WanaJF salam
Ninavyofahamu kati ya wanyama wafugwao, mbwa hufugwa kwaajili ya ulinzi. Mbwa mlinzi mzuri huwafahamu mabosi wake, kwa kawaida mbwa huwafahamu wakazi wote wa nyumba kupitia kwa bosi wake. Kama mbwa anakuwa rafiki wa kila afikaje nyumbani sio tena mbwa mlinzi, bali 'pet'.
Ikiwa mbwa anambwekea mgeni na hata kumng'ata mgeni il hali bosi wake anatazama tu, wa kulaumiwa kwa kawaida si mbwa bali ni bosi wake.
WanaJF wiki yote tumeshuhudia matusi ya UVCCM hususan yaliyoelekezwa kwa baadhi ya wazee wa chama chao. Lawama nyingi tumewatupia hao vijana kwa kukosa adabu hiyo. Hapo hatuzunguzumzii waliyosema kuhusu upinzani hasa Chadema. Pengine tungeona hiyo ni kawaida, tumezoea.
Kweli matusi wanayowaelekezea wazee wao hadharani ni bure? Hiyo UVCCM ndiyo chombo cha juu katika uongozi wa CCM? Kama sio chombo cha juu hayo matusi wanayotoa mabosi wao wameridhia? Kama hawajaridhia mbona hatuoni hata moja akiomba walau msamaha kwa niaba ya hao vijana waoliopotoka? Kama hawajapotoka, na wanachofanya ni sahihi nani kawatuma? Wanapata nguvu wapi ya kuwatukana wazee wa nyumbani mwao hadharani? Je, kama wamefanya hayo kwa wazee wa nyumbani mwao- tena waasisi wa chama chao, itakuwaje kwa vyama vingine?
WanaJF, ndiyo maana sasa naanza kuamini walichosema katika kikao chao cha Dodoma kuwa wanajipanga kuwa kila hali kupambana na Chadema.
Tutashangaa nini kwa chochote kutoka kwa hao vijana ambao wameonesha utovu wa adabu hadharani dhidi ya wazee wao, wakiwafanyia chochote Chadema?
Nadhani inatosha kuwalaumu hao vijana. Inafaa kumtambua aliye nyuma yao. Kwa bahati mbaya yeyote ambaye yuko nyuma yao hatambui anaongeza mgawanyiko ndani ya chama chao na kuharakisha kifo chake. Leo ni zamu ya Sumaye na Sita kutukanwa, kesho itakuwa zamu yake. Anayeua kwa upanga naye atakufa kwa upanga. Tusubiri...
Tutafakari haya kwa mtazamo wa siasa, na sio vinginevyo.