Mchakato wa kumwondolea Mkapa Mafao ya Rais mstaafu

Hii siyo issue ya chama, ni suala la sisi wenye nchi kuangalia namna gani kodi zetu zinatumika. Hatuwezi kuwalipia watu kama hawa wanaoenda majukwaani kutukana na kutetea uongozi mbovu. Ifike mahali tuangalie ukweli. Rais mstaafu angefaa kuwa mshauri na siyo chanzo cha kibri na kebehi ambazo hazina mpango, hasa kwa wananchi wanaohoji mambo halali. Tuache utani katika hili!!


Mwizi hastaafu, hivyo ndo changamoto ya sasa kwa TZ, kila mara anahisi ataumbuka iwapo timu yake itamomonyoka, inabidi ajaribu kila awezalo. huku kujaribu lolote na chochote ndo matokeo yake wanaongea pumba za kufa mtu, ni kujaribu kulinda maslahi yao ndo kunawaponza. Mwizi hastaafu!!!!
 
Naomba katiba mpya tuliangalie hili kwa mapana yake,kwa ukweli inachanganya kwa namna yake.Kwani mstaafu ni wa wote si wa ccm peke yao.
 
This is a point to NOTE kwenye katiba mpya. Kwenye katiba mpya itajwe EXPLICITY kwamba viongozi wa KITAIFA wastaafu watakaondelea kulipwa mafao kwa kodi zetu ni wale tu ambao hawako kwenye ACTIVE POLITICS. Kama kiongozi wa kitafia atakuwa kwenye active politics kama Mkapa, Msekwa, Sitta, Lowassa, Mboma (aliogombea ubunge), Dr. Shein (former VP)basi watakosa sifa ya kuendelea kutuzwa kwa kodi zetu.
 
Naunga mkono hoja, hawawezi kufanya kazi ya chama na kulipwa na serikali! walipwe na chama chao. kwa sababu wamegoma kujua kuwa walifika hatua ya juu ya kuwa watu wa Watanzania wote na kuamua kutumikia kachama kao basi walipwe na chama chao!
 
Wakuu,
Mkapa kama Rais mstaafu anaishi kwa kodi zetu sisi 'sons and daughters of the soil' bila kujali tunatoka chama gani. Wakati tukitegemea yeye kuwa mshauri wa masuala yanayohusu mustakabali wa kuendesha nchi, yeye anajikita kwenye kudharau wale wote wanaohoji mambo halali juu ya namna hii nchi inavyoendeshwa. Mafao ya viongozi wakuu wastaafu naona yanatumika vibaya. Kwa kuwa Mkapa bado yuko kwenye 'active politics' tena za kutetea uovu, ni wakati mwafaka tuanzishe mchakato wa kisheria wa kumwondolea mafao, kwani anaweza akalipwa kwenye siasa za CCM.

Mwongozo tafadhali...

Mkapa anajua kuwa wapinzani wakichukua nchi itakuwa kiama kwake. Ona mzee Mwinyi hana wasiwasi, Komandoo Salmin kule Zenji Karume hawana mhehemko. BWM ana mhehemko kwa kuwa anajua alichofanya akiwa madarakani, ufisadi wa kutupwa aliofanya bila aibu yeye na Anna Mkapa na ndugu zao, mauaji ya Zanzibar, kifo cha mwalimu kama alivyosema Vincent Nyerere etc. So he has more to loose kama CDM wakichukua nchi.

CCM wanajua hilo na ndio maana wanamtuma kwa kuwa wanajua hawezi kukataa! Angekuwa amefanya mema, sidhani kama angekuwa anajishughulisha na politics za TZ,angekuwa anatumika huko nje kidiplomasia
 
Kwa hakika suala hili ni lazima liangaliwe na kuchukuliwa hatua za haraka. Iwe ni moja ya kero ambazo Wabunge wa Chadema na Chadema kama Chama makini wanapaswa kulijadili kwa kina na kuona jinsi ya kulipatia ufumbuzi. Wana JF mtakumbuka jinsi mkapa alivyowapa CCM kiburi katika uchaguzi mkuu 2010 wakati wa kufunga kampeni pale jangwani alipowaita wapinzani kuwa ni sawa na "kokoto" hivyo hawana haki ya kuchaguliwa! Aina hii ya maneno ya kejeli hayakubaliki yatolewe na mtu analipwa mafao kwa kodi zetu sote. Ni lazima wapigwe STOP! NA WAKATI NI HUU.
 
Jamani tuwaache wazee wetu wapumzike, tusifanye mambo kwa visasi hatutafika mbali 2takuwa tunatafutana wenyewe kwa wentewe huku maendeleo yanadoda
 
kwenye suala la malipo ya viongozi wastaafu ni bora kabisa kuwaiga majirani zetu wa Malawi wanasheria nzuri kabisa kwamba kiongozi atalipwa mafao na serikali kama hatakuwa anajishughulisha na mambo ya kisiasa. Nimeipenda sana hiyo. Mstaafu kiongozi anatakiwa atulie ale nchi na awe anatoa ushauri kwenye Serikali basi . kuna hili suala lingine kumhusu waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, inakuwaje Serikalini anatambulika kama Waziri Mkuu Mstaafu mi kwangu mbona haiingii akilini, hivi ni kweli anastahili sifa hiyo?
 
Naunga mkono hoja. Ingawa sina ufahamu zaidi kisera za kichama na serikali (mfano USA) maana kipindi Obama anagombea Clinton alimpigia kampeni. Sema kinacholeta shida CCM ni genge la majambazi, wamepola rasilimali za nchi na bado ni waongo wa kutupwa!
 
Jamani tuwaache wazee wetu wapumzike, tusifanye mambo kwa visasi hatutafika mbali 2takuwa tunatafutana wenyewe kwa wentewe huku maendeleo yanadoda
..umesema vyema 'kupumzika',huko ni pamoja na kutofanya matendo yanayohamasisha makundi mengine katika jamii au tuseme wanyonge kutotendewa haki, kuhamasisha wizi na kuitetea serikali ambayo kila mtu anaona kuwa inachofanya sio sahihi, lakini kwa kuwa na yeye anatafuta ulinzi wa serikali hiyo anajiingiza kuitetea. Mtu kama huyo hastahili kula jasho letu, mdomo wake umsaidie kula.
 
Back
Top Bottom