Mbunge wa Morogoro agawia vifaa vya ujenzi wapiga kura wake

Msaada aliotoa ni kwa waathirika kutokana na nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali , ni mazingira yanayoeleweka badala ya kushinikiza kwamba anaendekeza watu, ni sawa na kusaidia walioathiriwa na mafuriko pale dar. Mbunge huyu asingeonyesha kujali wananchi wake kama alivyofanya ninyi mnaopinga huduma yake mngekuja na shutuma kwamba hawajali wapiga kura wake, huu ni mwono wa aina gani?


Turudi nyuma kidogo tuseme nyumba nyingi zimeharibiwa na upepo au whatever, huyo mbunge anaweza kuwasaidia watu kwa style hiyo? Au niweke swali hivi, hivi tutaendelea hivi hadi lini bila kuwa na coordination nzuri ya kukabiliana na majanga? N

yumba kuharibiwa kwa upepo au mvua siyo mara ya kwanza, je serikali, wananchi pamoja na wote wanaojiita viongozi wanakabiliana na hizo hali vyakutosha au ndo kupeana misaada kwa kutumia pesa ya mfuko wa jimbo harafu mbuge anajisifu katoa pesa zake kusaidia?
 
Hii tabia unawafanyia wasiojitambua tu; mtu mwenye akili zake kupewa msaada kama mtoto mdogo ni tusi la nguoni tena ni udhalilishwaji wa hali ya juu! When I see these things nashindwa kuji-control na nimeamua kuchange mind set ya raia wa Tanzania waache kabisa kudharauliwa. Siyo sifa hawa watu wana nyanyasa ndugu zetu ki-psychology kupita maelezo na ndiyo maana wanaendelea kupata nafasi wasizo stahili huku nchi ikiendelea kurudi nyuma kila siku kwakukosa wazalishaji kwani wote wanajengwa mtazamo wa kimatonya badala ya kutumia akili na nguvu zao kujiletea maendeleo.

Mkuu Ame, sijui kwa nini viongozi wetu wanashindwa kuitumia human resource (nguvu kazi iliyopo kutatua matatizo ya nchi)! jibu linalokuja ni ushikaji mwingi, kuoneana aibu, kubebana bebana na ujanja ujanja mwingi unaofanywa kwa watu wasiojiweza. Viongoiz wetu wafanye maamuzi magumu kama wanavyofanya wanapoamua kununua magari ya Mil 200 @ wakati hatuna madaktari wa kutosha, hatuna vyuo vya kutosha, walimu vyuo vikukuu wakikosa fedha ya kufanyia tafiti zenye manufaa kwa nchi nk.

Chukulia mfano: hapo morogoro ardhi ni nzuri, kwa nini asiwape mafunzo ya namna ya kusindika hata mazao yao ili wauze mikoa mingine na nje ya nchi? Chalinze matunda yanaoza kila siku, bila kujenga kiwanda cha kusindika hao matunda na kuyaweka katika hatua iliyo nzuri kuuzwa, badala yake mi nikipata kamshahara kangu nakimbilia juice ya south africa badala ya chalinze.

Hatuwezi kuendelea kwa kupeana misaada ya kihongo hongo tena kwa watu wachache huenda makada wa kambi yake, wakati huo huo kuna watu wengi wenye matatizo makubwa zaidi ya hao. Sikatai kuwasaidia lakini inabidi tuanze kupeana kavu kavu huenda ikasaidia huko mbeleni.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom