Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA akamatwa na Jeshi la Polisi.

Watu hawa maarufu kama machinga ni watanzania ambao baada ya ya serikali yao kushindwa kuwawekea miundo mbinu ya ajira wakaamua kujiajiri kama machinga.sasa unataka kuwaachisha shughuli hiyo bila kuwapa mbadala ili WAKAKABE MTAANI?

 
Mtumwa ni wewe ambaye muda wote unatetea kila kitu CDM wanachokifanya hata kama ni cha kipuuzi. Inabidi mkuu ubadilike, jifunze kuwa na mawazo huru. Kwa stahili hii CDM hawajengi bali wanazidi kubomoa na kujichimbia kaburi lao wenyewe!

Acha unafiki wewe...sasa kama serilikali yako inatoa elimu ambayo watu wanashindwa kujitegemea, wanajianzishia biashara ndogo ndogo halmashauri haziwaruhusu kufanyia mjini, unataka wafanyie wapi? ccm is no more, subirini 2015.
 
Anatafuta umaarufu kwa nguvu sana huyu mchungaji. Badala ya leo kuwa kanisani na kondoo wa bwana, yupo busy anahatarisha amani ya nchi.

Naona sasa ni wakati wa kuwawajibisha viongozi wa aina hii ili iwe fundisho na kwa wengine.

Wangemkamata kwa kosa lingine. Kwa hili nawahakikishia wanaendelea kuwapa umaarufu chadema
 
Duu masikini taifa letu linaelekea pabaya ila naonea huruma vijana wenzangu tusikubali kutumika km vichaa sioni umuhimu wa vurugu kwan mazungumzo yananafas kubwa ktk utatuz wa kero mbalimbali za wananchi jaman lengo la upinzan sio hilo msidanganye vijana.
 
Anatafuta umaarufu kwa nguvu sana huyu mchungaji. Badala ya leo kuwa kanisani na kondoo wa bwana, yupo busy anahatarisha amani ya nchi.

Naona sasa ni wakati wa kuwawajibisha viongozi wa aina hii ili iwe fundisho na kwa wengine.

Wewe na hao mashaitwan wa kijani hakuna tofauti! Nenda kapokee malpo ya tshirt na kofia njaa itakuua!
 
Hivi chadema hawana njia nyingine ya kupiga siasa zaidi ya kuchochea vurugu na maandamano? Huyu msigwa anataka asikike tu ndio maana anachochea vurugu iringa. Iko siku viongozi wa chadema watavua nguo hadharani ili wasikike kwani hizi vurugu wananchi watazichoka na kutakuwa hakuna njia nyingine ya kuwafanya wasikike.

wanapenda kukamatwa na polisi ili waandikwe magazetini

Teh teh teh.....Comment hii naifananisha na maneno ya mtu kama Nape au Mwigulu kwani hayana mshiko, nimesikitishwa sana kuona kuwa kijana kama wewe unakuwa muoga wa kuonyesha hisia zako kwa kukataa kuonewa hususani kunyanyaswa watu unao waongoza. Ndio maana kila siku umekuwa kigeugeu.......Huwezi kuwa kiongozi wa watu kama utaiogopa polisi hususani polisi ya CCM. Unapenda kuandika nonsense kama hii ili uonekane upo CCM. BADILIKA.
 
Mkuu mimi binafsi huyu Msigwa nashindwa kumuelewa
Anafanya vurugu kwa makusudi ili na yeye aandikwe kama yule kubwa jinga wa Arusha.
Anyway, mwisho wake ni 2015 kwani nitahakikisha anarudi kuuza kisosk pale kihesa

Kubwa jinga ni wewe ambaye hujioni kuwa ni wewe kikwazo cha watu kukosa haki.
 
Taaarifa kutoka Iringa zinasema mbunge wa Jimbo la Iringa Peter Msigwa wa CHADEMA amekamatwa na jeshi la polisi muda huu na yuko chini ya Ulinzi wa jeshi hilo.

Mchungaji Msigwa amekamatwa kwa amri ya Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Michael Kamuhanda kwa madai kwamba anawaunga mkono wafanyabiashara ndogondogo wa manispaa hiyo Machinga wanaopambana na polisi wanaowakataza kufanya biashara mjini.

Mchungaji Msigwa amekuwa mtetezi mkubwa wa wafanyabiashara ndogondogo kiasi kwamba kila anapoonekana maeneo ya manispaa hiyo hujikuta gari yake ikisukumwa na Machinga hao.

Itakumbukwa ni wiki iliyopita tu mbunge wa viti maalum Chadema Chiku Abwao alimshambulia vikali Waziri William Lukuvi kwamba analitumia jeshi la polisi Iringa kukandamiza Chadema na viongozi wake.

Mchungaji Msigwa ambaye pia ni mbunge machachari wiki iliyopita ametishiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufikishwa mahakamani kwamba amemtuhumu kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu.

kwa mafanikio aliyoyapata Msigwa kufikia kutembelea VX mwacheni achachawe maana si mchezo
 
Wabunge wa cdm wasipoangalia wengi wao watapoteza uhai wao kwa kufanya mambo kwa kishabiki bila kufuata taratibu!

hatutaki watu waoga humu bwana kuweni na mawazo ya mbali na fuatilieni matamko ya serikali, nchi hii imeshazama huwezi kuiokoa kwa kicheko. nina waswas wewe ni mkazi wa dar maana diyo waoga sana nchi hii
 
Mwisho wa siku mchungaji Msigwa atakuwa shujaa mbele ya wanyonge, tatizo lipo wapi kuwaruhusu machinga wapige mzigo siku 2!! Ukizingatia ni week end na serikali itapata mapato kwa kukusanya ushuru.


Pengine tutajua undani baadaye. Kwa sasa mimi nalioana kama tatizo la Mgongano wa Mamlaka. Serikali, ambayo inawakilisha mawazo ya CCM ipo upande mmoja ikitaka kuonesha bado ina nguvu ya kufanya maamuzi, wakati upande wa pili una wananchi, ambao kiutaratibu Msigwa ndiye msemaji wao.Wananchi wanataka na wao waeleweke kuwa wana maamuzi.

So inakuwa kama ni mgongano wa Mamlaka mbili ambazo mjinga mmoja kashindwa kuzi-reconcile. And Who is that? Hili ni tatizo la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa nionavyo mimi. You don't solve the problem by sending cops. You solve it kwa kutambua power bases na kuziwezesha kukubaliana. Reconcile the power bases! In meetings....

Hii nchi kuna watu wanapewa madaraka wana akili ndogo kweli kweli yaani. Hapo Iringa lazima kuna kitu hizo power base zinaweza kukubaliana kufanya. Hivi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Iringa ni nani? Alisomea kitu gani shuleni, na chuo gani hasa. Au ndo wale waliopewa kazi za serikali kubalance dini wakati kichwani hamna kitu? Reconcile the power bases fools! In meetings....
 
Kwa jicho hili la husuda toka kwa mkuu wa mkoa,lazima atumie mabavu ya Polisccm
 
CHADEMA ikiingia madarakani mambo yote ya kijinga yanayofanywa na haya mambwa ya ccm yataisha. maana wanaowapa kiburi leo cha kunyanyasa raia na mali zao hawatakuwa na sauti tena.
 
Hii style ya maandamano na kusababisha sintofaham kwa raia wengine haina mantiki kabisa,hebu wapinzani tuje na mbinu mpya ya ku tackle problem za wapiga kura wetu,nakumbuka mbinu hii tullitumia miaka ile ya 1995 tukiwa na NCCR-Mageuzi kisha ikahamia TLP na baadae ikatumiwa na CUF lakini ukianglia kwa makini hazukuleta mabadiliko yoyote,hivyo sioni ajabu kwa CDM kwani haitafaa kitu kama kule nyuma
 
Back
Top Bottom