Mbunge wa Hanang, Eng. Hayuma alilia Serikali athari za mafuriko ya Hanang

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE WA HANANG, ENG. HAYUMA AILILIA SERIKALI, ATHARI ZA MAFURIKO YA HANANG

Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara, Eng. Samwel Hayuma ameingukia serikali akiiomba kuwatazama kwa jicho la pili wafanyabiashara ambao wamepoteza mali zao kutokana na mafuriko ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 3, 2023.

Amesema licha ya Mafuriko hayo kusabisha vifo, yameleta hasara kubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara kwa kuwa baadhi yao wamepoteza mitaji huku wengine wakiwa na mikopo umiza.

Eng. Hayuma amesema ni vyema serikali ikawatambua wafanyabiashara hao ikiwemo wa soko kuu la kateshi linalojumuisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa, ambapo licha ya kuwapa mitaji, ikiwezekana zile bima mikopo walizokuwa wamezikata, zitumike kulipa madeni yao.

495dbfef-6803-4a70-8762-99fecbfb559c.jpg
 
Kama walikata bima ya mikopo bas italipwa,

Suala la mitaji na mm naunga mkono, changamoto waswahili watapiga parefu sanaaa
 
Back
Top Bottom