MESTOD
JF-Expert Member
- Nov 12, 2010
- 4,798
- 2,004
Swali zuri mno, kwamba imedhihirika wote bilankujali chama ni watu wasioweka mbele maslahi ya Taifa? Na hapa si wale wa CCM tu hapana, na vyama vyote! Tufanyeje tulio wanyonge? wapi kimbilio letu? Ni swali gumu mno.
Wewe mawazo yako yepi, tufute bunge? Katiba mpya iseme wabunge walipwe kima cha walimu? Dhana kubwa hapa ni watu kuwajibika ili taifa hili liendelee. Uadilifu na uwajibikaji wa mtu ni muhimu sana kuliko chochote. Kama bunge likiwa la waadilifu, litasimamia maslahi ya nchi na kuwawajibisha wafujaji.
My take, uadilifu wa wabunge hautapimwa kwa udogo wa mishahara, bali kuisimamia serikali na kuona inawajibika ipasavyo kwa wananchi.