Mbunge wa Morogoro agawia vifaa vya ujenzi wapiga kura wake

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
NYUMBA+KUEZULIWA..JPG

KUKABIDHI+VIFAA+-2.JPG

Mbunge wa Morogoro mjini Aboud amewakabithi mabati 30 na mbao 50 akina mama wawili wa Kihonda ambao uwezo wao ni mdogo kusaidia kuezeka nyumba zao zilizoathiliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha nyumba nyingi kuezuliwa zikiwemo hizo mbili za akina mama.

Ni dalili serikali haiwasaidii wanainchi ipasavyo, sasa wananchi kimbilio lao ni wabunge wao. Mambo kama haya yanasababisha wabunge kuzidi kuomba nyongeza ya posho za vikao ingawa wengi hawazitumii pesa hizo kwa manufaa ya wapiga kura wao bali kwa matumizi binafsi.
 
System mbovu sana hii! Huwezi kuwasaidia watu na kuwafanya wajikomboe kwa kuwapa misaada kila wakati. They have to creat jobs, good learning environment, good governance, social services etc. Sasa viongozi badala ya kuumiza kichwa kutatua kero kama hizo wanagawa pesa au misaada kwa wapiga kura ambao wana nguvu, wana akili na afya.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Asante sana. This is what I always say. Kazi ya Serikali sio kutoa misaada panapotokea majanga. Kazi yao ni kuwajengea uwezo wananchi wajikomboe kiuchumi. Kama vile kupeleka social services, mabarabara, elimu nk.
 
Akajambe! Huyu alishatuchuma sana kwa kupandisha nauli ya mabasi yake ya aboud ya moro dar na kinyume chake. Wakati mabasi mengine yote nauli ni 5.500 mabasi ya huyu jamaa ni 6.500 hadi 7.500 kipindi hiki cha Krismas na mwaka mpya. Ana huruma gani huyu na wapiga kura wake? Anachofanya hapa ni kujionyesha tu! Hatuangalii misaada ya mtu 2015, aache kujibalaguza. mwizi tu huyu.
 
Tangia Mh.Abood Achaguliwe Kuwa Mbunge Sijasikia Akisema Lolote La Maana Bungeni...! kwakuwa he is not open minded...,yeye anachojua tu ni kutoa misaada midogo dogo kuwaridishisha wananchi!
Morogoro kuna matatizo chungu mzima na changamoto kibao...!

+tuna vyuo vikuu vinne...ambavyo ni SUA cha kilimo na MZUMBE cha biashara,mumo na Jordan! Lakini kwenye suala la kilimo wakulima wa Morogoro hawafaidiki ipasavyo na SUA! kutokana na Link ndogo kati ya Chuo na Wananchi..Kwani Morogoro Ingetakiwa Ipige Hatua Kubwa kwenye Kilimo Kutokana na Hazina Kubwa Ya chuo Kikuu cha Kilimo kinachoongoza kwa kuwa na Maprofesa Wengi pamoja na Mbinu Mbalimbali za kilimo...Tukija kwenye suala la chuo cha Mzumbe...,Morogoro kuna Tatizo kubwa sana la watu kutokujua dhana ya ujasiriamali wakati wataalamu wapo bwererere Mzumbe! Kwanini Mbunge Asiandae hata semina ndogo ndogo kwa kwaajili ya wafanyabiashara wadogo hasa machinga,mama lishe jinsi ya kuwa mjarisiamali bora na kuongeza kipato na kuinua uchumi wa biashara zao na kuongeza mzunguko wa pesa morogoro

+Suala la Utalii...,Morogoro ina hifadhi zaidi ya tatu ambazo ni mikumi,selous,udzungwa na wami mbiki,...lakini Morogoro haifadiki na Utalii hata kidogo kwa kuwa makampuni mengi ni ya Dar es salaaam,..hata vijana wadogo tour guides wanatokea dar es salaam! morogoro imekuwa kama njia tu...tuna hazina kubwa ya milima ya uluguru lakini wananchi hawaendelezwi kufaidika na rasilimali zilikuwepo zaidi ya kutegemea kilimo cha matunda na mboga mboga wakati wanaweza wakafaidika na Utalii kupitia eco tourism programme kama wenzetu usambara

+suala La miundombinu na barabara! kwakweli paka sasa hivi ukimleta mtu yeyote aangalie barabara za mjini hasa kutoka foresthill paka mjini,au kutoka boma kwa mkuu wa mkoa paka mjini...hizo barabara ni chini ya kiwango hata miaka kumi zitakuwa ni written off...na bado maeneo mengi kama kihonda,mazimbu,mjimpya,kichangani barabara ni za vumbi...,wakati bajeti inapitishwa ya miundombinu nilimwona mbunge anapitisha tu kwa kicheko bila hata kuhoji kwanini utekelezaji wa suala la barabara jimboni kwake ni kwa spidi ya kinyonga tofauti na majimbo mengine!

+Suala la Usafi...,hili sina haja la kusemea kwani wenye macho wanaliona...,juzi kati mbowe alitumia hela zake kidogo kununua trekta la kuzolea uchafu pamoja na madebe ya taka!

+suala la Michezo! morogoro tulikuwa na timu nyingi tu moro ute,polisi moro na mseto lakini yeye amekuwa akiwekeza tu kwenye timu ya simba ambayo inawafaidisha wana msimbazi morogoro haifidiki na chochote

+suala la DHAHABU...,Morogoro kna dhahabu...eneo la mindu! lakini hakujafanyika utafiti wowote ule kwakuwa eti ni eneo la hifadhi la bwawa..,mbona Selous kulifanyika utafiti wa uranium

+jamani bado changamoto ni nyingi sana...naomba mbunge wetu asugue kichwa kuliko kumwaga pesa kusaidia vitu ambavyo Ni sawa na kupunguza Tatizo bali sio kutatua tatizo...ni sawasawa na mgonjwa wa malaria unampa tu dozi badala ya kumshauri pia anunue chandarua na kwani bado kila siku hataendelea kuumwa
 
Hizi ni rushwa za kisiasa ambazo mimi sikubaliani nazo hata chembe.

TAKUKURU mko wapi?

Tuwe na ubinadamu atoae kwa wenye kuhitaji anastahili pongezi. Nape na Mbowe wametoa misaaada kwa waathirika wa mafuriko ya DSM hatukusikia TAKUKURU, iweje kwa ABOOD
 
System mbovu sana hii! Huwezi kuwasaidia watu na kuwafanya wajikomboe kwa kuwapa misaada kila wakati. They have to creat jobs, good learning environment, good governance, social services etc. Sasa viongozi badala ya kuumiza kichwa kutatua kero kama hizo wanagawa pesa au misaada kwa wapiga kura ambao wana nguvu, wana akili na afya.

Kama issue ni ku creat jobs, Abood ni mmoja wa watu walioua nafasi nyingi za kazi Morogoro kuanzia kwenye viwanda vyake vyote alivyobinafsishiwa na serikali karibu vyote havifanyi kazi ukiacha cha Canvas ambacho watu wanafanya kazi masaa 12 pa day kuanzia saa 1 as - 1 us na bado wanalipwa chini ya laki 1 kwa mwezi.
Ukija kwenye mabasi yake yote hayana makondakta, ndio inawezeka anapunguza cost, lakini anashindwa kutengeneza ajira hata chache kwa kuajiri makonda, kwani wana price gani kubwa kiivyo hadi waje walete hasara?!
Huyu mtu angekuwa yupo serious na uongozi alikuwa ana nafasi kubwa sana ya kubadili maisha ya vijana wa jimbo lake la Morogoro kwa kutengeneza ajira kuliko wabunge wote wa TZ, sababu vitega uchumi vyake vyote vipo jimboni mwake.
 
Binafsi nampongeza kwa kuwasaidia hao wahanga wa mafuriko waliokosa hela za kurepea nyumba zao baada ya janga hilo.
 
System mbovu sana hii! Huwezi kuwasaidia watu na kuwafanya wajikomboe kwa kuwapa misaada kila wakati. They have to creat jobs, good learning environment, good governance, social services etc. Sasa viongozi badala ya kuumiza kichwa kutatua kero kama hizo wanagawa pesa au misaada kwa wapiga kura ambao wana nguvu, wana akili na afya.

Msaada aliotoa ni kwa waathirika kutokana na nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali , ni mazingira yanayoeleweka badala ya kushinikiza kwamba anaendekeza watu, ni sawa na kusaidia walioathiriwa na mafuriko pale dar. Mbunge huyu asingeonyesha kujali wananchi wake kama alivyofanya ninyi mnaopinga huduma yake mngekuja na shutuma kwamba hawajali wapiga kura wake, huu ni mwono wa aina gani?
 
great thinkers wengine bwana wana chekesha sana! janga linapo kufika kama nyumba kuungua, paa kuezuliwa, mafuriko nk watu wachache sana wana weza kuyakabili kwa wakati na bila kutegemea msaada! AKITOKEA MTU KAMA ABOOD,lazima tutambue na kuheshimu alichofanya.jambo la dharura linahitaji hatua za haraka kama alivyofanya. hata kama msaada huu ungetolewa na serikali bado ni msaada tu.
 
Asante sana. This is what I always say. Kazi ya Serikali sio kutoa misaada panapotokea majanga. Kazi yao ni kuwajengea uwezo wananchi wajikomboe kiuchumi. Kama vile kupeleka social services, mabarabara, elimu nk.

Sahihi kabisa wakuu
 
sure!!! Tuliambiwa zamani kuwa usimpe mtu samaki, lakini mfundishe namna ya kuvua samaki hao!!!!!
 
System mbovu sana hii! Huwezi kuwasaidia watu na kuwafanya wajikomboe kwa kuwapa misaada kila wakati. They have to creat jobs, good learning environment, good governance, social services etc. Sasa viongozi badala ya kuumiza kichwa kutatua kero kama hizo wanagawa pesa au misaada kwa wapiga kura ambao wana nguvu, wana akili na afya.

Hii tabia unawafanyia wasiojitambua tu; mtu mwenye akili zake kupewa msaada kama mtoto mdogo ni tusi la nguoni tena ni udhalilishwaji wa hali ya juu! When I see these things nashindwa kuji-control na nimeamua kuchange mind set ya raia wa Tanzania waache kabisa kudharauliwa. Siyo sifa hawa watu wana nyanyasa ndugu zetu ki-psychology kupita maelezo na ndiyo maana wanaendelea kupata nafasi wasizo stahili huku nchi ikiendelea kurudi nyuma kila siku kwakukosa wazalishaji kwani wote wanajengwa mtazamo wa kimatonya badala ya kutumia akili na nguvu zao kujiletea maendeleo.
 
Back
Top Bottom