Mbunge wa Kigamboni aahidi kulifanyia kazi suala la uchafu na uchakavu wa vyoo vya Hospitali ya Vijibweni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Faustine Ndugulile ameona hoja ya Mdau wa Jamii Forums aliyedai Vyoo vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam ni vichafu kwa ndani, vinatoa harufu kali na pia miundombinu yake ni chakavu, anadai kwa miezi mitatu aliyofika eneo hilo hakuna taa na chache zilizopo haziwaki.

Mbunge Ndugulile amejibu kwa kuandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa “Nawashukuru sana JamiiForums kwa taarifa hii. Tumeipokea. Naahidi suala hili kufanyiwa kazi kwa haraka. Lengo letu ni wananchi kupata huduma nzuri na kwenye mazingira safi na salama.”

Mudu mfupi baadaye Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu naye akajibu Katika post hiyohiyo “Huu ndio uwajibikaji tunaoutaka. Asante sana Dr Faustine. Ukweli changamoto nyingi za wananchi kuhusu utoaji wa huduma za Afya nchini hazihitaji hadi Waziri wa Afya aseme. Endapo viongozi wengi tunafuatilia kwa karibu utoaji huduma za afya ktk maeneo yetu basi ni dhahiri kuwa lengo la Serikali la kuwafikia wananchi na huduma bora za afya tunaweza kulifikia hata kabla ya 2030. Hongera sana Dr. Ndugulile. Wana Kigamboni wamepata Mbunge makini👍. Kazi Iendelee."

Hoja ya Mdau ni hii hapa = Vyoo vya Hospitali ya Vijibweni Kigamboni ni vichafu na vimechoka kuliko maelezo
 
Hii nchi kila kitu wanasubiri viongozi waseme hadi usafi. Smh
 
KATA ya Vijibweni ina Matatizo mengi sana sio hilo la uchafu wa hospital
Matatizo yaliyopo ni pamoja na barabara zote za kata
Barabara za mji mpya Monduli kwa Mkorea kuna mradi wa viwanja 300 vimepimwa ujenzi wa nyumba za kusasa umeanza lakini barabara hazina Mitaro na hazipitiki pia UMEME haujasambazwa ktk Eneo hilo
 
Back
Top Bottom