Mchumba wa rafiki wa dada yangu ambaye pia ni rafiki wa mume wa dada yangu anamtaka dada!!

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
HABARI WANA JF
Naombeni ushauri kwa hili!
Nina dada yangu ana rafiki yake mpenzi wameshibana sana na kuaminiana kiasi kwamba amekua kama mwanafamilia mwenzetu au ndugu......
Kutokana na maelewano hayo hadi marafiki wa shemeji wanamfahamu kama ndugu na ikatokea rafiki wa shemeji(mume wa dada) akatokea kumpenda kupitia dada na wamekua na mahusiano zaidi ya mwaka sasa!

Cha kushangaza ni kwamba siku moja huyu rafiki yetu(rafiki wa dada) akiwa safarini na shemeji yangu nae akiwa safarini huyo mchumba alikuja nyumbani na kuanza kumtongoza dada! Dada alichukia sana akamchukia sana huyo mwanaume hadi leo anamchukia maana aliona kama ile ni dharau... Huyo mwanaume tangu siku hiyo baada ya kukataliwa ameona aibu hata nyumbani hafiki kabsaaaa....

Sasa ameamua anataka kumwoa yule rafiki wa dada na huyo rafiki anataka kumpa dada majukumu kwenye hilo ila dada hataki kabsaa maana ameshamchukia huyo bwana na anamuona tu kama laghai wa mapenzi maana hana hata adabu.
 
title ya hii thread inachanya kwel duh! cjui mchumba wa dada, mume wa dad etc duh! Km vip ungewataja kwa majina tu teh! Anyway kwenye mapenzi fanya maamuzi mwenyewe!
 
Sielewi kama ni stori unatupa?, ni swali unauliza?, ni ushauri unaomba? ama ...dah! kaaaazi kwelikweli
 
Sielewi kama ni stori unatupa?, ni swali unauliza?, ni ushauri unaomba? ama ...dah! kaaaazi kwelikweli
ushauri daughter
maana shughuli yenyewe bado wiki chache sasa dada hataki kwenda na hawezi kumwambia rafiki sababu
 
ungeweka majina hata ya kubuni tuelewe

maana haponaona rafiki wa dada,na rafiki wa dada..
sielewi kabisaaaa
 
Kwa hiyo cc ka wana jf ndo una2ambia ili 2ikanye hyo njemba icmtongoze huyo dada yako au,maana hujaeleweka kama umeuliza swali au ume2simulia hadith!
 
Ingawa umeichanganya changanya story yenyewe nadhani tatizo hapa ni lile lile la kuchagua marafiki viwembe/viruka njia. Soma ile mada ya dada aliyetongozwa na rafiki wa mume wake utakuta kuna ushauri mzuri sana umetolewa na wadau.
 
Kwa hiyo cc ka wana jf ndo una2ambia ili 2ikanye hyo njemba icmtongoze huyo dada yako au,maana hujaeleweka kama umeuliza swali au ume2simulia hadith!
Hii hadithi inachanganya kinyama! Mimi mwenyewe toka mwanza nishaliona hilo!
 
Back
Top Bottom