Elections 2010 Mbunge wa Arusha apigwa hadi kuzirai na jeshi la polisi

Mbegu wanayopanda kwa tamaa zao za madaraka watakuja ijutia sana hawa CCM. Common wisdom imeyeyuka vichwani mwao na bado wapo desperate kwa kushindwa vibaya 2010. Ule usemi wao wa ushindi kwa vyovyote wajiandae maana siku watanzania wakianza kuziona nguo za kijana kama wameona nyoka wajue nchi itakuwa mashakani kwani polisi hawawezi kuwa kila mahali. Amani hailindwi kwa mtutu wa bunduki au vifaru. Amani inalindwa siyo tu kwa haki kutendeka bali kwa kuonekana haki inatendeka. Kitendo cha Mkuchika na kina Makamba kuagiza wakurugenzi wahakikishe CCM inashinda hata kama kura za madiwani hazitoshi wao kushinda kuna hatarisha amani ya nchi. Wanajua kuwa baada ya kufanya manuva yao watu watasahau kama walivyo sahau yaliyojiri November baada ya uchaguzi wajue wanajidanganya.

Ni ukweli usiopingika kuwa kama CCM pekee wamefanya uchaguzi wa meya basi huyo atakuwa bado ni mgombea wa umeya kupitia CCM kama walivyofanya kwa Uspika. Wampeleke huyo mgombea wao akapambane kwenye ukumbi wenye Madiwani wote wa Arusha. Kama wanatarajia CDM watafungua Kesi halafu wao waipige karenda mpaka 2015 May ndiyo watoe hukumu wajue wanamuweka mtu wao kwenye mazingira ya hatari kwa miaka mitano.
 
Awafungulie mashitaka kwenye mahakama ipi ambayo unategemea itatenda haki? Wakati kila mahali wameshika wao na hawataki kuachia hata umeya.

Lakini sisi ni wabinafsi na waoga wakubwa tunajihurumia hatuwezi kudai haki zetu barabarani kitu ambacho watoto wetu watakuja kutemea mate makaburi yetu na kutulaani kwa kutokuwa wajasiri.

TUAMKENI JAMANI HAYA MAMBO YA KIZAMANI SANA

Lazima tuanze kwa kuchukua hatua za kisheria ili kuthibitisha kwa ushahidi kuwa mahakama zinatoa hukumu za kupendelea.

Yasipofunguliwa mashtaka, hili suala la mbunge kupigwa litakuwa limepita tu hivi hivi kwa kuwa hizo hatua ambazo si za kisheria nazo hazijachukuliwa.
 
Ndugu zangu,

sasa nchi yetu imefikia pabaya,tumekuwa tukijadili kuwa uchaguzi uliopita haukuwa halali hatakidogo.Jana katika wilaya kadhaa kumekuwa na uchaguzi wa meya ikiwamo halimashahuri za mwanza,Arusha,kilimanjaro,msoma.ukerewe na hai.

cha kushangaza halmashahuri zote zinazochukuliwa na chadema zimepata shida sana ikiwamo kupigwa na kuumizwa vibaya.

Katika mkoa wa Arusha jana waliahirisha na leo viongozi wale wa mji wa Arusha wameamkia katika ukumbi na kukuta CCm wameamka saa kumi usiku na kupiga kura bila kuwaharifu madiwani wa chadema.ndugu zangu hii si halali,ninapoongea sasa Mbunge lema amepigwa na polisi mpaka kupoteza fahamu na bila hata haibu wamemfungia chumbani.

IGP na viongozi wa juu wa polisi wapo Arusha na baada ya kupata taarifa hizi wameacha kupokea simu.

Jamani mimi nafikiri mwisho wa kuionea au kuibembeleza CCM umefika hapa hakuna Democrasia.sheria inasema any election should be free and fair.

NA POLISI HAWARUHUSIWI KUINGIA NDANI YA KIKAO CHA COUNCIL KWANI NI KIKAO KAMA CHA BUNGE.

inasikitiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiisha sana na moyo wangu unamajonzi.

Naomba nifahamishwe ni hospital gani amelazwa Lema? Pia uchaguzi kufanyika usiku mbona hainiingii akilini? Matokeo yameshatangazwa ya uchaguzi huo? Nashukuru mkuu kwa taarifa lakini nijibu hayo maswali.
 
Wana JF naomba confirmation and update on the story. Kuna rafiki kanihabarisha kwamba mbunge Lema yupo hoi hospitalini baada ya kupata kichapo cha Polisi huko Arusha. Sijui ndo mambo ya chaguzi za Umeya?
 
NI HATARI!
kitendo kilichofanywa hakivumiliki kwa nchi yenye kunadi demokrasia kama Tanzania! wanachofanya ni usanii mtupu na kwa nini uchaguzi ufanyike alfajiri?

Walikuwa wana waaminisha watu kuwa vyama vya upinzani vitamwaga damu! mbona wafanya mambo ya ajabu namna hii!? Huu ni mwanzo tu wakuleta machafuko tutaona mengi kama katiba haita badilika kabla ya 2015. CCM msituingize kwenye machafuko.

 
mmh! kama ni kweli hii ni hatari, lazimamafisadi wakiongozwa na Lowasa watakuwa nyuma ya hii scandal. ccm watambua kuwa tone moja la damu watakayo mwaga itawaghalimu milele.
 
Ni kweli kapigwa ile mbaya na polisi, baada ya kudai haki itendeke kwenye uchaguzi wa umeya wa jiji la Arusha, ambapo CCM wamewaleta mamluki wakapige kura. Mbunge wa viti maalum kutoka Tanga ni mmoja wa watakaopiga kura ya umeya wa Arusha.

Hivi tunavyoongea Mh. Lema yupo hoi kaumizwa sana na polisi. And he is still under polisi custody for CCM's personal interests.

No freedom of Democracy in Tz.
 
ni kweli kabisa MP Lema kapigwa na polisi na kuondolewa eneo la tukio na gari ya police. Niko maeneo ya karibu nitawahabarisha zaidi
 
Awafungulie mashitaka kwenye mahakama ipi ambayo unategemea itatenda haki? Wakati kila mahali wameshika wao na hawataki kuachia hata umeya.

Lakini sisi ni wabinafsi na waoga wakubwa tunajihurumia hatuwezi kudai haki zetu barabarani kitu ambacho watoto wetu watakuja kutemea mate makaburi yetu na kutulaani kwa kutokuwa wajasiri.

TUAMKENI JAMANI HAYA MAMBO YA KIZAMANI SANA
Hapo umesema kaka ila taratibu tumeanza kuchoka na watu wengi wa arusha hawakujua kinachoendelea jana na leo....nimefika polisi wamejaa na silaha nikaenda halimashauri napo poli wametanda hawataki kuona mtu maeneo hayo zaidi ya dreva tax wa sehemu hizo...nikamuuliza polisi moja kwanini wamempiga Lema kwa dharau kabisa akajibu ulitaka tumfanye nini? ila Lema kaumizwa sana hii inaimanisha Tanzania hakuna amani tena imebaki kwenye kumbukumbu tu.....Nasikia wamesha mchangua meya na naibu wamempa yule wa TLP bw Kivuyo diwani wa sokoni one
 
Mh Godbless Lema amejikuta akiangukia mikononi mwa police na kupata kipigo kikali kabla ya kupakiwa kwenye karandinga na kupelekwa police kisa kugomea uchaguzi wa Meya wa Arusha. Godbless amegomea uchaguzi usifanyike kisa kuna mamluki mmoja aliyepenyezwa na ccm wakati yeye sio diwani wa kata yoyote ile mjini Arusha.
Mengi nitawajuza baada ya kupata habari kamili, naendelea kukusanya data zenye uhakika. Kaa standby....
 
Katika mkoa wa Arusha jana waliahirisha na leo viongozi wale wa mji wa Arusha wameamkia katika ukumbi na kukuta CCm wameamka saa kumi usiku na kupiga kura bila kuwaharifu madiwani wa chadema.ndugu zangu hii si halali,ninapoongea sasa Mbunge lema amepigwa na polisi mpaka kupoteza fahamu na bila hata haibu wamemfungia chumbani.

IGP na viongozi wa juu wa polisi wapo Arusha na baada ya kupata taarifa hizi wameacha kupokea simu.

Jamani mimi nafikiri mwisho wa kuionea au kuibembeleza CCM umefika hapa hakuna Democrasia.sheria inasema any election should be free and fair.

NA POLISI HAWARUHUSIWI KUINGIA NDANI YA KIKAO CHA COUNCIL KWANI NI KIKAO KAMA CHA BUNGE.

inasikitiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiis ha sana na moyo wangu unamajonzi.

Mwisho wa CCM ndiyo wakaribia hasa unapoona wanatumia nguvu nyingi kudhulumu haki ya raia wasio na hatia.....................
 
mmh! kama ni kweli hii ni hatari, lazimamafisadi wakiongozwa na Lowasa watakuwa nyuma ya hii scandal. ccm watambua kuwa tone moja la damu watakayo mwaga itawaghalimu milele.
na sikia alikuwa ametoa mil 200 kwa ajili ya kuhakikisha meya anatoka CCM, hasa ukizingatia vitega uchumi vyake viko arusha..
 
Huoni kuwa bado CCM yaweza kuibuka kideda kama huyo mwingine.............Namelo Sokoine kuongezwa kiujanjaujanja....yamaanisha CCM ni 15 na Chadema plus TLP ni 15.................Au CCM uwepo mgawanyiko na hivyo kuwaruhusu Chadema kushinda?
walikuwa 14, wakaongezwa namelo Sokoine na Mary Chitanda hivyo kuwa 16 huku CDM wakibaki 14 nawa TLP kawaunga mkono maana wamempa unaibu meya hivyo wana kura 17...
 
Inawezekana kweli uchaguzi kufanyika saa 10 ya usiku na tena madiwani wa chama kimoja wote wasishirikishwe au kushiriki? Ripoti yake itaandikwaje na matokeo yake yatatangazwaje? Hebu tusubiri kuona maajabu haya. Na Lema kapigwa katika mazingira yapi hasa?
 
Heshima kwenu wanjamvi,

Ni kweli Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Godbless Lema kapigwa sana na polisi [FFU].
Jana iliamuliwa kikao cha kumchagua Meya wa Jiji la Arusha kifanyike leo saa 3 asubuhi,kikao cha jana kilishindwa kumchagua Meya kwasababu CCM walitaka kumchomeeka mjumbe kutoka Tanga ili kuwasaidia kwenye mchakato wa kupiga kura pamoja na mizengwe ya kumchomeka mjumbe wa Tanga lakini bado CHADEMA walikuwa na nafasi ya kushinda kwakuwa diwani wa TLP Mheshimiwa Kivuyo alikuwa akiwaunga mkono CHADEMA.

Maajabu yalianza kujitokeza hiyo saa 3 asubuhi badala ya wajumbe wa CHADEMA kwenda kwenye kikao cha kumchagua Meya waliamua kufanya kikao Hotel Ikweta mkabala na ukumbi wa manispaa ya Arusha.Mheshimiwa Kivuyo baada ya kuona wajumbe wa CHADEMA hawaingii kwenye mkutano aliamua kuwafuata Ikweta Hotel kuwasihi wahudhurie kwenye kikao kwakuwa bado walikuwa na nafasi ya kushinda kiti cha umeya lakini juhudi zake hazikuzaa matunda wajumbe wa CHADEMA waliendelea kususia kikao cha uchaguzi wa Meya.

Mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi wa Meya Bwana E Chang'ah aliamua kufanya mawasiliano na ofisi ya waziri mkuu.Waziri wa nchi Tawala za mikoa na serekali za mitaa alitoa maagizo sheria zifuatwe kwa kuwa idadi ya wajumbe ilifikia nusu mchakato wa uchaguzi ukaendela bila ya wajumbe wa CHADEMA kushiriki kwenye kikao.Wajumbe wa CHADEMA wakajulishwa Meya tayari kachaguliwa wakaamua kuingia kwenye kikao wakiongozwa na Mheshimiwa Mbunge G Lema.Zilitokea purukushani za hapa na pale Lema akachomoa bastola FFU wakmvamia na kumpokonya na kumpiga vibaya sana.

Wanajamvi CHADEMA hawakuwa na sababu za kutoingia ndani ya kikao cha uchaguzi wa Meya.Meya alipochaguliwa wajumbe wa CHADEMA wakaamua kuingia sijui waliingia kufanya nini ?.Lema hakutakiwa kutoa bastola yake wakati askari wa usalama walikuwepo eneo la tukio sijui alitaka kumpiga nani ?.Ikumbukwe Lema ana kesi ya kutishia kuuwa Mkurugenzi wa Jiji.
 
Yale Yale ya ivory coast na zimbabweee.

Nimesema mara kadhaa hapa kwamba tz hakuna amani bali wanaoonewa na kudhulumiwa haki hukubali yaishe. Siku wakigoma kukubali tutaoneka pumbafu kuliko kuliko mwafrika aliye hai leo na wale wote waliokufa.
 
Back
Top Bottom