Mbunge wa Bahi Omary Baduel ameshinda kesi ya Rushwa iliyokuwa inamkabili

Mathias Lyamunda

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
1,369
558
Taarifa nilizozipata kutoka chanzo cha kuaminika Mbunge wa Bahi ameshinda kesi ya rushwa iliyokuwa inamkabili.
==============
Omary-30April2015.jpg

Mbunge wa Bahi, mkoani Dodoma, Omary Badwel

30th April 2015
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia huru Mbunge wa Bahi, mkoani Dodoma, Omary Badwel, (pichani) baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.

Kadhalika, mahakama hiyo imemuonya mbunge huyo kuacha kufuatilia maslahi na maisha ya watu na mali zao katika jimbo lake badala yake ajishughulishe na siasa na kutekeleza majukumu yake kwa jamii.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa na kusema mahakama baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri imeona bila kuacha shaka mshtakiwa hana hatia, hivyo inamuachia huru.

"Mahakama hii imeona ushahidi uliotolewa na Jamhuri mshtakiwa huna hatia na kwamba inakuachia huru… inawezekana kweli uliomba na kupokea rushwa lakini kwa ushahidi uliotolewa hauna mashiko ya kisheria wa kuweza kukutia hatiani, " alisema na kuongeza:
"Kwa kuwa ushahidi haujathibitisha mashitaka yaliyokuwa mbele ya mahakama hii na kama unaingilia maslahi, mali na maisha ya watu huko jimboni kwako uache endelea kufanya mambo yako ya kisiasa."

Alisema kwa mujibu wa ushahidi wa mazungumzo yaliyorekodiwa na wakati wa tukio uliotolewa mahakamani, sauti ya mshtakiwa haikusikika akiomba wala kushawishi rushwa, lakini amesikika aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Sipora Liana.

Alisema pamoja na mambo mengine, mshtakiwa ana wadhifa mkubwa na kwamba siyo rahisi yeye na kamati yote kuomba rushwa yenye thamani ya Sh. milioni moja kwa kila mjumbe.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa mshtakiwa akiwa kama Mbunge wa Jimbo hilo, Mjumbe LAAC na mtumishi wa umma, alitenda kosa hilo kati ya Mei 30 hadi Juni 2, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa kinyume cha Sheria ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, Mbunge huyo alishawishi kutolewa kwa rushwa ya Sh. milioni 8 kutoka kwa Liana ili awashawishi wajumbe wa kamati hiyo wakati wa kupitia ripoti ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka 2011/12.

Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa, Juni 2, mwaka 2012, katika Hotel ya Peacock, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alipokea rushwa ya Sh. milioni moja kutoka kwa Liana kwa ajili ya kuwashawishi wajumbe wa LAAC kupitisha ripoti ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka 2011/12 bila vikwazo.

Hata hivyo, Mbunge huyo alikana mashtaka dhidi yake na alikuwa nje kwa dhamana.

CHANZO: NIPASHE
 
Tanzania hii niijuayo hakuna mlarushwa Mkubwa anaweza shindwa kesi.Ni wala rushwa wadogo ndio wana kiona cha moto.($1=ths.2050).October tulirekebishe hili
 
Kuna suala la kuogopa kupoteza jimbo! Tuone Kama jina lake litarudi kwa kura za maoni!!! Wamefunika kombe........!!!
 
Anayeilaumu mahakama kumwachia anakosea sana ? naamimi hujasoma hukumu na mwenendo wa kesi sasa unalaumu mahakam kwa lipi? kama mashahidi wanajichanganya wenyewe unafikiri mahakama ifanyeje wakati unatakiwa uthibitishe shtaka pasipo shaka la maana? Aliyesoma mwenendo na Hukumu wa kesi hiyo pekee ndio mwenye haki ya kulalamikia hukumu hiyo
 
Anayeilaumu mahakama kumwachia anakosea sana ? naamimi hujasoma hukum

u na mwenendo wa kesi sasa unalaumu mahakam
kwa lipi? kama mashahidi wanajichanganya wenyewe unafikiri mahakama ifanyeje wakati unatakiwa uthibitishe shtaka pasipo shaka la maana? Aliyesoma mwenendo na Hukumu wa kesi hiyo pekee ndio mwenye haki ya kulalamikia hukumu hiyo

Una akili sana mkuu,kula LIKE
 
Anayeilaumu mahakama kumwachia anakosea sana ? naamimi hujasoma hukumu na mwenendo wa kesi sasa unalaumu mahakam kwa lipi? kama mashahidi wanajichanganya wenyewe unafikiri mahakama ifanyeje wakati unatakiwa uthibitishe shtaka pasipo shaka la maana? Aliyesoma mwenendo na Hukumu wa kesi hiyo pekee ndio mwenye haki ya kulalamikia hukumu hiyo

Kaa kimya wewe hujui mauzauza ya mahakamani, mahakimu wengi ni wala rushwa hawaachi hata sh 50,000/- wanatamaa sana
 
TAKUKURU huwa wanashindwa kesi nyingi, nchi hii ukihukumiwa Kwa kesi ya rushwa na ukapatikana na hatia basi umependa mwenyewe.
 
Anayeilaumu mahakama kumwachia anakosea sana ? naamimi hujasoma hukumu na mwenendo wa kesi sasa unalaumu mahakam kwa lipi? kama mashahidi wanajichanganya wenyewe unafikiri mahakama ifanyeje wakati unatakiwa uthibitishe shtaka pasipo shaka la maana? Aliyesoma mwenendo na Hukumu wa kesi hiyo pekee ndio mwenye haki ya kulalamikia hukumu hiyo

Unatakiwa kufahamu kuwa katika dola la wala rushwa, huo mwenendo wa kesi/mashitaka hutengenezwa.
 
Anayeilaumu mahakama kumwachia anakosea sana ? naamimi hujasoma hukumu na mwenendo wa kesi sasa unalaumu mahakam kwa lipi? kama mashahidi wanajichanganya wenyewe unafikiri mahakama ifanyeje wakati unatakiwa uthibitishe shtaka pasipo shaka la maana? Aliyesoma mwenendo na Hukumu wa kesi hiyo pekee ndio mwenye haki ya kulalamikia hukumu hiyo
TAKUKURU Wafatilie mwenendo mzima wa kesi, kuna inshu yatu kuongwa na kupoteza ushahidi, cocaine inabadilika inakua very fine grained sugar! afu mnategemea maendeleo!!. ONYESHA UNA AKILI TIMAMU OCTOBER KWA KUTOICHAGUA CCM.
 
Sasa kuna haja gani ya kesi kama matokeo yalishajulikana
Wanasheria mtusaidie hapa...fani imeingiliwa na ukanjanja?
Prosecutors sio wanasheria?
Magistrates sio wanasheria?
 
Back
Top Bottom