Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Alafu baada ya kufa Baba J ndio mwimbaji akawa dogo jack simela,au huyu dogo jack simela alikuwepo kitambo?
 
Mimi bhana naomba kujua hawa waliokuwa wanatajwa kwenye nyimbo za jagwa walikuwa na cheo gani kwenye bend,
1.Kamongo Manja(Manjalino)
2.Jolijo
3.Saidi Misape
4.Bonge mzito
4.Baba Dullah

1. Manjarino ni mdau mkubwa wa Jagwa
2.Jolijo ndio mkurugenzi wa Jagwa
3. Bonge Mzito ambae kwa sasa ni marehemu alikuwa shabiki mkubwa wa Jagwa ila alikuwa mwizi hatari miaka hiyo maeneo ya Mwananyamala, Tandale na Manzese
4. Baba Dullah nae ni mdau wa Jagwa.
 
Ok!ahsante sana kwa kunifahamisha,maana mi nilijua ni majina wale wapiga vyombo,unaweza kunitajia majina ya wapiga vyombo?
 
Alafu baada ya kufa Baba J ndio mwimbaji akawa dogo jack simela,au huyu dogo jack simela alikuwepo kitambo?
Hapana, kwanza Baba J hakufariki akiwa uraiani alipelekwa mahabusu ambapo huko ndio umauti ulimkuta. Kwa hiyo baada ya Baba J kupelekwa Jera akaja muimbaji mwingine jina kidogo limenitoka ila kama unaujua wimbo wa Kondacta wa Chaukucha yule muimbaji ndio aliechukua nafasi ya Baba J.
Baada ya huyo jamaa kwenda Chaukucha ndio dogo Jack akachukuliwa kutoka Morogoro kuja Dar kujiunga na Jagwa Music.
 
Ahsante sana kiongozi kwa darasa unalonipa,basi ndio maana kuna wimbo ameimba dogo jack unaitwa maisha popote,kumbe katokea morogoro kuja dar
 
Naskia kuna wanamuziki wa mnanda vibaka ambao walikuwa wanalala barabarani magari yakisimama wanayapora siku hiyo huko Kibada Kigamboni dereva alisimamishwa lakini hakusimama akawagonga wote wakafa,jamaa akawaimbia huo wimbo wa Ajali ya Kibada

Wengi wao si wote walikuwa kwapukwapu yaani mnanda na uporaji kama uji na mgonjwa wengi wanakuwa watu wa maskani hawana kipato cha kueleweka so wanaongeza kipato kwa kukaba na kupora watu.
 
1. Manjarino ni mdau mkubwa wa Jagwa
2.Jolijo ndio mkurugenzi wa Jagwa
3. Bonge Mzito ambae kwa sasa ni marehemu alikuwa shabiki mkubwa wa Jagwa ila alikuwa mwizi hatari miaka hiyo maeneo ya Mwananyamala, Tandale na Manzese
4. Baba Dullah nae ni mdau wa Jagwa.
Jolijo sifa nyingine kwa mwananyamala kisiwani ni mpishi maarufu wa pilau kwenye shughuli za kijamii
 
Ningependa kuja ilipo bendi moja ya mchiriku ambayo ili-modernize muziki wa mchiriku (kwa kuweka vinanda na magitaa)mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambayo iliitwa Hisani Musical Club ambyo ilitoa album yao moja iliyotamba sana miaka hiyo.

Nakumbuka kipindi hiko nikiwa mdogo nikipita Kariakoo ilikuwa vibanda vya wauza kaseti nyimbo zake zilipigwa sana mfano "uko wapi" Ally Mwinyi Hodari" "mola wangu nk. Mdau mwenye kujua taarifa zao na ikiwezekana kuwa na nyimbo zao azitupie hapa ili tukumbuke.
Interview ya gari kubwa.
Kumbe hiyo Albam iliyotamba jamaa walilipwa 80,000/- Tu
 
Mimi niko mbioni kufanya hivyo,kwani nina historia iliyoshiba ya mziki huu na nawajua watu wengi waliokua ni wadau wakubwa ambao wanaweza kunirekebisha nikoseapo.Halafu naupenda mziki huu.
Kama hutojali kuna what group la Mchiriku humo kuna wakongwe na wadau wanaoujua historia za muziki huu na wasanii wa sasa pia wapo humo. Kwa vile unataka kuandaa Documentary nakushauri ujiunge huko uchukue baadhi ya "madini" ambayo yatakusaidia kwenye Documentary yako. Ukitaka kujiunga nitumie namba yako ya WhatsApp PM.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom