Mbunge wa Arumeru Mashariki mh. Joshua Nasari ahamasisha wananchi kugomea Mwenge wa Uhuru

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia chama cha CHADEMA amehamashisha wananchi wa Jimbo lake kugomea shughuri zote za mwenge wa Uhuru ktk Jimbo lake kwani hauna tija kwa wananchi wa jimbo hilo na hauna maana yoyote.

Na kahamasisha wananchi wake kuendelea na shughuri zao za kila siku.

Hii inahashiria nini kwa nchi?

Hapa najiuliza nashindwa kupaja majibu yenye tija na umuhimu wa shughuri husika.

Mh. Kayanza Peter Pinda yupo katika ziara ya nchi bila shaka nchi nzima katika kukagua, kuhimiza na kufungua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ona imefika wakati hadi mama Tunu Pinda anauliza swali kwa mmewe anayetembea nae kote ii hari kwamba kama hawaonani.

Nauliza mwenge unauzunguka na Pinda anavyozunguka kuna tofauti gani????
 
Safi sana J.N naungana na wewe mwenge wa uhuru lengo lake lishapotea kwa sasa ni wizi na ufujaji wa fedha zetu za walipa kodi+kueneza maambukizi ya ukimwi+kurudisha nyumba maendeleo!
 
naunga mkono hoja

kwanini nchi iendelee kupoteza pesa kwa mambo ambayo yamepitwa na wakati
 
huu mwenge wakaupumzishe makumbusho tu.ukitathmini fedha na rasalimali inayotumika kupokea mwenge ktk halmashauri ni wazi utaona kuna ufujaji mkubwa usio na tija.
Kwa mfano:unaweza kusikia mafuta yaliyopangwa kutumiwa na idara flani ndani ya halmashauri yametumiwa kwenye shughuli za mwenge.

Mawazo ya nassari ndio mawazo mbadala yanayoendana na kizazi cha sasa.
Mbio za mwenge zimekuwa ni harakati za makada wa ccm kujinadi kwa wananchi kwa hiyo hauna tija katika mazingira ya sasa ya vyama vingi.
 
Nimekuwa nikijiuliza huu mwenge wa sasa ni kwa faida zipi pasipo kupata majibu!!
1.Kumulika mafisadi au kuwamulikia mafisadi?

Hivi bado wanafunzi wanachangishwa fedha ya mafuta ya mwenge?
 
Taarifa ya uhakika niliyonayo, walimu wote wa wilaya ya Mvomero walikatwa pesa kwa nguvu kutoka kwenye mishahara yao, eti kisa mwenge!!! Upuuzi mkubwa!! Mwenge ni ibada ya shetani na inapaswa tuugomee ili serikal ifaham kuwa wananchi tumeanza kuwa na akili sasa. . . . . .
 
Nimekuwa nikijiuliza huu mwenge wa sasa ni kwa faida zipi pasipo kupata majibu!!
1.Kumulika mafisadi au kuwamulikia mafisadi?

Hivi bado wanafunzi wanachangishwa fedha ya mafuta ya mwenge?

Malengo ya awali ya kuwasha mwenge yalikuwa mazuri sana!

"Kuwasha mwenge, na kuuweka Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete tumaini, pale ambapo hapa matumaini, upendo mahali penye chuki, na heshima ambapo pamejaa dharau!"

Tatizo ni kwamba, wapo nje ya malengo! Kucheza ngoma na kuiambukiza vijijini!
 
kwanza kazi ya mwenge ni nini? wanakula hela vibaya, kuna walimu walifanya kazi ya kuwasha na kuzima mwenge ila hawajalipwa hela yao mpaka kesho, hela imeliwa juu kw juu.
 
Hivi wanaposema mbio za mwenge zinazindua miradi wa maendeleo,hapa napata
kigugumizi.Kwani hiyo miradi imefadhiliwa na huo mwenge?Ni kwanini isizinduliwe
na kiongozi yeyote aliyeko karibu.Huu mwenge wangeurudisha juu ya mlima kilimanjaro
wauache uzimikie huko.
 
Kipi cha maana, wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji au kwenda kukaa mabarabarani kutwa na kupiga miayo wakisubiri mwenge na kisha waanze kukata viuno hadharani?
 
tangu nizaliwe wanainchi wanachangia mwenge lakini sijawahi kuambiwa wamepata bilioni ngapi kwenye michango hiyo.
 
By the way, hivi huu mwenge upo kisheria? Kwa sheria ipi au namba ngapi na ya mwaka gani?

Kama hakuna sheria yoyote basi kuukimbiza (eti kukimbiza ha ha ha ha) ni sawa na uwendawazimu wa mchana kweupe and Nasari is right.

Otherwise, kama unalindwa na sheria yoyote, the MP must be careful na hoja zake kwa wananchi.
 
Tunawasha mwenge na kuukimbiza nchi ili kuwamulikia mafisadi waone madini,mbuga za wanyama,misitu na mashamba makubwa yalipo.Hivi miradi haiwezi kuzinduliwa na kufanya kazi mpaka tulete moto?nampa big up Dogo Janja,hatuwezi kupoteza muda na fedha kufanya mazingaombwe ya kukimbiza moto!Na hili linawezekana mfano halmashauri ya karatu tangu iwe chini ya CDM walipiga marufuku moto wa mazingaombwe na haujawahi kwenda huko.
 
Back
Top Bottom