Elections 2010 Mchagueni Slaa: (mashairi)

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Nimelala nimekesha, jambo nimefikira
Bongo nimezichemsha, sipati jibu sawia
Hivi kweli Umekwisha Uzalendo Tanzania?
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Ona walivyoziuza, rasilimali za mtanzania
Kwa kweli inashangaza, mikataba waloingia
Kisha tukiwauliza, hawana la kutwambia
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Rushwa imekuwa ngao, kumdhulumu raia
Ubinafsi kwao nguo, vazi la kujivunia
Hizi ndizo sera zao, katu hawajui njia
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Wananchi amkeni, haki kujitafutia
Mtalala mpaka lini?, saa imeishawadia
Uwongo ukataeni Waache kuwatania
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Mkipiga kura zenu, chagueni mwenye nia
Waonesheni wanenu, muelekeo na njia
Fanyeni vitu vyenu, tuiokoe Tanzania.
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Mchagueni Slaa, kiboko cha Mafisadi
Huyu bwana hana njaa, atatwanga wakaidi
Ni kiongozi shujaa, si mtumwa wa itikadi
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
 
kaburunye naitika, wito uliotolewa
kwa kweli gamba la nyoka, hoja nimeielewa
ona tulivyopigika, kama vile tumelewa
CCM baibai, CHADEMA shikeni nchi

hawa uchungu hawana, matumbo mbele waweka
utajiri wagawana, wao kwa wao hakika
hawana hata uungwana, ukisema wanawaka
CCM baibai, CHADEMA chukua nchi

vilago tuwatupieni, sisiemu mafisadi
walichofanya ni nini, kila siku ni ahadi
kutudanganya acheni, ama kweli wamezidi
CCM baibai, CHADEMA chukua nchi
 
Umetimia wakati, joka kuliondosha
Tupaze zetu sauti, jitu hili kulifisha
Yake haki ni mauti, ulimwengu kuujulisha,
Oktoba imefika, joka hili liuliwe

Kazize kuchakachua , uchumi umetitia
Dhahabu limechukua, mafisadi kuwapatia
Mashimo kutuachia, eti uchumi umekua!
Oktoba imefika, joka hili liuliwe

Mali yote ya umma, lenyewe limekalia
Eti mali yake mama, wakati ya familia!,
Umma sasa kusimama ,mali ni kwa familia
Oktoba imefika, joka hili liuliwe

Kuliua tuwe makini, lisije kutukimbia
Kwanza taimu kichwani, halafu ndiyo mkia
Kura zetu kwa makini, na hilo ndiyo jambia
Oktoba imefika, joka hili liuliwe
 
HAZITAKI KURA ZENU

Hazitaki amesema, kwa hakika hazitaki,
Mbona mna muandama, kwa kisa kile na hiki,
Kikwete mtu mzima, na wala msihamaki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Pendo kitu cha hiari, hakina lazima katu,
Ni vema kujihadhari, msizidi kuthubutu,
Si kwa kero nazo shari, mumwache mwana wa watu,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mapenzi kweli maua, huweza ota popote,
Bali huhitaji nia, kuyahudumia yote,
Bila maji kumwagia, Hunyauka kwa vyovyote,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Wafanyakazi hataki, mwataka nini zaidi?
Msitumie mikiki, hali mu watu weledi,
Binadamu ana haki, kupima na kukaidi,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mbona hamna simile, huria kumuachia,
Mmeng'ang'ana na lile, hamtaki kusikia,
M-bembeleze milele, hataki kawaambia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mmejawa na hiana, kwa jibu alilotoa,
Kawaeleza bayana, wazi amewaambia,
Mwalitafuta laana, msilolitarajia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Kwa uvumba na ubani, kesha sema hazitaki,
Zaidi mwataka nini, awaeleze rafiki?
Tulia mkae chini, muwaze na kuhakiki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Hazitaki kakataa, kura zenu kasusia,
Japo mlete gitaa, na nyimbo kumuimbia,
Mumtembeze mitaa, kwa manoti mia mia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Hazitaki si ajabu, kura zisizo na soko,
Msiitafute tabu, kujipendekeza mwiko,
Bure mwajipa aibu, kwa kumpa mialiko,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.


Kaditamati shairi, kura zenu hazitaki,
Kila kitu ni hiari, shuruti haina haki,
Kuchagua ni fahari, lazima haipendeki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.
 
na mimi ngoja nijaribu...................

mlosema nimanani, WanaJF zingatia...
Tanzania mnadani, fisadi kuwapatia...
kura zetu ni thamani, usije kuwaachia...
Dr. Slaa mpeni, fisadi kuwaondoa...

Heshima Gamba la Nyoka, kuamsha yetu jadi
shairi yalotukuka, ujumbe umeunadi
Kaburunye yakamfika, kunena ikawa budi
Dr. Slaa mpeni, fisadi kuwaondoa...

Jibaba Bonge si nyuma, wake pia ni wosia
rasilimali umma, busara kuzikomboa
vita siyo lelemama, fisadi kuwatimua
Dr Slaa kasimama, fisadi kuwaondoa...

mpeni yenu dhamana, Dr Slaa Mchagueni
yu tayari kupambana, kuyaokoa madini
Urithi wa wetu wana, ulopokwa na shetani
Dr Slaa kasimama, fisadi kuwaondoa...

Kura zetu kazikana, Kikwete simtamani
Dawa ya Mjinga Kaona, JF kawaambieni
Katueleza bayana, ni vyema sikizaneni
Dr. Slaa wetu mwana, fisadi chonjo kaeni...

CCM si chama chetu, cha familia sikia
tuwambiaje wanetu, ni aibu simulia
baba wa taifa letu, aliko ahurumia
Imepotea thamani, aloacha kushikia

....duuuhhh kumbe kazi ngumu hii.............
 
simtaki ye kikwete,
ni kwa yake hali tete,
ilodhoofu ka mkate,
a hanifai kikwete.

uwezo wake dhaifu,
na hali yake ni mfu,
ni mtu wa majisifu,
na kujifanya nadhifu.

Slaa ndiye pekee,
tumaini jiwekee,
tena mtu wa pekee,
mwenye sifa za pekee.

ni hakuna kama yeye,
maishani atufaaye,
kura na tumpatiye,
atufae baadaye.

tuwaache mafisadi,
wale wote mahasidi,
wezi wa makusudi,
tuwazamishe zaidi
 
Waungwana mmenena
Maneno yenye maana
Kweli inauma sana
Yanotokea Tanzania

Watu wengi wanong'ona
Hali ni ngumu sana
Eti wao hawajaona
Jinsi tunavyoumia

Wao wanenepeana
Sisi tunakondeana
Vitu bei ghali sana
Hatumudu kununua

Kazi ni kwa kujuana
Tenda ni kwa kupeana
Rushwa si ajabu sana
Hawazijali sheria

Slaa hana hiyana
Kwa haki atapambana
Ni mtu makini sana
Kura yafaa kumpigia
 
Waungwana mmenena
Maneno yenye maana
Kweli inauma sana
Yanotokea Tanzania

Watu wengi wanong'ona
Hali ni ngumu sana
Eti wao hawajaona
Jinsi tunavyoumia

Wao wanenepeana
Sisi tunakondeana
Vitu bei ghali sana
Hatumudu kununua

Kazi ni kwa kujuana
Tenda ni kwa kupeana
Rushwa si ajabu sana
Hawazijali sheria

Slaa hana hiyana
Kwa haki atapambana
Ni mtu makini sana
Kura yafaa kumpigia

Ukifika na Songea, endelea Nachingwea,
Lindi ni Watanzania, usiache kupitia,
Usichoke kuongea, hakika watasikia,
Ni kipindi cha CHADEMA, sote tuifagilie.
 
Tumempata mwanana, mpambanaji hodari
Mzalendo pia mwana , mafisadi kukabiri
Utani kwake hakuna, kweli yeye dakitari
Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

Tumpe kura kwa wingi, uchumi kuukomboa
Tumpeni nyingi kingi, nchi kuisimamia,
Avuke vyote vigingi, mtandao kuubomoa
Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

Siku ile ikifika , kura tumpe Slaa
Yeye ndiye msifika , mafisadi kwao balaa
Wezi watetemeka, walisikiapo ‘Slaa'
Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

Anahaha makamba , kama anakata kamba
Mafuriko yamkumba, anenayo yote pumba
Chama chake kinayumba, sasa kutumia ndumba
Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa

Pipozi pawa ni sasa, kona zote yasikika
Ukombozi ndiyo sasa, ccm kuizika
Nchi yetu kutakasa, wakati ndo umefika
Siku ile ikifika, Kura zetu kwa Slaa
 
kikwete kweli hafai, kupewa tano nyingine,
yamfaa kapumzike, bagamoyo akasome
umaskini tanzania, akajifunze vidudu
raisi gani jamanini, hakui umaskini.

Wandugu nimejaribu beti moja next time yatakuwa mawili. Ndondondo si nchururu
 
kikwete kweli hafai, kupewa tano nyingine,
yamfaa kapumzike, bagamoyo akasome
umaskini tanzania, akajifunze vidudu
raisi gani jamanini, hakui umaskini.

Wandugu nimejaribu beti moja next time yatakuwa mawili. Ndondondo si nchururu
akajiunge na yahya,
asiye kuwa na haya,
wakabashiri ubaya,
kwa zao tabia mbaya.

anaabudu mizimu,
kikwete sinaye hamu,
sije peleka kuzimu,
ambako si muhimu.
 
kwa uongozi imara na wa haki,chadema hakika mwaweza,
si kwa vijana wala kwa wazee,pote mnakubalika,
mafisadi hawana nafasi,na hatamu hawawezi pata
dhamana iliyobaki kwa mtanzania,ni chadema iliyo imara


tumechoshwa na unyonyaji,unyanyasaji usio kifani,
vilio vya watanzania kwa mungu,hatimae vimefika mwisho
ni furaha iliyo kifani,kuijenga tanzania mpya,
dhamana iliyobaki kwa mtanzania,ni chadema iliyo imara.
 
Ghanini wana wa JF, iwe busara za kwetu
wenye mikono mirefu, waingie mchechetu
tusilale kama wafu, watuiba mali zetu
Zima mchezo mchafu, tuzilinde kura zetu

....duuhh naona kumbe taratibu mashairi yanapanda......lol
 
Hongereni washairi, ya kwenu tumeyasikia
Sifa imeshamiri, itikadi tumesikia
Sababu imejiri, ya chadema kuingia
Mpigie kura Slaa, wabunge na madiwani



Kumbe namimi wamo eeh!!!
 
Tunahitaji kiongozi, wa hekima na busara
Mwenye nzuri maamuzi, ya mwelekeo wa sera
Ambaye katu hawezi, Kutoa nchi Kafara
Slaa anafaa sana. yafaa apewe nchi

Wa kuleta mageuzi, kuondoa ufukara
Akifanya uteuzi, Unde serikali bora
Huyu ndiye Kiongozi, Kiongozilo imara.
Slaa anafaa sana. yafaa apewe nchi.
 
Tunahitaji kiongozi, wa hekima na busara
Mwenye nzuri maamuzi, ya mwelekeo wa sera
Ambaye katu hawezi, Kutoa nchi Kafara
Slaa anafaa sana. yafaa apewe nchi

Wa kuleta mageuzi, kuondoa ufukara
Akifanya uteuzi, Unde serikali bora
Huyu ndiye Kiongozi, Kiongozilo imara.
Slaa anafaa sana. yafaa apewe nchi.

1. Hatuna tena uhuru, umezidi uhasidi,
Uchumi wameudhuru, kodi hazina idadi,
Ulishindwa ubeberu, utakoma ufisadi,
Ewe CHADEMA karibu, Taifa kuikomboa.

2. Dokta Slaa kinara, Tanzania waijua,
Umeshafanya ziara, hakuna usichojua,
Ruvuma hadi Mara, Kigoma mpaka Nachingwea,
Ewe CHADEMA karibu, Taifa kuikomboa.

3. Wameibukia waongo, ikulu wang'ang'ania,
Wadhania ni pango, kila nyoka kuingia,
Katu hawanao mpango, ni bure wanadandia,
Ewe CHADEMA karibu, Taifa kuikomboa.

4. Tumedumu na ujinga, tunakufa kwa maradhi,
Mafisadi wanaringa, rasilimali wahodhi,
Twabaki twamangamanga, waneemika baadhi,
Ewe CHADEMA karibu, Taifa kuikomboa.

__________________________________________________________
"Wars are caused by undefended wealth" - Ernest Hemingway
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom