Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema apelekwa mahabusu

Wapenda Amani wa Arusha na CDM wasiokuwa na mrengo mkali jitihada zao za kumsihi lema kukubali dhamana hazikufanikiwa..

Sasa mtu kama huyu utamuita kweli shujaa?
kwa chadema ananaonekana shujaa...lakinini kwa waelewa anaonekana mbumbumbu. Usitumie nguvu yako kubwa kuhangaika nao ritz, waache wafu wazike wafu wao
 
Mods ina maana hamjaona matusi waliyonirushia hawa vijana wa Lema. Au mnataka niwajibu mnizawadie BAN.

Mzee,
Nakushari usijibu kitu utakula Ban, uliza mkuu Rejao yupo wapi? Si kala Ban alijibu tusi
 
kwa chadema ananaonekana shujaa...lakinini kwa waelewa anaonekana mbumbumbu. Usitumie nguvu yako kubwa kuhangaika nao ritz, waache wafu wazike wafu wao

Feedback,
Unadhani natumia nguvu basi nguvu nayotumia kama yako unaoitumia kulazimisha Lema awe shujaa
 
Kamanda Andengeye yupo Arusha kweli? Kwa nini vijana wake wanahangahika na vitu vidogo wakati mji wa Arusha ukiwa na challenges nyingi tu za usalama? Na ni kwa nini huyo kamanda wa Arusha mjini ameachwa na wakubwa zake kufanya mambo ya KUBWA JINGA? Arusha kumejaa mirungi,bhangi,dawa za kulevya,ujambazi nk. Badala ya Polisi kufanya kazi za kuondoa kero hizo,wanasaidiana na CCM kuhujumu Upinzani.
 
Siasa za namna hii cjui zitatufikisha wapi aisee manake Lema tangia awe mbunge cjui kama amefurahia ubunge wake kwa kweli......Wanamuamndama kinyama nadhani hata akishindwa kesi sidhani kama ccm watachukua jimbo hilo kule Arusha hii naona ni vita ya kisiasa isiyo na tija hapo mbele.
 
nashangaza sana mfumo wetu wa siasa na uendeshaji wa nchi yetu,tunapoteza muda mwingi kwenye malumbano yasiyo ya kimsingi na kuacha kutumia fikira zetu kwa mambo ya maendeleo,kila leo ni misamiati mipaya,mara kujivua gamba,mara kuwekana ndani lakini matatizo muhimu yanayoikabili nchi hayatiliwi maanani.Hii ni kutokana kuwa tumeshazaa tabaka la watawala.Wagonjwa wanasongamana muhimbili mwingine akiharisha mara moja ndege inakodishwa aende India.Ole wenu angalieni Gadafi,Mubarak walivyoadhirika binadamu ni binadamu tu.
 
Hizi kweli ni mbwembwe..... ila wapiga kura wake tuwe makini mwaka 2015, huyu jamaa analeta mbwembwe huku miaka mitano inayoyoma bila kutusaidia lolote wananchi wake... buuushit kwani tulimchagua ili akarumbane na kujipeleka jela... waraka mzima ni pumba tupu nyambafu weee!
 
Wakazi wa Arusha jitahíni kumuelimisha mbunge wenu. Kuna matatizo mengi ya kushughulikia. 2015 sio mbali.
 
Sikujua kuwa Mhe Lema ana akili kiasi hiki.

Siku nyingi ametafuta jinsi ya kuwasiliana na machalii waliokuwa pamoja kwenye ile biashara ya kupora magari na sasa wako jela. Kwa kujipeleka mwenyewe jela atapata fursa ya kushauriana nao na kuweza kujenge utetezi mzuri wa kesi yake inayokuja ya wizi wa magari.

Huyu chalii kumbe iko kichwa licha ya elimu yake ya Form II.
 
Mbunge wa Arusha Goodbless Lema anatumia mbinu inayoitwa civil disobedience. Mbinu hii imetumiwa na wanaharakati na watu maarufu duniani waliokuwa wanadai haki kutoka kwa watawala wakandamizaji. Hawa watu ni kama Mahatma Gandhi, Luther King, na Mandela. Hii mbinu inatumika kupinga sheria na amri kandamizi zinazotoliwa na watawala ili kuhujumu kikundi cha jamii ndani ya nchi kwa faida ya watawala.

Kwa mfano Mahatma Gandhi alipambana sana na wakoloni wa Kiingereza kule India kwa kutumia hii mbinu mpaka wakoloni wakaondoka wenyewe. Kuna wakati alishitakiwa na kutakiwa kulipa faini lakini yeye alisema hatalipa hiyo faini na hakulipa. Gandhi ni miongoni wa viongozi maarufu kuwahi kutokea hapa duniani.

Mandela alichagua kwenda gerezani badala ya kuwa mnafiki na kukubali masharti ya makuburu. Tunajua alikaa jela miaka zaidi ya ishirini na baadaye aliachiwa na kuwa shujaa wa ukombozi wa mtu mweusi wa Afrika Kusini.

Luther King aliendesha harakati za kudai haki bila fujo kwa watu weusi na wengine ambao hawakuwa na haki sawa kama wazungu kule Marekani. King ni mtu maarufu duniani na hata kushinda marais wengine wa marekani. Hivi majuzi tu sanama yake ilizinduliwa kule marekani na imewekwa sehemu maarufu na muhimu sana kwa watu wa marekani.

Hawa wote walifanikiwa katika harakati zao.

Katika jamii yenye ukandamizaji wa haki kwa kutumia sheria na amri na kutishia watu kwa silaha na jela inafika wakati watu wanachoka na wanaanza kudai haki zao kwa njia ya civil dionedience.
 
Hajapata kutoke kiongozi mwenye msimamo mpenda watu kama lema tz,anaamini katika haki na anapinga dhulma ya aina yeyote.
 
Wakitokea watu 10 kama kamanda Lema nawaambieni polisi wa serikali ya ccm pamoja na mahakama zao lazima watafuata haki na ukweli.
Watanzania wamenyanyaswa vya kutosha, wanahitaji mkombozi, na si mwingine, ni viongozi ambao wapo tayari kufa kwa ajili ya kudai haki na usawa. Huyo si mwingine bali GODBLESS JONATHAN LEMA kamanda wa nchi kavu!

Mungu Mbariki Lema
Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania
Amen!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom