katika kampeni zenu zilizowawezesha kuzikonga nyoyo nyingi za Watanzania.
 
Dr Slaa amezungumza vizuri sana. Kwa yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania na alibahatika kuangalia kipindi kile ni lazima ampe kura Dr Slaa, vinginevyo mtu huyo haitakii mema nchi yetu. Nilikuwa nimekaa na wadada wawili ambao wote kabla ya mdahalo kuanza walisema kura zao watampa Kikwete na wabunge wa CCM hata kabla ya kipindi kuisha walikuwa wamebadili mawazo na kusema kwamba kura zao watampa Dr Slaa na wagombea ubunge wa chadema. Hongera sana Dr Slaa, hongera sana chadema kwa kuwa makini sana katika kampeni zenu zilizowawezesha kuzikonga nyoyo nyingi za Watanzania.

Watu wote sasa waka hakiki majina yao kwenye vituo vyao vya kupigia kura ili kujua kuwa utapigia chumba gani, kumekuwa na tabia ya kuhamisha majina na kusababisha mkanganyiko siku hiyo. Kwa hiyo ukijua ni chumba kipi utapigia kura inasaidia sana kuhakikisha unakamilisha jukumu hilo muhimu.
 
Big-up Dr Slaa, mdahalo ulikuwa mzuri sana, yaani naweza kukufananisha na Maalim Seif Sharif Hamad kule Zanzibar
 
Jamani mwenzenu nina raha moyoni mpaka basi. God bless Tanzania. God bless Dr. Slaa


Wewe kama mimi sasa tusubiri Watanzania kuushangaza Ulimwengu kwa kuwaambia walimwengu kwamba ndiyo Tanzania bila thithiem inawezekana kabisa.
 
Ahsanten sana kwa kutupa updates...Naona tumaini jipya limeshawadia...Mungu atakuwa nasi hadi dakika ya mwisho.
 
Raisi wa tanzania kuanzia wiki ijayo dr wilbroad slaa akizungumza katika mdahalo wa leo amesema katika swala la ufisadi na mafisadi hakuna mtu/fisadi atakayeachwa"kila jiwe litageuzwa,"no stone will remain unturned" na pia ameongeza kuwa watanzania wakichagua ccm ni maafa'
 
:frusty:Duhh! Wadau wengi wa jamii forum naona wako nje ya nchi sasa nani atapiga kura?:smash:

Kaka wengine tupo bongo wewe hujui siku hizi mtandao unapatikana anywhere shukrani ziwaendee TTCL, Zantel, na Zain na pia kwenye simu hivyo tuko pamoja katika hili
 
nadhani vibaraka,makada na wadau wa thithiem kama vile thalma,ridhi,miraj,mkamb,jw,jeykey,na kinana wamepata heart attack baada ya kusikiliza mdahalo wa slaa,ile familia ya ikulu sijui iko katika hali gani now

Mkuu inabidi waji-tune tu kuwa maisha yanawezekana hata bila kuwa ikulu. Wamwache Dr. Slaa mwenye uchungu na nchi yake achukue usukani kwa maendeleao ya watanzania.
 
:frusty:Duhh! Wadau wengi wa jamii forum naona wako nje ya nchi sasa nani atapiga kura?:smash:
Umepigwa changa la macho.
Mie nipo bongo tena daresalama lakini nimefuatilia mdahalo online.
Wengi tupo hapa bongo ila ni wasafiri wa kwenda na kurudi. tunaperuzi JF kila tunapofika kwenye kituo.

Long live JF
 
Back
Top Bottom