Mchango wa ERB na CRB

Tangawizi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,173
3,896


Kama zilivyo nchi nyingine zinazoendelea, Tanzania inahitaji sana mchango wa wahandisi na makandarasi ili kiu ya maendeleo ya kweli, ipatikane sambamba na ujenzi wa miundo mbinu kwa wananchi wake walio katika kona mbalimbali za nchi yetu.

Ili kukidhi ubora wa huduma zinazotolewa, serikali ilianzisha bodi ya wahandisi(ERB) na ile ya wakandarasi(CRB).

Kinachonitatiza mimi ni kuwa mchango wa bodi hizi umekuwa hafifu ama hauonekani kabisa kwa maana ya kuchukua nafasi ya mbele katika kushauri, kuelimisha, kukuza viwango vya kimataifa na hata kuonyesha njia pale ambapo inabidi, kutokana na kazi wanazozifanya.

Kuna mifano mingi ambayo inanifanya nione vyombo hivi vya udhibiti, vimechukua role ya mwalimu mkuu zaidi, nikiwa na maana kazi pekee wanayoiona ndiyo mahususi kwao ni kuandikisha wahandisi na makandarasi, kuandaa annual meetings, na vitu vingine ambavyo wanavifanya on routine basis, year in year out. Ningeweza kufurahi kama wangeweza pia kuwa na kazi zenye kutoa majawabu ya matatizo mbalimbali yanayohitaji input zao.Kwa mfano,

1. Miji mingi Tanzania inaendelea kujengwa bila kufuata utaratibu na hivyo kuifanya kukosa miundo mbinu ya msingi kama umeme, system nzuri za maji safi na taka, barabara zisizo na mipangilio ambazo zinachangia kuongeza foleni na kadhalika
2. Kukosa input zao kwenye uendeshwaji wa viwanda vikubwa kama vile vya madini, ambavyo vina mchango mkubwa katika pato la Taifa na kuajiri maelfu ya watanzania.Migodi mingi bado inajitangaza kuoperate kwa hasara na bodi hizi kama chachu ya utalaamu wa maeneo hayo vimekaa mbali na kuona kana kwamba suala la tija si sehemu yao. Mimi nionanvyo, kwa kutumia utaalamu wa watu wengi wa fani za uhandisi, wangaliweza kuwa sehemu ya ushauri na kutafuta ukweli wa yale ambayo wawekezaji wanayaeleza.Kwa sasa hakuna anayeweza kujua ukweli wa migodi kufanya kazi kwa hasara na sababu zinazochangia
3. Ukiangalia leo mji kama Dar es salama, pamija na foleni zisizo kwisha, junction ya ubungo imekuwa kero kubwa.Engineers wako wapi kutupa solutions? Badala yake solutions zinatolewa na wanasiasa. Nilifikiri ingeliwezekana kuwa na session among these professionals ambazo zinayaangalia matatizo ya jumla ya kihandisi na nini ushauri wao bila kujari nini wanasiasa wataamua. Ilivyo sasa hakuna ushauri kama huo na pale tatizo linapokuwa sugu, basi namna pekee ya kujikwamua ni kufanya kisiasa zaidi na zaidi.
4. Wenzetu wengi, ikiwemo South Africa, wamo ama kwenye Washington accord au namna nyingine ya ushirikiano ili kuwezesha ubadilishanaji wa maarifa, technologia na ujuzi. Sisi tumesimama katika kisiwa, tunaona pengine hilo pia halituhusu. Tunawezaje kupata utaalamu wa kufanya mambo makubwa kama tumekaa pembeni kama watazamaji? Ina maana project zote kubwa itabidi zifanywe na makampuni ya nje tu hata kama funding zake ni local? Naamini pia bodi hizi zinasuasua kwa hili

Mifano ipo mingi tu ya ulegelege wa bodi zetu hizi. Nia yangu si kuzibeza, bali kuzipa changamoto na kuwaomba kuwa proactive zaidi ili mambo yanayohitaji utaalamu wao, wawe na uwezo wa kutoa michango zaidi. Siamini kazi pekee wanayostahili kufanya ni kusajiri tu..kama ndivyo basi tumepotea njia!!
Inasikitisha kusikia kwamba procurement ya capital equipment na capital projects ndo zinazoongoza kupoteza hela nyingi katika manunuzi ndani ya Taifa. Bodi hizi mnatoa mchango gani kuboresha mambo ili kudhibiti vitu kama rada, ukodishaji wa ndege, ununuzi wa ndege zilizo chini ya kiwango etc? Kazi kwenu maana bado naamini mchango wenu unahitajika ila mipangilio ya sasa hainishawishi kutegemea mchango kama huo.

Pengine niombe elimu zaidi ya kwanini siwaoni kama mchango wao upo wazi kwetu.
 
Back
Top Bottom