Mbunge wa Bahi Omary Baduel ameshinda kesi ya Rushwa iliyokuwa inamkabili

Judiciary system ya Tanzania inazidi kujidhalilisha. Kama huwezi kumfunga Baduel kwa kesi ya wazi inayohusu rushwa kama ile sijui ni nani sasa anastahili kwenda gerezani. Idara ya mahakama haina maadili, RIP judiciary system in Tanzania. Rushwa ni adui wa haki

Upo sahihi mkuu.
 
Omary-30April2015.jpg

Mbunge wa Bahi, mkoani Dodoma, Omary Badwel.




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia huru Mbunge wa Bahi, mkoani Dodoma, Omary Badwel, (pichani) baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.

Kadhalika, mahakama hiyo imemuonya mbunge huyo kuacha kufuatilia maslahi na maisha ya watu na mali zao katika jimbo lake badala yake ajishughulishe na siasa na kutekeleza majukumu yake kwa jamii.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa na kusema mahakama baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri imeona bila kuacha shaka mshtakiwa hana hatia, hivyo inamuachia huru.

"Mahakama hii imeona ushahidi uliotolewa na Jamhuri mshtakiwa huna hatia na kwamba inakuachia huru… inawezekana kweli uliomba na kupokea rushwa lakini kwa ushahidi uliotolewa hauna mashiko ya kisheria wa kuweza kukutia hatiani, " alisema na kuongeza:


"Kwa kuwa ushahidi haujathibitisha mashitaka yaliyokuwa mbele ya mahakama hii na kama unaingilia maslahi, mali na maisha ya watu huko jimboni kwako uache endelea kufanya mambo yako ya kisiasa."

Alisema kwa mujibu wa ushahidi wa mazungumzo yaliyorekodiwa na wakati wa tukio uliotolewa mahakamani, sauti ya mshtakiwa haikusikika akiomba wala kushawishi rushwa, lakini amesikika aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Sipora Liana.

Alisema pamoja na mambo mengine, mshtakiwa ana wadhifa mkubwa na kwamba siyo rahisi yeye na kamati yote kuomba rushwa yenye thamani ya Sh. milioni moja kwa kila mjumbe.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa mshtakiwa akiwa kama Mbunge wa Jimbo hilo, Mjumbe LAAC na mtumishi wa umma, alitenda kosa hilo kati ya Mei 30 hadi Juni 2, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa kinyume cha Sheria ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, Mbunge huyo alishawishi kutolewa kwa rushwa ya Sh. milioni 8 kutoka kwa Liana ili awashawishi wajumbe wa kamati hiyo wakati wa kupitia ripoti ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka 2011/12.

Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa, Juni 2, mwaka 2012, katika Hotel ya Peacock, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alipokea rushwa ya Sh. milioni moja kutoka kwa Liana kwa ajili ya kuwashawishi wajumbe wa LAAC kupitisha ripoti ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka 2011/12 bila vikwazo.

Hata hivyo, Mbunge huyo alikana mashtaka dhidi yake na alikuwa nje kwa dhamana.



Chanzo: Nipashe
 
Orodha ya PCCB yenye majina zaidi ya 200 waliotiwa hatiani ni VEO na WEO tu. Nchi hii wakubwa hawasumbuliwi. Hata kama angeshikwa na fedha mkononi huko Mahakamani tungewambiwa hizo si noti, bali ni majani ya mkungu!!!
 
Orodha ya PCCB yenye majina zaidi ya 200 waliotiwa hatiani ni VEO na WEO tu. Nchi hii wakubwa hawasumbuliwi. Hata kama angeshikwa na fedha mkononi huko Mahakamani tungewambiwa hizo si noti, bali ni majani ya mkungu!!!

Kiukweli inasikitisha sana,kwa TAKUKURU kuangushwa kila kesi inayohusu vigogo hasa wa chama hichi cha KIJANI na wafadhili wao,inabidi sasa tuanze kuhoji MAADILI ya hao waendesha mashtaka ya hii eti inayoitwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
 
Dar es Salaam. Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana alimuachia huru Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Badwel aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa, lakini akamtaka kurekebisha tabia yake mbele ya watu wanaomzunguka.

“Kama una vitu ulivyokuwa ukivifanya jimboni kwako uviache, ujirekebishe. Kama una tofauti na watu wako, urekebishe na usiguse mali wala vitu vya watu wengine,” alisema Hakimu Mkazi Hellen Liwa wakati akisoma hukumu ya mbunge huyo aliyeshtakiwa kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh8 milioni na kupokea Sh1 milioni.

Kwa mujibu wa mashtaka dhidi yake, Badwel alinaswa kwenye mtego wa Takukuru baada ya kupokea rushwa ya Sh1 milioni kwenye Hoteli ya Peackock kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Sipora Liana ili amsaidie kufanya ripoti ya fedha iwe safi.

Lakini Hakimu Liwa alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, ameona hakuna ushahidi unaoweza kumtia hatiani mshtakiwa bila ya kuacha maswali.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Liwa alisema amemuachia huru mbunge huyo baada ya kupitia ushahidi, vielelezo pamoja na utetezi wa mshtakiwa mwenyewe na kubaini kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake pasipo kuacha shaka yoyote.

Hakimu Liwa alisema katika ushahidi wa CD uliowasilishwa na ofisa mtaalamu wa uchunguzi wa Takukuru, kuna mazungumzo kati ya Liana na Badwel ambaye alikuwa akiomba rushwa na kwamba Mahakama ilisikia sauti hiyo na kuona kwa upande mmoja inafanana na ya mshtakiwa lakini akasema haifahamu sauti ya mlalamikaji.
“Hata hivyo, niliposikiliza hiyo CD, sikusikia mshtakiwa akiomba rushwa. Nilisikia mlalamikaji akianzisha mazungumzo na mshtakiwa akijibu na ilikuwa ikionyesha mshtakiwa akizubaa, mlalamikaji anamchangamsha.”

Alibainisha kuwa siku hizi kuna watu mitaani ambao huigiza sauti za wengine na mlalamikaji alidai kuwa yeye na Badwel hawafahamiani vizuri na kwamba ushahidi huo unatia shaka mbele ya Mahakama.

Alisema mshtakiwa alikanusha kuomba wala kupokea rushwa, lakini alikiri kuwapo Hoteli ya Peackock siku ya tukio kwa mazungumzo mengine. Kwa maelezo yake, mlalamikaji alionyesha kuwa wabunge hao walikuwa na ushirikiano na kusaidia mtu mwenye hati chafu kwa kuchukua fedha.

“Mahakama inajiuliza mshtakiwa alikuwa na nguvu gani kama mjumbe, ya kushawishi kamati kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Liana na alikuwa na nguvu gani ya kusaidia ripoti chafu iwe safi?” alihoji Hakimu Liwa.

“Kama ni kweli mbunge huyu na wadhifa wake anaweza kupokea rushwa ya Sh1 milioni ni kuharibu utu wake na ni aibu kubwa kwa Taifa. Lakini mashahidi wote walisema walimuona Liana akiwa na bahasha ya kaki na aliiweka juu ya meza.”

Hakimu Liwa alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote mawili yanayomkabili mbunge huyo pasipo kuacha shaka yoyote na hivyo kumuachia huru

Mwananchi,April 30
 
PCCB haiko kwa ajiri ya vigogo,na ndio maana huwa hakuna kigogo ambaye chombo hiki kina weza kumuadabisha!
 
Mbunge wa CCM kupelekwa Mahakamani kwa kosa la rushwa ili kuwa ni zuga,rushwa ni rushwa kwa mdogo kwa kiongozi wa CCM ni takrima.
 
PCCB haiko kwa ajiri ya vigogo,na ndio maana huwa hakuna kigogo ambaye chombo hiki kina weza kumuadabisha!
Unasemaje kuhusu Liumba,vipi kuhusu yule mkurugenzi mkuu wa TBS..Tunatakiwa tuwaunge mkono Pccb,vita ya rushwa ni ngumu sana tuache kulaumu,Kuthibitisha mashtaka ya rushwa ni vigumu kuliko hata kuthibitisha kesi ya ugoni.
 
Back
Top Bottom