MCs, Wapiga Picha, Make-up artists n.k na matumizi ya Picha zetu

Wakuu, Habari za muda huu?

Leo nakuja kwenu na hii mada ama sijui niite tabia ama vipi. Yaani kumekuwa ni kawaida sasa ya makundi haya: Wapiga picha, watu wa make up, ma-MC, mafundi nguo etc. Yaani wao wanakupa huduma na unalipia na bado wataku-post kwenye Mitandao ya Kijamii (Social Media) kila sehemu.

Kama alikuwa mpiga picha basi utajikuta kila mahali, au kama alikuwa MC wako basi naye atapost picha za sherehe nzima kwa jinsi alivyopiga picha yeye au kuchukua video. Inafika wageni waalikwa mnajikuta huko mitandaoni. Kama alikushonea nguo vivyo hivyo, kama alikupaka makeup naye ni yale yale.

Na kuna wale umenunua nguo, kiatu etc basi kwa kuwa anakujua, siku ukivaa tu hicho kitu labda ukapost bila hata kuwatag. Watakuja hapo “asante kwa kutuchagua” “asante kuturuhusu tukuhudumie” au watachukua picha wakapost kwao na maneno kibao. Je, kama mwenyewe nilikuwa sitaki watu wajue nimenunua kwenu?

Ni nadra kukutana na wanaokuuliza/muuliza mwenye tukio lake kabla hawajapost.

Kwa kweli hii tabia inakera sana, bora hata pangekuwa na makubalino au punguzo la bei katika huduma zao. Mkubaliane kabisa kwamba atatumia picha zako kutafutia wateja hivyo mkubaliane bei kabisa. Sio nakulipa kila kitu halafu mara paaa! picha zimejaa mtandaoni au ukiamka siku inayofuata unakuta familia nzima mpo mtandaoni.

HOJA YANGU:
Jamani hii ni sawa?

Ulinzi wa data upo wapi? Hivi watu wanajua kwamba wana haki juu ya picha/taarifa zao? Hivi wenye matukio wanajua kwamba wanaweza kataa kupostiwa, wanajua ni haki yao kuruhusu au kukataa? Na hao wanaoposti wanajua ni kosa bila ridhaa ya mhusika?

Nini maoni yako?
Una point ya msingi.
 
MCs wa maharusi kurusha picha na video za watu kwenye page zao bila ruhusa za wahusika. Ipo siku watashtakiwa na kudaiwa fidia ndio watanyooka.
 
Umeongea jambo la muhimu sana.
Kwanza nikiwa mdau wa tasnia hii napenda kukutoa tongotongo kadhaa.

Moja, kuna sheria inayomlinda mtu yeyote dhidi ya matumizi yapicha zake popote endapo hakuomba idhini, ikiwa hata kupigwa picha.

Pili, baadhi ya wateja wetu huwa tuna waomba, kuwa tutatumia baadhi ya picha zao kiofisi.

Tatu, baadhi ya wateja hupenda kupostiwa kutokana na tukio zuliloingia mkataba.

Nne..
 
Nashukuru sana. Kama kuna makubaliano ni sawa mkuu. Au kama mteja kataka mwenyewe pia sio tatizo.

Vipi wale wanaopiga picha kwenye sherehe za watu na wanaziuza kwa nje hivi, kama huna hela picha hupati kabisa. Huwa sielewi kabisa yaani
 
MCs wa maharusi kurusha picha na video za watu kwenye page zao bila ruhusa za wahusika. Ipo siku watashtakiwa na kudaiwa fidia ndio watanyooka.
Kwa kweli ipo siku litawakuta jambo…
 
mi nishawahi kumuwakia mtu, nilitengeneza saa ya mtu kama zawadi na ni surprise si nikakuta kaipost kwenye mitandao yake bila makubaliano!! sema tu hjuwa na hela nilimsamehe kidogo nimdai fidia!!
😂😂😂😂 mkuu umenichekesha. Kwa kweli atakuwa kajifunza kwa hilo
 
Hivi anapotjmiq picha yako...anakulipa au anakupa discount????
Mkuu sidhani, labda ndio hiyo kuombwa kutumia ama ujikute tu ushawekwa😃

Kuna harusi moja nilisimamia bana, wee yaani kesho yake picha zimejaa kwenye page ya Mc, nikawauliza maharusi wala halikuwa tatizo kwao kabisaaa na wamelipia huduma vizuri tu. Nilikoma🥲🥲
 
Nashukuru sana...
Vipi wale wanaopiga picha kwenye sherehe za watu na wanaziuza kwa nje hivi, kama huna hela picha hupati kabisa. Huwa sielewi kabisa yaani
Inaitwa BINGO.

Imepewa jina la BINGO sababu ni sawa na ile kamali unayocheza ya bingo ya pata potea.

Hawa jamaa wanaopiga hizo picha kwanza ni njaa, pili wanafanya biashara ya pata potea, yaani kuna wakati analipa studio shs 10 alafu anapata shs 7.

Pili hawo jamaa wanafanya vile ikiwa na maana hawajaingia mkataba na wenye sherehe ila wanaomba kwa kamati ya ulinzi siku ya sherehe, ujue zile picha za mkataba wageni waalikwa huwa hawazipati so hawa wanaitwa (wapiga bingo au zangazanga nk) wanawapa ndg, jamaa, marafiki, wageni waalikwa picha zao za kumbukumbu ya sherehe.

Wewe ukionw picha yako alafu ukawa huna pesa ya kuigomboa basi unaiacha tu.
 
Miez mitatu imepita Silent ocean walitumia picha yangu kwenye kutangaza biashara wakat nikiwa napokea bidhaa zangu na nilishawalipa kila kitu wametumia sura yangu bila makubaliano hivi nikiamua kuwadai 500M kama fidia sitoboi kweli?
 
Kuna yule bibi harusi wa katokisha amepostiwa mpaka kwenye Nigeria webs kwamba mume yuko busy anacheza yeye yuko busy anakata keki halafu amenuuuunaaaaaa na keki amekata karibia sahani nzima halafu mapande mkubwa makubwaa.....comments za waja ni negative tu...
Sasa hii si kudhalilishana tu jaman
 
Miez mitatu imepita Silent ocean walitumia picha yangu kwenye kutangaza biashara wakat nikiwa napokea bidhaa zangu na nilishawalipa kila kitu wametumia sura yangu bila makubaliano hivi nikiamua kuwadai 500M kama fidia sitoboi kweli?
Nenda kirafiki kwanza, ukiwa umetunza copy zenye picha zako, wakikuzingia na wewe wazingue.
 
Back
Top Bottom