Mchungaji Gwajima Kuueleza Umma Kesho kuhusu Mkenya wa Ulimboka

oooooh, kumbe ni vile vikanisa vyetu pale Tanganyika packers? Hivi ni vikanisa vya CCM na mara nyingi kila Jumapili vinakuwa na mgeni rasmi toka CCM kutoa neno! Kwa maana hiyo hivi vikanisa ni idara ya TISS? Watu hawaogopi kumchezea mungu!

Umekosea hapo, sio vikanisa vya CCM. Tuliache hilo halina ushahidi
 
kweli ndiyo pale Dr. aliposema "tunahitaji voingozi wenye hofu ya mungu" sasa naona serikali yetu haina hata chembe ya hofu kwa mungu ndio maana wanatumia hata madhabahu takatifu ili kujinufaisha na kuwafanya watu wa mungu wawaamini ili waendelee kutenda maovu. ''wanatafuta kibali cha kufanya maovu kupitia madhabahu takatifu."
 
1.Ni "mchungaji" huyu huyu aliyetumika katika kampeni za
chama hapa nchini.

2. Ni "mtekaji/mtesaji" huyu huyu aliyetubu katika kanisa
lake!

3. Si ajabu kusikia jambo hili limehusianishwa na "vyama
vingine" kwa sababu tu ya kuhusisha sababu ya kwanza
na ya pili hapo juu.

4. Nia itakuwa inafanikiwa kuwahadaa wa-TZ kwa mambo
yasiyo na msingi ili "kuwasahaulisha" tu katika chanzo cha
mambo yenyewe(MADAI) ya madaktari.
 
oooooh, kumbe ni vile vikanisa vyetu pale Tanganyika packers? Hivi ni vikanisa vya CCM na mara nyingi kila Jumapili vinakuwa na mgeni rasmi toka CCM kutoa neno! Kwa maana hiyo hivi vikanisa ni idara ya TISS? Watu hawaogopi kumchezea mungu!

Umenena vyema mkuu, Nape naye alishakwenda huko na kuna thread humu, ama kweli the movie is starting soon..... Kwi kwi kwi... Where is my popcorn bag!
 
Ha ha ha ha haaaa Kumbe ni Gwajima!!! Kova atueleze kwanza uhusiano wake na gwajima alafu mengine ndio yafuate

Wallahi nchi hii imeoza ikaoza kupindukia...eiiiiiish sometimez nadhani ni vizuri ukjifungia ndani kwako bila chombo chochote cha mawasiliano ili usijue wala kusikialolote linaloendelea nchi hii
 
mi najua kuungama wanafanya wakatoliki na hwa walokole huwa wanapayuka mbele za watu wao wanaita kushuhudia.....sasa huyu jamaa alienda kuungama au kushuhudia?!
 
Jamani hii picha ilisha ungua kitambo.Hakuna cha Mkenya wala Mnubi.Ulimboka kesha taja muhusika aliyemwona akichukua simu yake na wallet.Kona za nini?hivi angesema kwa kauli yake kuwa alimwona Lema na kachukua simu na wallet yake ingekuaje?pangechimbika na stori za Mkenya tusingesikia.
 
Huyo mchungaji wa bata, mchungaji gani huyoanatoboa siri za mungu wake

Umeona eeeh. Waumini watakimbia, na atakosa sadaka hivi hivi. Nani atakubali 'ushuhuda' wake uishie police?
 
Sielewi hii kitu,
Eti Mkenya mmoja mwenye uhusiano na genge moja la wahuni huko kwao alikodishwa kutekeleza huu mpango uliofanyika mwishoni wa mwezi wa sita, wiki mbili baadaye anajisalimisha katika kanisa fulani ili asamehewe..Ni kwanini hakwenda Polisi moja kwa moja badala yake apitie kanisa fulani?

Kama huyo jamaa ni "professional" kweli kama Kova anavyotaka tuamini asingeweza kukaa wiki mbili nzima Tanzania asubiri kwenda kanisani...Polisi tafuteni stori nyingine kwa kifupi..We don't buy it..
 
Mchungaji wa kweli anafahamu wajibu wake kama WAKILI wa SIRI za Mungu. Pia amri isemayo USILITAJE BURE JINA LA MUNGU WAKO. Je wakili akivujisha siri ahesabike vipi? Kna watesaji wengine wa taifa, mf. wezi, wala rushwa waliowahi kutubu? Nao wataanikwa lini hadharani? Kila wakili na awe mwangalifu kutoa taarifa apatazo kupitia kazi yake akijua kuna aliye juu yake wa kuhukumu, na ukweli una siku yake ya kudhihirika ili ujitenge na uongo. Mchungaji Jipime kisha chukua hatua za ujasiri kuhusu kutoa au kutotoa tamko hilo!!
 
Baada ya kufanya bidii za maksudi kutaka kujua sakata hili la shambulizi la Mwenyekiti Wa Jumuia ya Madaktari TZ, Dr. Steve Ulimboka pamoja Na madai yaliyotolewa Jana Na Kamanda Kova kwamba Kuna Mtu anaedaiwa kuhusika Na utekaji Na shambulizi Hilo aliyejitokeza kujisalimisha ndani ya Kanisa linaloongozwa Mch Josephat Gwajima, pamoja Na utata uliosambaa juu ya matamshi hayo, nimebahatika hatimae kuongea na Mchungaji huyo..

Yeye mwenyewe Kwanza amekiri kusikia taarifa hizo Na pia maelfu ya watu miongoni mwao ni washirika NOa watu wengine nje ya Kanisa nao wamekuwa wakimtafuta ili kupata ukweli Wa matamshi hayo ya Polisi

Mchungaji huyo ambaye Kwa mtazamo ni mpole, mkimya Na mwenye maneno yaliyonyooka, akasema kwamba kuna taarifa aliletewa Na walinzi wa Kanisa kwamba kuna kijana mdogo tu alikuwa akidai yeye ndiye Kinara wa sakata Hilo la kumteka daktari huyo..Na walinzi Hao wakampeleka kituoni Na kumkabidhi huko.. Sasa cha Ajabu ni taarifa ya Jana ya jeshi la polisi juu ya uhusika wa tukio Hili..

Na yeye Kama kiongozi imemgharimu kuwaita Upya wale walinzi Na kupata kutoka kwao taarifa hiyo Na hatimae kesho kwenye Ibaada maalum ataelezea Mkasa wote ulivyokuwa ili jamii ielewe nini kilichojiri..

Nimepitia comment nyingi za watu humu kila Mtu akinadi Na kusema lake, wapo wanaotukana Na wapo wanalalamika Kwa namna wajuao.. Labda nitoe rai kwamba ni vema tuwe Na subira Na kupata Picha kamili hiyo kesho..

Mimi mwenyewe nitawahi mapema Na Kama kawaida ya TAMKO nitawajuza kila kitu..matusi kejeli si mahali pake nadhani kuna kamchezo kanaendelea ambako lazima kafichuliwe sasa.. Jambo Hili si Dogo linagusa masikio ya mataifa mengi Kwa sasa..

..
Nilivyomsikia Ibaada inaanza mapema saa tatu hivi, ila mishale ya saa Tano yeye ndipo anapoanza kuongea, so kabla ya kuendelea Na mahubiri atafafanua kwanza utata huo, kisha baadae ataendelea Na mahubiri Kama kawaida.. Sasa Kama kuna waandishi wa Habari Na watu wengine baada ya fafanuzi lake wanaweza kuondoka, Sasa Muda wa Sadaka ni mwisho kabisa wa ibaada yote.. Sasa anayesema kwamba anaitwa Kwa Sadaka sidhani Kama atakuwa Na Busara hapa..

Mimi naona kuna mamluki wanataka kutibua Tusijue nini kiko nyuma ya Pazia..watanzania Wa Leo Tuko Na macho mingi

..

..

Nimepita hapo kanisani kwake, sijaona Kanisa wakulu, ni Uwanja tu mkubwa wazi wa kilichokuwa kiwanda cha nyama-Tanganyika Packers LTD, embu Tujuzane watu wanakaaje hapo.. Wakuu au kuna mahema wataweka AMA vipi, nimepita Na mkweche wangu hapo ni wazi tu .. Embu mdau anayeelewa atujuze zaidi..
 
Huyu mchungaji ana leta unafiki sasa, yani ana taka kujiosha tujue hahusiki, huo ndio uhuni amabao sikuutegemea kutoka kwake!

Kwanza ni mchungaji gani huyu anatoa sirii za waumini?
Ni majambazi wangapi walio uwa watu wamekwenda kwake na haku waita polisi.

Sasa ana take advantage kupata sadaka kwa kusema ataeleza kesho kilichoteokea, huu ni uwongo mtumpu ana taka kujaza waumini kesho na hakuna atakacho kieleza tofauti na kova.

Huu ni utoto wa mch ngwajima na kova.
 
Back
Top Bottom