SULEIMAN ABEID
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 390
- 385
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiingia mikataba mingi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii na kwa bahati mbaya sana mikataba hii hutuzwa kwa siri kubwa, wabunge na wananchi wamekuwa wakilalamikia utekelezaji dhaifu wa baadhi ya mikataba bila kupata majibu fasaha.
Lakini pia taarifa za PPRA, CAG na PCCB zimekuwa zikionyesha wizi na ufisadi mkubwa katika utekelezaji wa baadhi ya mikataba. Mheshimiwa Spika, Usiri uliowekwa kwenye mikataba iliyoingiwa na Serikali kwa niaba ya wananchi umewekwa kwa ajili ya kumlinda nani? Na hii ni kinyume cha Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, Ipo mifano mingi lakini naomba nitoe mfano wa Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, zimekuwa zikitolewa taarifa za ucheleweshaji wa mradi huu na kumekuwepo na taarifa za 8 kuongezewa muda wa mkataba kwa mkandarasi kwa miaka miwili zaidi, badala ya mradi kukamilika Juni 14, 2022 sasa utakamilika mwaka 2024, suala hili ni la kisheria na kimkataba, usiri unaowekwa na Serikali katika mradi huu unazua maswali mengi sana ya kujiuliza:-
Mheshimiwa Spika, Mkandarasi anapaswa kulipa CSR ya 4% ya thamani ya mradi na kwa mantiki hiyo, pamoja na mambo mengine Watanzania walitarajia kuelezwa bayana yafuatayo:-
Mheshimiwa Spika, Leo tunaambiwa mkandarasi anaongezewa muda wa miaka miwili zaidi, lakini hakuna maelezo yoyote, mradi unaongezewa muda kwa gharama za nani, vigezo na masharti yaliyomo katika mkataba yameathiriwa vipi na ongezeko hili la muda (variations).
Mheshimiwa Spika, Usiri huu unaleta hofu na mashaka makubwa kuhusu kukamilika kwa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, kuna wasiwasi wa kupotea fedha za CSR jumla ya Tsh Bilioni 260, pia inaonekana mkandarasi anabebwa ili asilipe faini ya ucheleweshaji kiasi cha Tsh. Trilioni 1.3.

- Ni lini Serikali ilifanya tathmini ya kina kuhusu utekelezaji wa mradi huu na Bunge limeshirikishwa kwa kiwango gani kuhusu tathmini hiyo?
- (ii) Ni nani amesababisha ucheleweshaji wa mradi na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake?
- Mradi unaongezewa muda wa utekelezaji kwa gharama za nani na hayo majadiliano yamefanywa lini na yamefanywa na nani?
Mheshimiwa Spika, Mkandarasi anapaswa kulipa CSR ya 4% ya thamani ya mradi na kwa mantiki hiyo, pamoja na mambo mengine Watanzania walitarajia kuelezwa bayana yafuatayo:-
- Haki yao ya kisheria na kimkataba kufuatia ucheleweshaji huo, Mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors ya Misri amechelewesha mradi kwa miaka miwili, kimyume cha mkataba na kwamba anahusika na faini ya 10% na hivyo kwa ucheleweshaji wa miaka 9 miwili anapaswa kulipa faini ya Tsh. Trilioni 1.3. Kwa nini hili suala halizungumzwi na haliwekwi wazi kwa watanzania? Mheshimiwa Spika, Kamati za Bunge zilishaeleza katika vikao vya kamati na ndani ya Bunge lako Tukufu kuwa sababu kubwa za ucheleweshaji ni za mkandarasi mwenyewe na ushahidi wa ‘hansard’ za Bunge upo.
- Pia tunafahamu kwa mujibu wa Mkataba, Mkandarasi anapaswa kulipa 4% ya Mkataba kama CSR ambayo ni jumla ya Tsh Bilioni 260, licha ya mkandarasi hadi sasa kulipwa 57% ya mkataba na kwamba amekuwa akilipwa kwa wakati lakini hajalipa hata senti moja ya CSR.