lukindo
JF-Expert Member
- Mar 20, 2010
- 8,466
- 9,028
Nawasalimuni
Ni wazi kuwa hakuna hata Mtanzania mmoja anayekubali na atakayekubali kuwa mali wanazomiliki Chama Cha Mapinduzi - CCM ni halali yao. Hii ni kwa hata CCM wenyewe pale wanapotakiwa kueleza ukweli juu ya mali hizo.
Kwa kifupi ni kuwa mali nyingi kama sio zote zilipatikana kwa nguvu ya wananchi (umma), na kwa vile kulikuwa hakuna vyama vingi hata mtu asie na chama ilimpasa kuchangia na hii inaeleweka kwa kila mmoja wetu. (Mwenye mawazo tofauti katika hili tunaomba atufafanulie)
Jinsi gani ziliangukia mikononi mwa chama?
Kwa vile mali nyingi zilipaswa kusimamiwa kama tunavyofahamu na halmashauri, manispaa au jiji na hizi taasisi zilitumika kuwakilisha wananchi maana serikari isingweweza kusimamia moja kwa moja. Hivyo ilikuwa ni sawa kupitia taasisi hizi kuwa wasimamizi wa mali husika kwa niaba ya wananchi.
Kwanini zirudishwe kwa wananchi sasa?
Tumeshuhudia kwa miaka ya karibuni kuwa umeingia mgawanyiko na ubinafsi wa hali ya juu katika chama hiki kikongwe ambao unahatarisha usalama wa mali hizi za wananchi (sio za CCM kumbuka). Mfano wa karibuni ni jengo la makao makuu ya Umoja wa Vijana ambapo sasa litamilikiwa na watu wachache katika mkataba tata kama CCM wenyewe walivyoainisha. Huu ni mfano mmoja kati ya mamia ya jinsi tunavyokaribia kupoteza urithi wa nchi waziwazi.
Ili kunusuru mali hizi tuanze na viwanja kama KIRUMBA wa Mwanza na SHEIKH ABEID wa Arusha virejeshwa kwa Harmashauri husika ili waviendeleze. (Nasema hizi sehemu mbili kama sample tu). Hilo ni pendekezo la jinsi ya umiliki wa mali hizi unavyoweza kuwa, yaani chini ya Halmashauri husika. Ikiangukia CCM, CUF, NCCR, TLP, CDM nk ndiyo wawe na jukumu la usimamizi kwa 'sense' ya uwakilihi wa wananchi. Pia tunaweza kupitia report ya Jaji Nyalali ili kuwa na uhakika wa jinsi walivyoliona ili suala.
Tahadhali:
Kuchelewa kuchukua hatua kunaweza kupotezea taifa vitu vya msingi na thamani, wananchi wake pamoja na vizazi vijavyo. Sidhani kama anaweza kusimama mtu sasa hivi ndani ya CCM na kutuhakikishia (katika hali ya uungwana, uzalendo na ukweli) usalama wa mali hizi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI DUNIA
Nawakilisha