Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
WAKILI STEPHEN BYABATO(MB) MGENI RASMI MKUTANO WA CCM BUKOBA MJINI.

Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Stephen Byabato tarehe 12 Machi, 2023 alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukoba Mjini.

Kupitia Kikao Hicho Mhe. Byabato Alizungumzia Kuhusu Miradi Mbalimbali inayoendelea kutekelezwa, Pia aliendelea kuisemea baadhi ya Miradi iliyokamilika, na itakayotekelezwa kufikia mwaka 2025.

"Kuhusu Stendi Kuu, Mkandarasi atasaini Mkataba, kwa kianzio cha Bilioni Moja na muda si mrefu ataingia eneo la mradi kuanza kazi ya ujenzi".

Aidha Mhe. Byabato Aligusia swala la Maji katika Mji wa Bukoba na kuwaomba Shirika la Maji (BUWASA) wapunguze gharama kwa Wananchi katika ulipaji ili huduma ya Maji ipatikane.

"Kuhusu Maji Kwa Bukoba Mjini Sio Shida, Nimewaomba Wenzetu wa BUWASA wapunguze Gharama Au Waje na Mpango wa kulipia Kidogo kidogo uku wananchi wakiendelea kuunganishiwa Maji, Zile Kata tano zilizokuwa zimebaki na changamoto ya Maji ambazo ni Buhembe, Kahororo, Kashai, Nshambya na Nyanga tunakwenda kuziunganishia huduma ya Maji. Imetengwa Bilioni 3 kwa ajili ya mradi huo na 80% ya fedha imeshaletwa".

Pia alisema "Katika kipindi cha Miaka miwili, Bukoba Mjini tumepokea zaidi ya Bilioni 4 kwa Elimu ya Sekondari na Elimu ya Msingi. Fedha hii imetoka kwa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan"

Aidha alisema "Watu wa Musira Kata ya Miembeni ile Boti yetu tuliyoiahidi ili kusaidia Usafirishaji, Mashine inafungwa Wiki ijayo".

Mwisho Alisema "Sisi viongozi wa Chama na Serikali tumekubaliana kwa pamoja HATUTOGOMBANA"

WhatsApp Image 2023-03-13 at 08.52.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-13 at 08.51.59.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-13 at 08.52.00.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-13 at 14.41.08(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-13 at 14.41.06(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-13 at 14.41.06(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-13 at 14.41.07(1).jpeg


#ByabatoKazini.
#JimboLetu.
#KaziIendelee.
 
Mimi nataka stendi basi...nitampa kura 2025...

Ile stendi haifai kabisa
na soko mbona kama haliko!stendi ni danganya toto ni bora asingeitamka lkn sababu wanasiasa wanatafuta kiki basi tumwache.yetu macho 2025 panapo majaliwa.ninavyoijua bukoba na watu wake sisemi.
 
Ajitahidi umeme uende vijijini, vijijini hakuna umeme REA ilikwama yeye ndiye Naibu waziri wa umeme
 
Back
Top Bottom