Mbunge Mwakilishi wa Wafanyakazi nchini ampongeza Rais Samia kwa kujali Maslahi ya Watumishi nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Viti Maalum Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate kufuatia Sikukuu ya Mei Mosi iliyofanyika Kitaifa Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro amempongeza Rais Samia kwa kutoa hotuba iliyozidi kuleta matumaini mazuri kwa wafanyakazi wote nchini.

Mhe. Janejelly James Ntate amesema Rais Samia amekuwa kiongozi mzuri wa kuigwa kwani amefanya maslahi ya wafanyakazi nchini kuwa kipaumbele kwake huku akisema "Uadilifu na Ueledi Kazini Ndilo Chimbuko la Maisha Bora kwa Wafanyakazi"

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Mkoani Morogoro amewaambia Wafanyakazi kuwa kuanzia mwaka huu zile nyongeza za mishahara za kila mwaka ambazo zilisitishwa kwa muda mrefu, zinarudi tena.

“Katika yote yaliyotajwa mwaka jana ikiwemo uundwaji wa Mabaraza ya Taasisi 40 za Umma, kulipwa mafao kwa wakati kwa wastaafu na waliondokewa kazini kwa vyeti feki, kupunguzwa kiwango cha kodi ya mapato ya PAYE kutoka 9% hadi 8% na kuongezeka kwa mshahara na mliomba kuondoa tozo kwenye mihamala kibenki, kupandisha madaraja ya Watumishi, kuongezwa umri wa Mtoto kuwa Mwanachama wa NHIF. Mambo yote mliyoyataka mwaka jana Serikali imetekeleza kwa 95% Wafanyakazi ni Mashahidi sehemu ndogo iliyobaki Serikali inaendelea na utekelezaji” - Rais Samia

Rais Samia amesema Serikali imelichukua suala la maombi ya Walimu kulipwa posho (Teaching Allowance) na inalifanyia kazi. "Tumelichukua tutakwenda kuliangalia uwezo wa Nchi halafu tuone tutafanya nini?” - Amesema Rais Samia

Mhe. Janejelly James Ntate amezidi kusisitiza wafanyakazi wote nchini kuiishi Kauli mbiu ya Mama Samia ambayo inasema "Uadilifu na Ueledi Kazini Ndilo Chimbuko la Maisha Bora kwa Wafanyakazi" ili kuendelea kufanya kazi kwa weledi, bidiii, kujituma, uaminifu, ubunifu na kuzidi kulijenga Taifa

Mwisho, Mhe. Janejelly James Ntate amesema yeye kama mwakilishi wa wafanyakazi bungeni yupo tayari kutumwa ajenda zozote zinahusu maslahi ya wafanyakazi kwani ndilo jukumu lake kubwa la kumchagua kuwa mbunge kwa ajili ya kuwasemea

Kauli Mbiu: Mishahara Bora na Ajira za staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi, Wakati ni Sasa!

WhatsApp Image 2023-05-02 at 11.54.30.jpeg
FvCdz_GWcAUgB9v.jpg
FvC2d3xagAIn5Lh.jpg
FvCYhDuXwAAGBwr.jpg
 
Back
Top Bottom