Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
Diwani Chadema kuwania umeya Arusha
Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 13th December 2010 @ 11:08
DIWANI wa Kata ya Kimandolu katika Jiji la Arusha, Estomi Mallah amepitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwania kiti cha umeya wa jiji hilo.
Mallah aliyekuwa akitajwa kwa muda mrefu kuwania nafasi hiyo, alipitishwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Chadema ya Wilaya ya Arusha kilichofanyika juzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Arusha, Derick Magoma, Kamati ya Utendaji iliamua kupitisha jina la Mallah bila ya kipingamizi chochote baada ya kuungwa mkoani na wajumbe wote waliohudhuria kikao hicho.
Magoma alisema Kamati ya Utendaji ilizingatia vigezo mbalimbali kupitisha jina la mgombea huyo huku akitaja mojawapo ya kigezo kuwa ni uzoefu katika nafasi ya uongozi pamoja na uadilifu.
Tumepitisha jina la Diwani wa Kata ya Kimandolu, Estomi Mallah, hivyo ule uvumi wa muda mrefu tumeukata mzizi na huyo ndiye atakayepeperusha bendera yetu katika kuwania kiti cha umeya wa jiji la Arusha, alisema Magoma.
Mshindi wa kiti cha umeya wa Jiji Arusha atapatikana kwa wingi wa kura za wajumbe kutoka vyama tofauti huku Chadema ikifungana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wote kwa kuwa na wajumbe 14, wakati Tanzania Labour Party (TLP) ina kura moja ya diwani mmoja.
Chadema ina madiwani wanane, madiwani watatu wa Viti Maalumu, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini pamoja na wabunge wawili wa Viti Maalumu, wakati CCM ina wajumbe 14; madiwani 10, Mbunge wa Viti Maalumu na madiwani watatu wa Viti Maalumu.
Hata hivyo, kura moja ya TLP kupitia kwa diwani wake wa Kata ya Sokoni One, Michael Kivuyo, ndiyo huenda ikaamua kitendawili cha umeya wa jiji kwa upande atakaamua kuupigia kura. (tamati).
Caption Page 27 Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo akimkabidhi Meneja Mkuu Msaidizi wa Benki ya Exim, Vamadevan Sreeekuma (wa pili kushoto) tuzo ya utayarishaji mzuri wa hesabu ya mwaka 2009 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa benki hiyo, Lydia Kokugonza na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mercy Silla. (Na Mpigapicha Maalumu).