Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,726
Hivi CUF wanapinga nini? Mke au mme wako bado ni mme wako, awe amelala kwa kukukumbatia au kukupa mgongo, maadam kitanda ni kimoja.
hawa ccm si walikatazwa midahalo???huyo hamad rashid amemuaga makamba?
Asante kwa taarifa
Nataka Hamad awaeleze watanzania kama bado wao ni wapinzani au ndio hivyo tena
sina uhakika sana na hiyo taarifa mana ni mara nyingi ITV Wamekua wakiahidi kuwa na midahalo ya kipindi maalumu cha Dr. Slaa ila baadae haikuwepo ngoja tusubiri.
BIG UP
MZEE GOMEZI
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.
Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.
Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.
Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.
Sure midahalo kama hii ni muhimu kwa zama hizi za ukweli na uwazi, hili ni fundisho kwa CCM, wanaogopa nidagalo kama mama mkwe, wanajua madhambi na uchafu wao.:whoo:
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.
Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.
Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.
Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.
CCM Wakiona huu mdahalo una athari kwao wanapandisha dau ITV mdahalo unafutwa
Kunta Kinte mdahalo maana yake si lazima muwe mnapingana.Hizi siasa zetu jamani! badala upinzani uwe kitu kimoja kupambana na chama tawala kunufaisha maslahi ya wananchi, wanapambana wenyewe kwa wenyewe!Nashindwa ku-imagine jinsi gani baba January anachekelea hili!