Mchina original

Mbava

Member
May 18, 2011
30
1
Vp wana JF, Naombeni mnielimishe katika hili, nimekuwa nikienda dukani kutafuta simu flani eg Nokia 5800 music express nikaambia tuna simu ya mchina original! Nisaidieni hivi kweli kuna simu ya nokia ya mchina original? Nisaidieni kwa wanaofahamu nishaurini ninunue au la?
 
Majority ya Nokia zinatengenezwa China, so yes ni original from China.
 
china original ndio nini wazee.
ni za kufyetua tu hizo. na mara nyingi zina leta usumbufu katika charging system baada ya muda mchache tu wa matumizi.
sishauri nokia origina from china.
ila kuna simu za kichina original ambazo hawajaiga mashirika makubwa kama vile TECNO au ITel. hizi ni simu madhubuti au ngumu tuseme
 
Simu zote za nokia bila kujali zinatengenezwa nchi gani ni original kwa ubora uleule iwapo tu zitatengenezwa na kiwanda halali cha nokia, hivyo zipo nokia original from china.
sema sasa kuna nokia fake zinazotengenezwa mtaani huko china na wajanja, kuzijua inahitaji utalaamu kidogo.
Cheki kunapost ya juzi juzi ilikuwa inaelezea haya mambo
NB si kila kinacho tengenezwa china ni fake, tatizo ni nchi hii haisimamii sheria ya ubora hivyo wafanyabiashara wetu wakifika china wanaulizwa unataka simu ya bei gani? simu aina moja unakuta kuna ya dola 10, dola 20, dola 50,dola 100 nk
So utakavyoshuka bei ndio unapata famba utakapo panda bei unapata kitu makini (hii ni kwa bidhaa zao)
 
Back
Top Bottom