Elections 2010 Mchague Slaa, tuiponye Tanzania

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Nimeliona shairi hili katika FOSI (Friends of Slaa) ni kaona niwashirikishe.


Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania


Nimelala nimekesha, jambo nimefikira
Bongo nimezichemsha, sipati jibu sawia
Hivi kweli Umekwisha Uzalendo Tanzania?
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Ona walivyoziuza, rasilimali za mtanzania
Kwa kweli inashangaza, mikataba waloingia
Kisha tukiwauliza, hawana la kutwambia
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Rushwa imekuwa ngao, kumdhulumu raia
Ubinafsi kwao nguo, vazi la kujivunia
Hizi ndizo sera zao, katu hawajui njia
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Wananchi amkeni, haki kujitafutia
Mtalala mpaka lini?, saa imeishawadia
Uwongo ukataeni Waache kuwatania
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Mkipiga kura zenu, chagueni mwenye nia
Waonesheni wanenu, muelekeo na njia
Fanyeni vitu vyenu, tuiokoe Tanzania.
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Mchagueni Slaa, kiboko cha Mafisadi
Huyu bwana hana njaa, atatwanga wakaidi
Ni kiongozi shujaa, si mtumwa wa itikadi
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
 
Hii imekaa kama kwaya ya kanisani!!
Mchungaji Slaa akiipata hii itamsaidia, kuenezea sera zake


Me nakaa pembeni waliofubaa ndio watamchagua
 
Kwetu tuko kumi nane, kura ya Urais wote tunampa Dr Slaa,

Ubunge na udiwani mmoja kura yake ni CCM, na mmoja mwingine kura ya udiwani tu ni CCM, the rest kura ni CHADEMA;

Akili zetu haziko likizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom