Mchungaji Mtikila atoa Kali

Sasha Fierce

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
361
5
1236091616_mtikilaweb.jpg



Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, leo aligeuka kioja baada ya kutinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, akiwa amenyuka suti kali na tai lakini miguuni akiwa amevaa kiatu kimoja cheusi na kandambili nyekundi huku akitembelea mkongojo.Hali hiyo iliibua kimbembe Mahakamani hapo kiasi cha kuwafanya watu kusahau hata kufuatilia kesi kubwa ya ufisadi inayowakabili Yona, Mgonja na Mamba.Akionekana hana ‘tyme’ na mtu, Mtikila alitinga hadi katika chumba cha mawakili na kuwasabahi Yona, Mramba na Mgonja.

Mwandishi aliamua kumstopisha Mwanasiasa huyo mkongwe na kumuuliza kulikoni alikuwa ameripuka kwa staili hiyo, ambapo alijibu kuwa mnamo Februari 16 akiwa nchini Zimbabwe alivamiwa ndani na Joka kubwa aina ya Kobra ambalo lilimg’ata mguu, lakini hakuweza kupata matibabu kwa siku tatu ingawa alikuwa anakesha na kuomba.Wakati mtandao huu ulipokuwa ukichonga na Mtikila watu kibao wakiwemo mawakili, walikuwa wamemzunguka wakimshangaa ikiwa ni pamoja na kucheka, lakini hali watu walizidi kuvunja mbavu baada ya kueleza kuwa alikaa siku tatu bila matibabu na alipona bila kutibiwa .

“Du! Mchungaji huyu kwa kamba ‘Fix” hajambo, inawezekaba vipi mtu ukapona baada ya kung’atwa na Kobra mwenye sumu kali bila matibabu? Labda aling’atwa na nge, maana Kobra ni masaa machache tu mtu anavuta”alisikika kijana mmoja akisema.
 
Kwakwakwaaaaahhghhhh! Duh kweli hapa Reverend Mtikila katoa kali! Hii inapaswa iingie kwenye ZE KOMEDI, 2009!
 
Hii kali ya mwaka na je ni kesi gani ilimpeleka mahakamani? naje Zimbabwe alikwenda kwa shughuli gani?
 
Fix nyingine za kitoto. Siku tatu bila matibabu na kapona. Sasa mkongojo wa nini. Alichoka kuomba au hakujumuisha kurejeshewa nguvu mguuni?
 
1236091616_mtikilaweb.jpg



ambapo alijibu kuwa mnamo Februari 16 akiwa nchini Zimbabwe alivamiwa ndani na Joka kubwa aina ya Kobra ambalo lilimg’ata mguu, lakini hakuweza kupata matibabu kwa siku tatu ingawa alikuwa anakesha na kuomba.

Ni kwanini mnakuwa na imani haba? Yeye aliomba sumu kali ya nyoka SWILA isiwe na madhara juu yake, tatizo liko wapi?
 
Mtikila anazeeka vibaya wakubwa!alikua anataka kuwavuta watu wa media sana sana,ili walau wananchi tujue NA JAMAA NAE YUPO!tehe tehe tehe tik.

TUMEMSHTUKIA HUYU MZEE!ni vema akaonyeshwa MLANGO WA KUTOKEA.siasa za kizazi hichi naona HAZIMFAI TENA.aungane na wazee wenzie wastaafu kupumzika
 
...na eti kuna watu wanampigia kura mtu kama huyu awe rais, duh!!!
 
Jamani kupona kwa maombi is possible - na labda alipona KUFA - yaani sumu haikumuua -
so tusibishe sana - si ndio ile miujiza?? au mnadhani miujiza inafanyika sehemu fulani fulani tu - kama mikutanoni, makanisani??? NO - hata ukiwa peke yako Mungu anatenda miujiza na hiyo ndiyo ya hizi LAST DAYS -[ be informed]
 
Tarime mbona alienda Hospitali kushonwa baada ya kupopolewa mawe?, si angefanya maombi. Huyu jamaa muda wake umeisha, alivuta baadhi ya watu enzi zake za kutetea walalahoi dhidi ya Magabacholi, kumbe walikuwa (magabacholi) wakipita mlango wa nyuma anachukua chochote, sasa kaisha.
 
Haya akiyazungumza Kanisani kama kawaida yao watamuamini, kwa nguvu za bwana, aleluja, Ameen.

Kanisani kunavituko vingi zaidi ya hivyo
 
Kwanini hawakumuuliza angevaa kiatu badala ya ndala kungetokea nini. Au ukigongwa na nyoka huyo mguu unakuwa mzito?
 
Haya akiyazungumza Kanisani kama kawaida yao watamuamini, kwa nguvu za bwana, aleluja, Ameen.

Kanisani kunavituko vingi zaidi ya hivyo

Msikitini mnazungumza habari za mtume muhamad kuoa mtoto wa miaka sita.
msikitini kutakuwa na vituko zaidi kama maustadhini wenu wataamua kuwapa hadithi zote za mtume wenu feki.
 
Msikitini mnazungumza habari za mtume muhamad kuoa mtoto wa miaka sita.
msikitini kutakuwa na vituko zaidi kama maustadhini wenu wataamua kuwapa hadithi zote za mtume wenu feki.

umejuaje kama mtoa hoja ni mwenda msikitini? we kweli kabonde, na akili yako pia kabonde.
 
Kweli mtikila naona kiroho chake kiko juu jamani .......huenda akachana na siasa sasa aeneze neno la bwana kwani huo ni muujiza mkubwa... Mtikila muombee Balali afufuke aje atueleze ziliko Fedha...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom