Mchakato wa kutafuta jina mbadala la Tanganyika !

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Naomba wana Jf mpendekeze nchi yetu iitwe jina gani, Mungano uko ukingoni kuvunjika, jina la Tanganyika doesnt

sound good na jina la Tanzania limepatikana kutokana na Muungano.

(Tanga means kutanga tanga, Nyika means Mwitu =>Tanganyika= kutanga tanga mwituni, Mtanganyika=mtu wa kutanga tanga

mwituni) Mimi ningependa jina la nchi yetu iitwe Tafania. Bora niitwe Mtafania kuliko Mtanganyika, Je wewe unapendekeza jina gani?
 
Jina siyo tatizo, kipaumbelekwa sasa ni kuelekeza nguvu zetu zoooooooooooote kuuvunja huu muungano, tuwaunge mkono uamsho ili hii biashara iafanyike mapema kabla ya 2015.
 
ivi tanganyika ipo me nasikiaga tu
  1. Tanganyika law society(TLS)
  2. medical association of tanganyika (MAT)
  3. viwanja vya Tanganyika Packers
  4. lake tanganyika
  5. international school of Tanganyika
  6. tanganyika arms
  7. lake tanganyika hotel.
 
ivi tanganyika ipo me nasikiaga tu
  1. Tanganyika law society(TLS)
  2. medical association of tanganyika (MAT)
  3. viwanja vya Tanganyika Packers
  4. lake tanganyika
  5. international school of Tanganyika
  6. tanganyika arms
  7. lake tanganyika hotel.


mkuu kama umeshawahi kwenda Tanga kuna daraja la safina( nafkiri jina limebadilika) ukiwa unaingia jiji la tanga kuna kibao kikubwa cheupe chenye maandish meusi kinachosomeka TANGANYIKA sasa mimi mpaka leo sijapataga mtu akanielezea vizuri kwanini pale kwenye ule msitu ndipo pamewekwa hiki kibao.
 
Bora iitwe tafadhani na mie niitwe mtafadhali.

Hii inatokana na kiongozi wetu kila siku kwenda kusema 'tafadhali. . . ' wakati wa kuomba misaada.
 
Tafania maana yake nini? Isije ikawa nchi ya maboflo halafu tukakubali jina bila kuulizia Boflo
Ndahani Tafania inatokana na neno tafunwa......Hata na wewe unaweza kupendekeza jina la nchi yetu, sio lazima
kufata mawazo yangu
 
Last edited by a moderator:
Boflo vipi mkuu! ... kwi! kwi! kwi! ... naona unaanza kuangalia maboya yako wapi ili meli itakapozama uwe tayari umeshayavaa!! ..

Usiwe na wasiwasi wa kuanza kutafuta jina mbadala la Tanganyika ... kwa Tanzania hii na viongozi wetu jinsi wanavyoogopana ... sioni kiongozi mwenye ubavu wa kuamka asubuhi na kusema kuanzia leo tunavunja muungano! ... hakuna mwenye ujasiri huo! ... wanapiga kelele tu! ...

Usiwe na wasiwasi ... meli ndio kwanza inazidisha mwendo! ... usikimbile boya ... bado muda wake .... usijali ni upepo tu (dhoruba tu) ... utapita!
 
Ibaki kuwa Tanzania. sababu ni moja tu kuwa ni jina lililotokana na matakwa yetu wenyewe na si la kubambikiwa na wakubwa. Litumike hata km wapemba na waunguja wakijitoa ktk muungano kama jina CRDB linavyotumika hivi sasa. CRDB kwa asili yake lilimaanisha Cooperative na Rural Development Bank ( benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini, lakini hata baada ya kuachana na sera na malengo yake ya asili benki hiyo imeendelea kutumia jina hilo bila kasoro.
 
Back
Top Bottom