Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Hivi CUF wanapinga nini? Mke au mme wako bado ni mme wako, awe amelala kwa kukukumbatia au kukupa mgongo, maadam kitanda ni kimoja.
 
kweli?
sijawahi kuwasikia wote katika mdahalo wowote wakiwa wanajenga hoja!
Lakini mdahalo huo unalenga kupata nini baadae?
Unalenga kuonesha kwamba kiongozi wa upinzani aliyepita ni bora kuliko wa sasa au ?

Sidhani kama kulikuwa na ulazima huo,ila kama topic ni kuhusu ulazima wa kuwa na katiba mpya itapendeza kuwaangalia wote mawazo yao ni yapi katika hilo!
 
sina uhakika sana na hiyo taarifa mana ni mara nyingi ITV Wamekua wakiahidi kuwa na midahalo ya kipindi maalumu cha Dr. Slaa ila baadae haikuwepo ngoja tusubiri.

BIG UP

MZEE GOMEZI
 
Ningependa mdahalo uruhusu wahusika kuulizana maswali na pia kukanushana pale hoja zinapopingana, nisingependa kuona midahalo ya Shaban Kisu wakati wa uchaguzi ya "Mchakato majimboni" Ile haikuwa midahalo mizuri maana ilikuwa inakwepa watu kujibu maswali yanayowalenga wao moja kwa moja na vyama vyao badala yake shaban kisu aliweka maswali ya jumla jumal. Mdahalo (mahojiano ) Ya Dr. Slaa mpaka sasa ndio yaliyokuwa bora kuliko mahojiano yoyote yaliyowahi kufanywa kutokea mbio za uchaguzi 2010 zianze nionavyo mimi. Hata hivyo yanahitajika kuboreshwa zaidi.
 
Nataka Hamad awaeleze watanzania kama bado wao ni wapinzani au ndio hivyo tena

CUF Followers dont give a dam about mambo ya Muungano, they got what they wanted in Zanzibar - Serikali ya Muungano, so CUF and CCM Zanzibar are working together to make sure kwamba hayo Mafuta yaliyogundulika huko yanasimamiwa na Wazanzibar wenyewe na sio Jamhuri ya Muungano. So we shouldnt expect anything from them kwenye mambo ya Muungano. Na sisi Watanganyika inabidi tusimame kidete hadi kieleweke kama kilivyoeleweka Zanzibar. So lao ni moja huko Zanzibar sidhani kama wanajali sana kinachoendelea Tanganyika.
 
sina uhakika sana na hiyo taarifa mana ni mara nyingi ITV Wamekua wakiahidi kuwa na midahalo ya kipindi maalumu cha Dr. Slaa ila baadae haikuwepo ngoja tusubiri.

BIG UP

MZEE GOMEZI

CCM Wakiona huu mdahalo una athari kwao wanapandisha dau ITV mdahalo unafutwa
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.

Ahsante kwa taarifa, lakini mdaharo ungefaa awepo mwakilishi kutoka chama tawala dhidi ya wapinzani. Vinginevyo kama Hamadi awajibie hoja zao
 
fundisho kwa ccm ipi? hujui CUF ni CCM namba 2 tatizo ni majina tu? baada ya miaka mitano CUF itakuwa kwishney ............:eek:
Sure midahalo kama hii ni muhimu kwa zama hizi za ukweli na uwazi, hili ni fundisho kwa CCM, wanaogopa nidagalo kama mama mkwe, wanajua madhambi na uchafu wao.:whoo:
 
Jamani tunaomba mtuwekee clips za live humu ndani ya jamii forum ili waliopo nje ya network washuhudie.
JF.....GO BEYOND BORDERS
THANK YOU WADAU.
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.


Kama ni kweli basi mimi nakuwa sana na mashaka kuhusu umakini wa hawa CHADEMA. Hivi huu mdahalo utatusaidia nini hasa. Huyu HR anaotoka chama cha CUF ambacho ni mpumbavu tu ambaye hawezi kuona kuwa agenda yao ya Uislamu imewageuza CCM B atleast kwa wakati huu ambo baadhi ya viongozi ni moja ya agenda yao. Viongozi wa chadema wanatakiwa wawambie Watanzania na hasa wa bara, kwani huko visiwani wao hawana tatizo kwa sasa, ni vipi kura zimechakachuliwa, mikakati ya kudai katiba mpya, tume mpya ni ipi, na mengine yanayo lalamikiwa, sasa hawaoni kuwa wanapoteza muda bure na wanaacha mambo ya msingi yalioyo mbele yao na mnakumbatia ya upuuzi mtupu.

Hivi viongozi wa CDM hawaoni tayari wamesha poteza umakini? wabunge wao walitoka nje ya ukumbi wa bunge kupeleka ujumbe wa msisitizo wa madai yao, baada ya kutoka nje ya ukumbi walifanya nini cha ziada kutilia mkazo ujumbe huo? jibu ni hakuna. Matokeo yake wameicha agenda hiyo hewani kibaya zaidi wakanyamaza kimya wakiwachia kina Zitto, Shitambala, Shibuda Leticia nk.Wakitumiwa kuwatoa wananchi kwenye jambo la msingi na kuiletea jamii midahalo mingine ambayo haina tija zaidi ya kuendelea kuwapa mafisadi sehemu ya kupumulia na kuwapa muda na fursa zaidi ya kupanga mikakati ya kuimaliza CHADEMA.

Nashindwa kusita kujiuliza kwamba kama umakini wa viongozi wa CDM ni hivi ingekuwa je wachakachuaji wangewaachi wakawa watawala?

Ushauri wangu kwa viongozi wa CDM na hapa nikiwalenga wale ambao ni makin,i ni huu, kama nyie sio wa sanii jueni kati yenu kuna watu wanaendeleza maslahi ya mafisadi na chama choa, kama kati yenu kuna ambao mnania ya dhati kabisa kabisa kuikomboa na kuiokoa nchi hii basi fanyeni hivyo kwa umakini mkubwa mkiitegemea nguvu ya umma ambayo ndio msaada wa uhakika wala si ya hawa vibaraka na vikaragosi vya mafisadi wanotaka kuwapoteza.
 
kwa wenye kutaka kuhudhuria pale moven pick na kuuliza maswali kadi zinapatikana kwa Adeodatus Kakorozya wa EABMTI kwa simu namba 0718 607 403 Nasikia zimeshaanza kutoka sasa mimi nimemuagiza jamaa yangu keshanichukulia dawa ni kuwahi wana Jamvi
 
CCM Wakiona huu mdahalo una athari kwao wanapandisha dau ITV mdahalo unafutwa


Na kweli si mliona juzi MUNGU alivyowaumbua ITV,mtangazaiji wao mwanadada alivyoonekana kumnyoshea mkono mwenzake kwa kasira akimuelekeza kuiondao ile taarifa ya kiongozi wa Kanisa la KKKT, Unafiki unaumbuliwa hapahapa.
 
Mimi sijaelewa mantic ya mdahalo huu ni ninin? nikutueleza kazi,shughuli na muundo wa serikali kivuli bungeni au la! kwanini mdahalo huu uwe kati ya CUF na CDM tu? hapa kitu gani kimelengwa? hivyo tuseme Hamad akieleza vizuri kuliko Mbowe ndio ata kuwa mkuu wa kambi ya upinzani bungeni na kuunda serikali kivuli bungeni? serious I'm confused....
 
Hizi siasa zetu jamani! badala upinzani uwe kitu kimoja kupambana na chama tawala kunufaisha maslahi ya wananchi, wanapambana wenyewe kwa wenyewe!Nashindwa ku-imagine jinsi gani baba January anachekelea hili!
Kunta Kinte mdahalo maana yake si lazima muwe mnapingana.
 
Back
Top Bottom