peri
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 2,579
- 1,164
Malengo ya awali ya kuwasha mwenge yalikuwa mazuri sana!
"Kuwasha mwenge, na kuuweka Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete tumaini, pale ambapo hapa matumaini, upendo mahali penye chuki, na heshima ambapo pamejaa dharau!"
Tatizo ni kwamba, wapo nje ya malengo! Kucheza ngoma na kuiambukiza vijijini!
mkuu, mwenge unamulika mipaka kvp au unaletaje amani na matumaini?
Hakukuwa na sababu ya kuwa na mwenge wala hauna tija na haukuwahi kuwa na tija.
Amani, upendo na matumaini vinatokana na watu wenyewe sio kitu kisicho na uhai.
Huko ni sawa na kuabudu sanamu lisiloweza kujifuta vumbi pale linapo chafuka nawe unalitegemea likukinge na shari.
Nasari kama mbunge angetakiwa kutoa hiyo hoja yake bungeni na sio kuanzia kwa wananchi.
Angetakiwa atumie wananchi kama silaha ya mwisho baada ya bunge kukataa hoja yake.